Spika Ndugai anasema hawezi kuwafukuza bungeni Wanawake kwa maana dunia itamshangaa; lakini hashangai Serikali kuwafukuza shule wanawake

Spika Ndugai anasema hawezi kuwafukuza bungeni Wanawake kwa maana dunia itamshangaa; lakini hashangai Serikali kuwafukuza shule wanawake

Huyo ndugai anajitekenya mwenyewe.. Halima na wenzake siyo wabunge kwa mujibu wa katiba ya nchi kwa sabb chama chao kimesha wavua uanachama.

Mwaka 2017 Sophia Simba alipovuliwa uanachama na CCM huyo huyo ndugai alikuwa spika, mbona hakumkingia kifua? Au Sophia siyo mwanamke?!

Kama hataki kuheshimu Katiba ya nchi aliyoapa kuilinda, hafai kuendelea kuwa spika
Alivyokua mjinga anadhan anawakomoa chadema, kumbe anaikanyaga katiba
 
Nafikiri kuna shida mahali. Naomba nimpe ushauri Ndugai.
  1. Jambo la kwanza akatae kupokea barua toka Chadema ya kuvuliwa uanachama wabunge 19.
  2. Ashauriane na Mwanasheria mkuu wa serikali na alete muswada wa dharura wa kubadili kipengele kinachotumiwa na Chadema katika kuwatimua
  3. Kikao kijacho cha bunge mswaaada uwe tabled na upitishe na uanze kutumika mara moja.
Bila hivyo kila siku atajichanganya tu!!
We ni mjinga suala la mbunge kuwa mwanachama lipo kikatiba, kubadilisha kipengele ni kuifanyia katiba mabadiliko

Chadema kazi yake ni kuwapa taarifa tume na spika, sio kazi ya spika na tume kuwapangia nin Cha kufanya chadema
 
"Naagiza Halima popote alipo aje haraka sana mbele ya kamati ya maadili na ikibidi ataletwa hata kwa pingu" punde si punde mtetezi wa wanawake hasa mtetezi wa Halima Mdee na wenzake 18 a.k.a Ndugai anamfukuza Halima bungeni kwa mwaka mzima.
Ndo nashangaa na mie hapa, mweeeeh huyu spika ni hovyoooooh kabisa.
 
Wakuu amani iwe nanyi

Mwendelezo wa mtifuano mkali, CCM sasa inamtetea mwanamke kwa kila namna.

Ni hivi: Jana spika Job Ndugai alisema kuwa hawezi kuwafukuza bungeni wale akina mama kwa sababu dunia nzima itamshangaa kwa kuwafukuza wanawake bungeni na hali hiyo itapelekea yeye binafsi kuandikwa katika vitabu vya maajabu ya dunia kama spika wa hovyo.

Ikumbukwe pia kuwa wanawake hufukuzwa shule pindi wapatapo ujauzito na hawaruhusiwi kurudi hata baada ya kujifungua.

Sasa swali: Kwanini spika anahisi ni aibu kumfukuza mwanamke bungeni ila ni sawa mwanamke huyohuyo kufukuzwa shule?
Kufukuza watoto wa kike waliopata mimba kwa kurubuniwa na wanaume wakwere na bodaboda ni kuwanyima haki, si tu ya wao kuja kiuwa wabunge bali hata elimu ya awali ya kulea huyo mtoto atakayetokana na mimba, hii ni dhambi kubwa kuliko kumfukuza mbunge ambaye amevunja katiba.
 
Pole sana swali lako litafaa sana kwenye vigodoro. Hapa ni swala la KATIBA ya nchi JMTz
Mwenyewe unajionaaa una hoooooja
Katiba imefuatwa vizuri ndio maana zile nafasi za ubunge zilitangazwa kwenye gazeti la serikali
 
Mwenyewe unajionaaa una hoooooja
Katiba imefuatwa vizuri ndio maana zile nafasi za ubunge zilitangazwa kwenye gazeti la serikali
Shida imeletwa Mara baada ya chadema kuwatimua uwanachama wale wabunge.Ndugai analazimishwa na katiba kuwatoa nje wale wabunge.nje ya hapo anavunja katiba aliyoapa kuilinda na kuifadhi.
 
Back
Top Bottom