Spika Ndugai ataka Walimu waongezewe kazi wafundishe masomo kuanzia matatu ili kupunguza uhaba wa Walimu

Baadala ya walimu kuongezewa mishahara baada ya kusaidia kuiba kura na kuongoza kura feki vituoni wanaongezewa masomo ya kufundish.duh ama kweli maccm hawana rafiki wa kudumu
 
Kweli huyu ni ndugai, yaani mwalimu afundishe masomo 5? huo mchanganyikano kwenye ubongo wake utakuwa zaidi ya nyungu...ni sawa na kusema kwa sababu wewe tayari ni daktari unaweza pia kufanya kazi za injinia na mwanasheria, aibu nimeona mimi...
 
Kila nikiona mtu kaandika deportivo nacheka mpaka mbavu zinauma.
Anyway huyu Ndugai anyamaze tu. Yeye yupo huko bungeni hamna cha maana anachokifanya na bado analipwa hela nyingi.
Asitukaushe kizazi mfyuuuu
Ukipenda unamalizia kabisa "Deportivo la Coruna"[emoji851]
 
Muheshimiwa speaker mbona unakosa ya kushauri Serikali? Hujui kama kadri mtu anavyokuwa na masomo mengi anapunguza ufanisi? Umeshinda kushauri Wizara na Serikali kulipa mdeni na kupandisha madaraja, unataka Mwalimu mmoja afundishe masomo matatu shule.
Ama kweli, ulishapata wewe. Huoni shida tunazopata walimu, unachoona ni kuwa hakuna kazi tunazofanya.
Kwani hujui kwa kawaida Mwalimu mmoja anatakiwa kuwa na watoto wangapi anaoweza kiwamudu? Inakuwa kama mtu asiyeona? KWA hiyo unataka kusema walimu wanatosha sana tatizo wanafundisha masomo machache!

Hongera sana Job Ndungai, lisimamie hilo, ikiwezekana Mwalimu mmoja afundishe masomo saba (7) hapo tutakuwa tumetatua tatizo.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpatie! Walimu tuna maumivu..... Hilo mnalijua..
 
Wakiongezewa hayo masomo hivyo mwalimu mmoja awe anafundisha madarasa mawili au matatu kwa pamoja?siyo rahisi kama kupiga mtu kwa gongo.
 
Hayo masomo matatu hadi matano ya kufundishwa na mtu mmoja ni masomo gani hayo?

Yani kwa mfano mwl afundishe masomo yafuatayo:

Physics
Geography
Chemistry
Biology
Kiswahili

[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]

Ndugai BURE kabisa.
Ndugai anatakiwa aeleweshwe taratibu kuhusu suala la specialization kwenye taaluma, inawezekana alikimbia umande au alipata elimu ya hapa na pale ya kuunga unga kwa cello tape, msameheni bure..
 
Hivi mazingira ya ulaya na hapa kwetu yanalingana?kea Nini tunapenda kujilinganisha na mataifa makubwa wakati hata Angola wanatuzidi kiuchumi?Ni aibu.
Ni huyo speaker wako analinganisha nchi yetu ambayo tu madawati ni changamoto na nchi ambazo zimeendelea
 
Ndugai, kufundisha somo moja badala ya matatu sio uhaba wa waalimu! Ni uwigo (scope) wa ufahamu wa mwalimu.

Hata hivo uhaba umalizwa kwa kutoa ajira. Kwa namna nyingine anakiri serikali haina uwezo wa kuajiri waalimu wapya. Sasa waalimu watatupiwa hata masomo wasiyowaweza ili mradi kuwe na mtu anajaza nafasi tu!! Pathetic!
 
Nimekua najiuliza wale walimu wangu wa shule za kata ambao notes tuu kuandika ubaoni wanaachiwa wanafunzi wajiandikie

Sijui sijui sijui itakuaje anyaway mitano tena
 
Kauli yake imenikumbusha kombe la dunia ambalo Saudi Arabia walipigwa goli nane, sasa na sisi mpaka jiwe aondoke tutakuwa tumepigwa kumi bila na siyo nane. Nasema Mitano tena...
 
hii hoja Rais Magufuli hawezi kuikubali, mzee wetu Magufuli amefundisha ana uzoefu na kufundisha anajua kwamba haiwezekani mwalimu kufundisha masomo matatu hadi matano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…