Spika Ndugai awaapisha Humphrey Polepole na Riziki Lulida. Asema Bunge linawatambua Wabunge 19 wa Viti Maalum waliofutiwa uanachama CHADEMA

Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Bi Magreth Thacher alupofariki kuna kundi la watu walipita barabarani kusheherekea kifo chake, nilikuwa sijawaelewa lakini sasa nimewaelewa...
Wewe uelewe tu kwamba Mungu ameumba watu wema na wabaya kwa ajili ya kutenda mapenzi yake. Kuna watu wabaya duniani ambao wanaitaji watu wabaya zaidi kwa ajili ya kuwanyoosha ili wawe kwenye msitari.
 
Of course ni kweli bado ni wabunge, taarifa lazima ziende NEC then ndio ziende kwa Spika. Zikifika kwa Speaker akatae tuone.
 
Cha kushangaza ni Ndugai huyohuyo ndio alimfungia Halima Mdee mwaka mzima kutokukanyaga bungeni. Leo eti ana mahaba naye! Kama kuna motoni kweli basi huyu atakuwa kuni.
Ndio siasa! Mbona nyie mlikuwa mko tayari kuua mtu ili mradi kumtetea Mdee ila leo mnamuita mzee?

Pia umesahau ya Lowasa? Haya yanayowapata Chadema ni halali yenu.
 
Ndio siasa! Mbona nyie mlikuwa mko tayari kuua mtu ili mradi kumtetea Mdee ila leo mnamuita mzee?

Pia umesahau ya Lowasa? Haya yanayowapata chadema ni halali yenu

Kachukue nafasi ya Esta bulaya kwa mdee naona kazi imemwelemea
 
Spika Ndugai amesema bunge linawatambua wabunge wote 20 wa chadema
Legally, ataendelea ‘kuwatambua’ mpaka siku CHADEMA wakimuandikia barua Msajiri wa Vyama na yeye akamwandikia Speaker

Kipindi kile cha CUF ya Lipumba Msajiri aliact faster na Ndugai akafuata speed ileile. Nima mashaka kama kwa case hii ya akina Halima kama watakuwa tayari kuharakisha mambo.
 
Ndugai is a donkey and Magufuli is a rider on the fateful journey to utopia.
 
Anayelidhalilisha bunge ni spika mwenyewe kwa kukosa weledi, akili, na busara kubwa za kuiongoza chombo hiki.
Ndugai ni kielelezo tu cha Nchi ilipofikia. Haiwezekani mtu mmoja afanye anavyotaka na Nchi yote ikubali tu kikondoo
 
Kachukue nafasi ya Esta bulaya kwa mdee naona kazi imemwelemea
Kwani mimi niko chadema!?

Mimi ni mwanaume na niko ccm, hizo nafasi za akina Halima ni za nyie wanawake wa huko chadema ndio maana mnapigana vikumbo.
 
Kama CHADEMA ni chama halali cha siasa maamuzi yao yaheshimiwe labda hao wabunge 19 kama watabaki Bungeni kwa idhini ya Spika lakini kama ni kwa mujibu wa sheria ya nchi Chadema imewafuta vyeo wale wote waliokiuka miiko ya chama chao pamoja na kuwafuta uwanachama.

Ni aibu kwa mtu wa chama kingine cha siasa kuingilia maamuzi ya chama kingine kwa sababu tu ana kofia,hizi hizi sheria tunazozipotosha leo kwa ulevi wa madaraka siku za usoni zitatuadhibu hizi hizi pale tutakapokosa kinga.Si vizuri kuingilia kazi za Bunge lakini tuheshimu matakwa ya sheria zetu ambazo ziko kihalali kulinda nchi yetu.

Inasikitisha mtu na elimu yake na umri wake kufanya vitu vya hovyo kisa ana kofia.Tukumbuke kila mmoja anayeapa kiapo haramu siku ya mwisho atakijutia,USIAPE BURE JINA LA MUNGU WAKO.
 
Mbunge anatokana na chama,mbunge kama amekosa sifa na kupoteza sifa za kuwa mwanachama wa chama kilicho mdhamini kuwa mwanachama ,anapoteza nafac ya kuwa mbunge, hilo halitakiwi kujadiliwa.

CCM mwaka 2017 walimfukuza uanachama Sophia Simba,kutokana na utovu wa nidhamu na kwakua alikua Mbunge wa viti maalum, kwakukosa uanachama wa ccm alipoteza nafac yake ya ubunge wa viti maalum na badala yake aliteualiwa mwingine.

Chama chochote cha siasa kina utaratibu ulio ndani ya katiba yake, katiba ndio muongozo wa Chama, na katiba za vyama zipo kwa mujibu wa sheria za nchi .

Ieleweke kwamba Ndugai si sheria na wala hayuko juu ya sheria .
 
Ndugai ni kielelezo tu cha Nchi ilipofikia. Haiwezekani mtu mmoja afanye anavyotaka na Nchi yote ikubali tu kikondoo
Jamaa ni Speaker wa hovyo pengine kuliko yeyote kuwa kutokea duniani.
Hata watoto wadogo wanamdharau
 
Kila la heri wote walioapishwa.Kila la heri Spika Ndugai!!
Maisha yanaendelea!
 
Mbunge anatokana na chama,mbunge kama amekosa sifa na kupoteza sifa za kuwa mwanachama wa chama kilicho mdhamini kuwa mwanachama ,anapoteza nafac ya kuwa mbunge, hilo halitakiwi kujadiliwa..
Spika yupo juu ya sheria.Rejea suala la Cecil Mwambe mbunge wa Ndanda.Kuna watu walijaribu kwenda mahakmani,kama nakumbuka vizuri!
 
Kuna jambo kweli halipo sawa katika Nchi yetu, hivi kweli uvunjifu mkubwa wa katiba uliofanyika Spika wa Bunge anakuja na utetezi mwepesi kiasi hichi.
uvunjifu upi?kipengele kipi kimekiukwa labda ukatuhadithia kidogo
 
Hata ukifungua kesi hakuna haki tena nchi hii maana kila kitu sasa anamuua mtu mmoja
 
Halafu unawatisha vyombo vya habari washindwe kufanya majukumu yao ya kitaaluma katika shughuli zao za kila siku mbona Kikwete ni rais Mstaafu na alitumika na ccm kupiga kampeni, Rais mstaafu wa awamu ya pili alitumia vyombo vya habari kumpigia debe rais wa sasa kuwa rais wa kudumu kupitia vyombo vya habari, Ndugai hayo hukuyaona ili tu waliokutangulia katika kiti hicho ndio wazee?
 
Kama kawaida anaanza kuwatisha.

Wale wamefukuzwa sasa sijui watawakilisha chama gani wakiwa bungeni? Hamna mtu aliyetegemea kuwa Spika atakubali wanyang'anywe ubunge ingawa kwa kufanya hivyo anapingana kabisa na Katiba aliyoapa kuilinda.

Na kama amesema hayo kuhusu wastaafu basi yeye ndiye asiyewatendea haki kwa kutaka kuwanyima haki yao ya msingi ya kutoa maoni yao.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…