Spika Ndugai awaapisha Humphrey Polepole na Riziki Lulida. Asema Bunge linawatambua Wabunge 19 wa Viti Maalum waliofutiwa uanachama CHADEMA

KUHUSU WABUNGE KUAPISHWA GEREJI.

Bashir Yakub, WAKILI.
+256 714 047 241.

Kanuni ya 30( 1 ) ya Kanuni za Kudumu za Bunge za Mwaka 2020 inasema kuwa,

" Kwa kuzingatia Ibara ya 68 ya Katiba, kila Mbunge, kabla ya kuanza kushiriki katika shughuli za Bunge, ataapishwa na Spika mbele ya Bunge Kiapo cha Uaminifu "

Kanuni ndogo ya (2 ) inaendelea kusema kuwa,

(2) Bila ya kujali masharti ya fasili ya (1), endapo Mbunge atachaguliwa au kuteuliwa baada ya Uchaguzi Mkuu, Spika atamwapisha katika:

(a) kikao chochote cha Bunge iwapo kuna Mkutano wa Bunge; au

(b) eneo litakalopangwa na Spika iwapo hakuna Mkutano wa Bunge unaoendelea na baadaye
Spika atatoa taarifa Bungeni kwenye Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Bunge unaofuata.

Kwa hii ( b ) maana yake kama hakuna mkutano wowote wa bunge unaoendelea kwa muda huo, basi Spika anaweza kuwaapisha wabunge eneo lolote atakalopanga . Kanuni iko uchi ksbisa.

Kanuni hii yote ya 30 inatafsiri na kutoa maelezo ya ziada kwa Ibara ya 68 ya Katiba inayotaka Wabunge kuapishwa mbele ya bunge.

Wassalaam.
 
Katiba ndiyo sheria mama, Je, Katiba inatambua m'bunge asiye na chama?

#Tutaelewana
Anapiga domo tu....

Gurudumu la kisheria halijaanza. NEC itapewa taarifa, na kama hakuna zuio lolote, NEC inabidi itangaze hawa 19 wamepoteza sifa za kuwa wabunge na Speaker atapewa taarifa kama alivyopewa za wao "kuteuliwa" na atalazimika kuzifanyia kazi. Hakuna grey area, ni matakwa ya kikatiba.

Sasa hivi yuko sahihi, bado ni wabunge; mchakato bado.
 
Hao wabunge 19 ni wabunge kwa kupitia chama gani?
 
Boss tunasubiri update ya kesi ya vifurushi, sio sawa kuwekewa kikomo cha matumizi wakati tumelipia huduma.
 

Huyu Ndugai ni mwehu tu kama wengine, haya maneno anayo yaongea leo utafikiri sio yeye anayewatukanaga
 
Hiki ndicho tunachohitaji. Swali la nyongeza, palikuwa na haraka gani kiasi hiki wakati kuna mkutano mwingine wa bunge unakuja?
 
Ndugai HIV inazadi kumtafuna ubongo na haufanyi kazi tena. Lakini mtu ana uhuru wa kuamini kuwa marehemu aliyezikwa bado yu hai
 
Spika Ndugai amemuonya Mbowe akiwa kama mwanamme aliyefundwa asirudie tabia ya kutukana na kukemea wanawake hadharani.

Kadhalika amewaonya wale wote wanaowakebehi wabunge 19 wa Chadema na kuwaita Covid 19 waache mara moja.

Na kwamba Chadema ni kampuni ya mtu binafsi.

Jana nilileta uzi wa swali iwapo kuna haja ya Spika Ndugai kumjibu Freeman Mbowe.
Nashukuru Spika ameondoa ule utata wa kanuni ya kiapo.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote!
 
Hajaongea kama Spika ila ameongea kama "Mtumwa" ulishawahi ona wapi mbunge asiye na chama wala hajateuliwa na Rais.
 
Mkuu Bashir Yakub , kwanza asante kwa kutuelimisha, naomba kuuliza, katika kula kiapo, katiba imesema
  1. Kwa kuzingatia Ibara ya 68 ya Katiba, kila Mbunge, kabla ya kuanza kushiriki katika shughuli za Bunge, ataapishwa na Spika mbele ya Bunge Kiapo cha Uaminifu "
  2. Hiki ni kiapo cha uaminifu kwa spika au kwa Bunge?.
  3. Lengo la kiapo ni nini?, kumtumikia Spika au kulitumikia Bunge?.
  4. The significance ya kiapo, ni kuapa mbele ya Bunge au ni anayeapisha?.
My Take.
Mimi navaa viatu vya mtunga katiba, alidhamiria nini wakati aliposema mbunge ataapa mbele ya Bunge?
  1. Kwa vile kazi ya Mbunge ni kufanya kazi za kibunge, Essence ya kiapo ni kuapa mbele ya Bunge kazi ya Spika ni shahidi tuu wa kiapo hicho kufanywa mbele ya Spika, kama ilivyo kuapa mbele ya wakili, hakimu au jaji.
  2. Significance ya kiapo ni kiapo cha uaminifu kwa Bunge, na sio kiapo cha uaminifu kwa Spika!.
  3. Mbunge anaapisha ili kulitumikia Bunge sio ili kumtumikia Spika!,
  4. The role of Spika kwenye kiapo ni muapishaji, hivyo kitu muhimu kabisa kwenue kiapo ni Bunge na sio Spika!.
  5. Hivyo kanuni hiyo imamfanya Spika kuwa muhimu kuliko Bunge, popote Spika anaweza kuamua kuapishia, hivyo kanuni hiyo imempa Spika mamlaka ya kujigeuza Bunge, hivyo sasa wabunge wanaapa tuu mbele ya muapishaji badala ya mbele ya Bunge!.
Kanuni yoyote ikienda kinyume cha katiba inakuwa ni batili, void abinitio!.
P

 
Komrade uliahidi kuachana na siasa, nini kimekusibu? Ahaaaa ila nimeamini kweli jamaa yumo humu.
 
Kwa hiyo ukifukuzwa uanachama bado unaendelea kuwa mbunge, Hivi watalaam wa katiba mpo wapi mbona katiba inakanyagwa mmekaa kimya! Kwanza hao ubunge wameupataje! Watanzania siku mkiamka mjue jua limezama.RIP Jomo Kenyatta.
 
Leo CCM wanawatetea akina mdee, kweli dunia inaenda kasi.
 
Good!
 
Ni uchungu wa kufukuzwa Covid 19 ndiyo unamuuma? Kwenye speech ya Mbowe wapi katukana hao covid zaidi ya kusema dada zangu, mama zangu what happened? Ndiyo tusi na kama amewatukana kama anavyodai atamfanya nini, hana uwezo wowote juu yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…