Bashir Yakub
Member
- May 27, 2013
- 96
- 1,745
KUHUSU WABUNGE KUAPISHWA GEREJI.
Bashir Yakub, WAKILI.
+256 714 047 241.
Kanuni ya 30( 1 ) ya Kanuni za Kudumu za Bunge za Mwaka 2020 inasema kuwa,
" Kwa kuzingatia Ibara ya 68 ya Katiba, kila Mbunge, kabla ya kuanza kushiriki katika shughuli za Bunge, ataapishwa na Spika mbele ya Bunge Kiapo cha Uaminifu "
Kanuni ndogo ya (2 ) inaendelea kusema kuwa,
(2) Bila ya kujali masharti ya fasili ya (1), endapo Mbunge atachaguliwa au kuteuliwa baada ya Uchaguzi Mkuu, Spika atamwapisha katika:
(a) kikao chochote cha Bunge iwapo kuna Mkutano wa Bunge; au
(b) eneo litakalopangwa na Spika iwapo hakuna Mkutano wa Bunge unaoendelea na baadaye
Spika atatoa taarifa Bungeni kwenye Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Bunge unaofuata.
Kwa hii ( b ) maana yake kama hakuna mkutano wowote wa bunge unaoendelea kwa muda huo, basi Spika anaweza kuwaapisha wabunge eneo lolote atakalopanga . Kanuni iko uchi ksbisa.
Kanuni hii yote ya 30 inatafsiri na kutoa maelezo ya ziada kwa Ibara ya 68 ya Katiba inayotaka Wabunge kuapishwa mbele ya bunge.
Wassalaam.