Spika Ndugai awaapisha Humphrey Polepole na Riziki Lulida. Asema Bunge linawatambua Wabunge 19 wa Viti Maalum waliofutiwa uanachama CHADEMA

Spika Ndugai awaapisha Humphrey Polepole na Riziki Lulida. Asema Bunge linawatambua Wabunge 19 wa Viti Maalum waliofutiwa uanachama CHADEMA

Kwamba wakati Sophia Simba alipofukuzwa Uanachama ccm ndiyo press pekee ambayo alitakiwa kukifanyia kazi?
Bahati nzuri au mbaya danadana zote hizi ni rejea za baadae kwa watakaokua hai. Mbowe na timu yake najua wanazo pesa za kula kwa miaka kidogo ila anaemruhusu Job Ndugai kutumia mamlaka ya uspika kukeuka taratibu tulizojiwekea kama nchi kwenye katiba yetu siyo afya njema kwa watoto wetu na bali siyo kuwakomoa CHADEMA.
CHADEMA ni jina tu.
Ndio hivyo mkuu.... mimi sijatunga katiba wala kugawa majukumu. Ukiona kuna taasisi haifuati sheria na katiba, unaruhusiwa kwenda kushitaki. Lakini ukweli ndio huo. Mchakato wa kufukuza Mbunge sio mwepesi tu kama kuita press conference.

Tuna tabia ya kuchukulia vitu poa, ndicho kilichowaponza kina Maalim Seif na kujiuzuru kwa Lipumba. Mtu kaandika barua, wao hawakuifanyia kazi. Kesho kaandika barua barua kutengua ile ya kwanza, wanaanza ku-panic.

CHADEMA wamemaliza kikao Ijumaa, weekend inatosha kabisa kuandaa barua rasmi kwenda kwa hao COVID 19, na kwenda kwa Tume kuitaarifu kuwa kikao cha kamati kuu kimewavua uanachama hao watu. Then waone Tume itafanya nini, kama ikishindwa kuchukua hatua stahiki wafuate taratibu za kisheria.
 
Mkuu Bashir Yakub , kwanza asante kwa kutuelimisha, naomba kuuliza, katika kula kiapo, katiba imesema
  1. Kwa kuzingatia Ibara ya 68 ya Katiba, kila Mbunge, kabla ya kuanza kushiriki katika shughuli za Bunge, ataapishwa na Spika mbele ya Bunge Kiapo cha Uaminifu "...
Umeuliza na kujibu mwenyewe , ahsante kwa maelezo yako.
 
Ha ha ha, hapo lazima mzee mzima ulegee - watoto 19 wakali wote wa wako! Naona Mdee ndiyo anamyong'onyeza kabisa mzee shingoni.

Yaani hata mie ninge calm down
 
Bidada mi sina stress hata huyo Kayafa wenu akitawala 40 years consecutively (japo hawezi toboa maana mdudu kamchakaza)...
Aah kumbe ndiyo wewe uliyeolewa na basha la kibeberu huko Ulaya!! Endelea huko huko wala hatukuhitaji hapa TZ!! Tabia hiyo watz hatuhitaji kabisa ndiyo maana Lissu Amsterdam amechemsha!
 
Mkuu Bashir Yakub , kwanza asante kwa kutuelimisha, naomba kuuliza, katika kula kiapo, katiba imesema
  1. Kwa kuzingatia Ibara ya 68 ya Katiba, kila Mbunge, kabla ya kuanza kushiriki katika shughuli za Bunge, ataapishwa na Spika mbele ya Bunge Kiapo cha Uaminifu "...
Nadhani watu tunapata tabu kuona tofauti ya Shule na Jengo la Shule, Mahakama na Jengo la Mahakama, Kanisa na Jengo la Kanisa, Bunge na Jengo la Bunge.

Mara nyingi hivi vitu ni conceptual zaidi ya literal. Shule inaweza kuwa hata chini ya mpapai, na ikaitwa shule. Kwa wenye kumbukumbuku sawasawa, kwenye kesi ya mauaji iliyokuwa inamkabili Zombe, mahakama iliahamia kwenye msitu wa Pande, unaweza kusema ni batili kisa haikuwa kwenye jengo la mahakama kuu? Hapa Bwana Mbowe alikuwa too literal.
 
Heshima ya chombo muhimu cha kutunga sheria kwisha kabisa
 
MKuu kwa kejeli hizi huwasaidii Chadema bali unawapoteza. Ulitakiwa, ninavyodhani, uwape maelekezo wafungue kesi ya kikatiba ama ya aina yoyote ile na inyofaa kuhoji na kupinga utekelezaji wa shughuli za bunge chini ya Mheshimiwa Spika Ndungai. Ni hayo tu!
Wewe nae unachekesha wafungue kesi kwenye mahakama hipi hapa Tanzania
 
Bunge linawatambua au spika ndio anawatambua ? , bunge ndio limesema au spika ndio amesema ?
 
Nafasi kumi alizopewa Rais na Katiba ya JMT ni kama katika wabunge waliopo hakuna mtu ana sifa anazotaka lakini sio mbunge ndio anateua sasa huyu wetu anateua watu wa ovyoovyo ili kujaza makasuku kule mjengoni shida
Kumbuka Chadema kwa chaguzi zote za serikali kuu zilizopita wamekuwa wakipeleka bungeni viti maalumu wake zao,mahawala zao,washikaji zao,dada zao,mama zao na hata kwa kuuza nafasi hizo kwa waliofika dau.

Sasa walitegemea safari hii mchezo huo ungeendelea ghafla umeyeyuka wamepaniki hatari .Poleni sana haitotokea tena bahati hiyo kujirudia ni ngumu sana Kama ngamia kupenya kwenye tundu la Sindano
 
Mi ningekuwa ndo Ndugai, hawa ningewaapishia kwenye Car Wash kabisa ili ma-CCM wenzangu yaseme "...Si mnaona tuliwaambia hakuna kifungu kilichovunjwa pale... eti Mbowe alikuwa anahoji akina Mdee kuapishwa garage, si mnaona akina Polepole hao wameapishiwa kwenye carwash!

Amini usiamini... kuwa mwana-CCM raha sana! Yaani huumizi kichwa!!!
Acha kukejeli wewe,usijitoe ufahamu kwa posho mnazopewa na Mbowe kwenda mitandaoni kutetea maamuzi ya kikundi Cha wahuni(kamati kuu ya Chadema) yakiongozwa na jemedari mchumia tumbo Mbowe/Yuda
 
Huku ni kuongeza gharama za bure, si wangeapishwa pamoja na wale COVID- 19 leo.
Bilashaka hata mama yako, shangazi yako, Bibi yako, dada yako nao jina lao ni Covid 19 .Kumbuka hao nao ni wanawake
 
Nafasi kumi alizopewa Rais na Katiba ya JMT ni kama katika wabunge waliopo hakuna mtu ana sifa anazotaka lakini sio mbunge ndio anateua sasa huyu wetu anateua watu wa ovyoovyo ili kujaza makasuku kule mjengoni shida
Yani anayekufaa wewe unadhani anafaa kwa kila mtu? Fikiria nje ya box lako mkuu
 
Back
Top Bottom