Spika Ndugai awapongeza Wakenya kwa kuonesha mubashara Vikao vya Kamati vya Bunge

Sasa hii ndio maana ya ile kauli "kuuma na kupuliza"
 
Hivi watu huu unafiki wao huwa wanaufanyia tathmini au ndio wameweka mbele matumbo yao tu!!?
 
Asiyejua maana ya unafiki ndio huo, anajisikiaje kusifu bunge live la Kenya wakati nchini kwake amezuia.
Hapo chacha yani kuna watu mshipa wa aibu ulishakatika siku nyingi sana
 
Hiyo ni sawa na kwenda kumsifia mke wa mwenzio kuwa akivaa suruali anapendeza sana, lakini hutaki wakwako avae kwani unasema ni vazi la kihuni.
[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Lord have mercy on him.
 
Anawapongeza wanaume!!
 
Mnafiki mkubwa. Bongo mbona wanajifungia chumbani. Gizani! Na yeye na naibu spika wanaweweseka tu
 
Jamani, tusibadirishe historia; hivi ni yeye (spika ) ndiye aliyetaka bunge lisiwe live? Tusije kumuonea mgogo wa watu
Dola inaundwa na mihimili mi3 inayojitegemea.

1.Serikali
2.Bunge
3.Mahakama

Kila muhimili una kiongozi wake na maamuzi yake,kwa Bunge Kiongozi mkuu ni Speaker yeye ndio anayeamua liendeshwe vipi,Waziri alitaka lisiwe live kisa ni gharama lakini kuna baadhi ya vyombo vilitaka kuonyesha bure lakini vikakatazwa,yeye kama speaker ilitakiwa aseme kitu na yeye ndio angeamua kama serikali haina uwezo wa kuendesha basi mimi kama spika naruhusu vyombo binafsi virushe bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…