Spika Ndugai awataka wabunge wajenge nyumba Dodoma kwani hata wabunge wa Kenya wote wana nyumba Nairobi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Spika Ndugai amewataka wabunge wafikirie kujenga nyumba jijini Dodoma badala ya kutegemea nyumba za kupanga.
Ndugai amesema hayo baada ya wabunge kudai TBA inawasumbua kuhusiana na mikataba yao ya upangaji na kuliomba bunge liwasaidie.

Spika Ndugai amewaambia wabunge wanapaswa kujenga nyumba Dodoma kwani ni mahali pazuri na kwamba hata wabunge wa Kenya wote wamejenga nyumba zao Nairobi na wabunge wote wa Uganda wanamiliki nyumba Kampala.

Ndugai amemalizia kwa kushauri kwa sababu bunge linavunjwa June 19 na wabunge wote watalipwa kiinua mgongo kizuri sana basi wamwone waziri Jaffo au Lukuvi wawape viwanja na kujenga nyumba haraka kwani kwa mbunge Dodoma ni second home.

Source Star tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Huyu naye! Ana uhakika wabunge woooooote, waliopo kwenye Bunge hili, wataendelea kuwa wabunge kwenye Bunge lijalo? Au, siku zote wataendelea kuwa Wabunge?
 
Kwani ubunge ni kazi ya kudumu aseme wabunge wajenge nyumba Dodoma? Halafu wakati hamna vikao vya bunge hiyo nyumba nani akae? Halafu mtu akihamia Dodoma waanze kuja na kauli za kutelekeza jimbo?
 
Bwashee Dodoma ni mahali pazuri kuishi!
 
Kwanini Bunge lisijiongeze na kujenga Hostel zake za kisasa, kwani vikao vya Bunge huchukua muda gani? CCM hawashindwi kitu - kama Ndungai anaona TBA wanawazingua hawa walinzi na watetezi wa serikali, wanaweza jiongezea posho ya kupanga Lodge au Hotel, kama ilivyo sitting allowance.
 
Hapo sio jiji la kibiashara kama Nairobi au Kampala

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom