Spika Ndugai awataka wabunge wajenge nyumba Dodoma kwani hata wabunge wa Kenya wote wana nyumba Nairobi

Spika Ndugai awataka wabunge wajenge nyumba Dodoma kwani hata wabunge wa Kenya wote wana nyumba Nairobi

Spika Ndugai amewataka wabunge wafikirie kujenga nyumba jijini Dodoma badala ya kutegemea nyumba za kupanga.
Ndugai amesema hayo baada ya wabunge kudai TBA inawasumbua kuhusiana na mikataba yao ya upangaji na kuliomba bunge liwasaidie.

Spika Ndugai amewaambia wabunge wanapaswa kujenga nyumba Dodoma kwani ni mahali pazuri na kwamba hata wabunge wa Kenya wote wamejenga nyumba zao Nairobi na wabunge wote wa Uganda wanamiliki nyumba Kampala.

Ndugai amemalizia kwa kushauri kwa sababu bunge linavunjwa June 19 na wabunge wote watalipwa kiinua mgongo kizuri sana basi wamwone waziri Jaffo au Lukuvi wawape viwanja na kujenga nyumba haraka kwani kwa mbunge Dodoma ni second home.

Source Star tv

Maendeleo hayana vyama!
KUMBE!
 
Kwanza ubunge ni miaka mitano na siku za kukaa bungeni kwa Mwaka hazizidi siku 120
Hivyo sio afya kujenga nyumba utakayoishi siku 120 kwa Mwaka

Pili miji huendelea kutokana na shughuli za biashara malazi, chakula, starehe, n.k pale mbunge anakuwa na nyumba in amaana atakula nyumbani, atalala nyumbani hivyo mahoteli na migahawa haitapata walaji hivyo Kodi Ajira zitapungua.

Unapowashawishi wajenge maana yakeunataka wahamie Dodoma hata baada ya kustaafu ubunge kitu ambacho sio afya kwa maendeleo ya miji na majiji. Watu warudi kwao baada ya kipindi Cha ubunge na utumishi kuisha.

Bank zimeruhusiwa kujenga jengo la makao makuu tu huko kwengine wanatakiwa kupanga, unafiriki bank wangepewa mwanya wajenge wenyewe nini kingetokea?
 
Spika Ndugai amewataka wabunge wafikirie kujenga nyumba jijini Dodoma badala ya kutegemea nyumba za kupanga.
Ndugai amesema hayo baada ya wabunge kudai TBA inawasumbua kuhusiana na mikataba yao ya upangaji na kuliomba bunge liwasaidie.

Spika Ndugai amewaambia wabunge wanapaswa kujenga nyumba Dodoma kwani ni mahali pazuri na kwamba hata wabunge wa Kenya wote wamejenga nyumba zao Nairobi na wabunge wote wa Uganda wanamiliki nyumba Kampala.

Ndugai amemalizia kwa kushauri kwa sababu bunge linavunjwa June 19 na wabunge wote watalipwa kiinua mgongo kizuri sana basi wamwone waziri Jaffo au Lukuvi wawape viwanja na kujenga nyumba haraka kwani kwa mbunge Dodoma ni second home.

Source Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Kwa Wabunge hubadilika, mimi ningeshauri kila Halmashauri / Jimbo la uchaguzi lipewe kiwanja lijenge nyumba kwa ajili ya kumpangishia Mbunge wake na hiki kitakuwa ni chanzo cha mapato cha kudumua kwa halmashauri husika,
 
Back
Top Bottom