Spika Ndugai, Baadhi ya wanawake wakipewa cheo kazi yao inakuwa ni kufoka na kuweka watu ndani

Spika Ndugai, Baadhi ya wanawake wakipewa cheo kazi yao inakuwa ni kufoka na kuweka watu ndani

Dodoma. Spika wa bunge, Job Ndugai amewataka wanawake wenye mamlaka kutotumia vyeo vyao vibaya.

Spika Ndugai amesema mtu akipewa mamlaka halafu akaanza kuvimba na kushurutisha kwa kuwaweka watu ndani kwani kunawaondolea sifa ya kuwa viongozi.
Bila kuwafokea Wadanganyika hawafanyi kazi!! Huoni sasa siku hizi ukienda maofisini yamerudi mambo yale yale ya zamanii ya kulembua macho ofisini badala ya kuwahudumua wananchi; wanajua hakuna lolote litakalowafaya wawajibike!!
 
Anyway ujumbe umefika Shinyanga ila hao Wabunge wa Uviko19 unaowakumbatia inakuwaje.

Kosa la Sophia Mjema ni lipi? Kuwahimiza watendaji kufanya kazi yao vizuri kama ilivyoagizwa ili kufikia malengo?

Ndugai kwanini anawashambulia kina mama viongozi ili hai kulikuwa na wanaume viongozi kama Bashite enzi ya mwendazake waliofanya mabaya na yeye aliufyata mkia wake na hakusema lolote? Ndugai amekuwa mbunge wa Kongwa kwa miongo mingi na hakuna la maana alilofanikisha isipokuwa kupiga bakora wapinzani wake!

Tuanaushahidi kuwa bila viongozi kuwa wakali mambo yetu hayaendi; hivyo kuna kila sababu ya viongozi kuwa wakali lakini watumie haki na WASIUE!!!
 
Nasikia huko Karagwe kuna watu wamewekwa ndani kwa amri ya DC, eti wameshindwa kulipa hela ya mizinga ya nyuki.
Je kama nyuki hawakuweka asali!
 
Aliyemuhukumu mbowe na kuiaminisha Dunia kuwa mbowe Ni Gaidi na ushahidi wanao wa kutosha Ni nani?

Anayepelekea kupindishwa kwa sheria katika kesi hiyo Ni nani?

Aliyetoa hongo ya madaraka baada ya kuona hyo kesi inakaribia kupigwa chini Ni nani?

Kifupi Hangaya ndiye anayelazimisha kumfunga Mbowe! Acha maCCM mtafunane , ila ukwel uko wazi kwa Kila mwenye akili!

Huyo Hangaya msimtetee, yeye ndiye anayewapa viburi wanawake wengine aliowapa mamlaka!
Anawadharau sana wanaume
 
Kwa hiyo Ndugai ameamua kumvua nguo chifu Hangaya?

Maana hizo ndio sifa zinazomgusa moja kwa moja mama maushungi.
Kuna mwingine mkuu wa mkoa wa Shinyanga anashurutisha taratibu za manunuzi zisifuatwe ili kuwahi pesa alizopewa zisirudishwe hazina. Et afisa manunuzi anasimamishwa kazi hadi miradi inayohusu pesa hizo iishe ndio arejee kazini!!!

Kumbe serikali inatumia kodi za wananchi kulipa watu wasio fanya kazi pasipo sababu za msingi kisa chuki tu dhidi ya mtu kusimamamia sheria, kanuni na taratibu za manunuzi?
 
Viongozi wafuate utaratibu sheria,ukali wawafanyie Wake/Waume zao majumbani ndugu.

Kwa sisi wabongo kufuata sheria na taratibu hakutoshi viongozi lazima wajiongeze na ukali!! Bila hivyo hatuendi.
 
Kwa sisi wabongo kufuata sheria na taratibu hakutoshi viongozi lazima wajiongeze na ukali!! Bila hivyo hatuendi.
Nchi haiendeshwi kwa ukali inaendeshwa kwa kufuata Katiba na Sheria,
kama unaona ukali unafaa mswaada upelekwe Bungeni ili Ukali ufanywe sheria, ili kuwapiga makofi watendaji wa Serikali Nchi haiendeshwi kwa hisia Ndugu.
 
Back
Top Bottom