Spika Ndugai hana mamlaka ya kupinga maamuzi halali yaliyofanywa na Kamati kuu ya CHADEMA

Awamu hii hawafuati sheria za nchi, usijisumbue, wanajua vizuri kabisa wanavunja sheria lakini hawajali, msijichoshe kupigia mbuzi gitaa, muhimu tuombe kama taifa siku ziende haraka mwisho wao ufike waondoke, au Mungu akipendezwa awapende zaidi mapema.
Siku ziende waondoke haraka?.Umeshasema kuwa hawafuati sheria za nchi lakini still bado unaamini kuwa watatoka.Binafsi sidhani,labda kama wamejipangia sheria za kuzitii na za kuzisigina.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Sasa utaiacha CCM umchague nani nchi hii ? Hivyo vyama vya kuunga mkono ushoga na kuuza nchi ndio tuvichague ? Endelea kijifariji humu lakini kumbukeni hiyo EU haiwezi kuwaweka wapinzani madarakani.
Ile siku bwana mdogo Ndugai anamuapisha Polepole lakini anaongelea mambo ya Chadema na kusema kuna "unyanyasaji wa kijinsia" akiwatumia akina Halima Mdee kama Mfano. Halima anafanya press yake na kusema Chadema hakuna mfumo dume kama inavyoelezwa, maana wao wamekuwa viongozi huko. Ndugai anajionaje?
 
Refer mwaka 2017 wakati CCM inamvua ubunge Sophia Simba, akiwa Mwenyekiti wa kina mama hapo hapo mbunge wa viti maalum, ubunge wake ulikoma pale pale, CCM ilipotangaza kumvua uanachama.

Kwanini hivi sasa Spika Ndugai afanye vinginevyo, wakati Chadema ilipofanya vivyo hivyo kwa kikao chake cha Kamati Kuu kuamua kuwavua uanachama wabunge wake wa akina Halima Mdee?
Na ndugayi huyu huyu ndo alikuwa spika wakati huo!
 
Nimeshangazwa sana na kauli aliyotoa Spika Ndugai hivi leo, wakati akiwaapisha wabunge wapya Humphrey Polepole na yule mwanamama Riziki Lulida, kuwa wabunge wa kuteuliwa na Rais katika zile nafasi zake 10 alizopewa kwa mujibu wa Katiba

Spika Ndugai amenukuliwa akisema kuwa hatambui maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu ya Chadema na akaendelea kusisitiza kuwa ataendelea kuwatambua wabunge hao 19 aliowaapisha wiki iliyopita kuwa ni wabunge halali!

Nimkumbushe tu Spika Ndugai kuwa yeye analazimika kuongoza Bunge lake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977

Katiba hiyo katika ibara ya 71(1)(e) inasema kama ifuatavyo nanukuu:-

Ibara ya 71(1)
Mbunge yeyote atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake litokeapo lolote kati ya yafuatayo.

Ibara ya 71(e)
Ikiwa Mbunge huyo atakoma kuwa mwanachama wa chama cha siasa alichokuwemo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge.

Katiba ya nchi yetu haina wagombea binafsi, sasa tumuulize Spika Ndugai anaposema kuwa ataendelea kuwatambua wabunge hao waliuvuliwa uanachama wao na Chadema, atawatambua wakiwa ni wanachama wa chama gani?

Sasa sielewi Spika Ndugai anaposema kuwa hao wabunge wa viti maalum wa Chadema wataendelea kuwa wabunge, anasimama katika Ibara ipi katika Katiba hii ya nchi?

Wenyewe tumeisoma Katiba ya nchi na ipo wazi sana katika suala hili.

Nimkumbushe tu Spika Ndugai kuwa hii siyo Mara ya kwanza kwa chama cha siasa kufukuza wanachama wake na Bunge hilo likatii maamuzi hayo ya Chama, kwa kuwa ndivyo inavyotakiwa kwa mujibu wa Katiba.

Mwezi March 2012, Chama Cha Mapinduzi kiliwafukuza wanachama wake 12 na miongoni mwao alikuwemo, Sofia Simba, aliyekuwa Mwenyekiti wa wanawake, ambaye pia alikuwa ni mbunge.

Kilichofuata ni huyo Sophia Simba kuvuliwa ubunge wake, kwa kuwa lilikuwa ni sharti la Kikatiba.

Mwezi July 2017, Kikao cha Kamati Kuu cha CUF kiliwavua uanachama wao wabunge wanane wa chama hicho.

Vile vile Bunge hilo lilitekeleza Mara moja na kuwavua wabunge hao, ubunge wao kwa kuwa ni kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Sasa swali linakija ni kwanini chama cha Chadema kilivyotekeleza sharti hilo la Kikatiba, Bunge hilo hilo liwe na maamuzi tofauti?

Hii double Standard ya utekelezaji wa sheria inatokana na nini?

Nimalizie kwa kusema kuwa Spika Ndugai hana mamlaka yoyote ya kikatiba ya kuingilia maamuzi yaliyofanywa na chama cha kisiasa kinachotambulika kihalali na msajili wa vyama vya siasa.

Anachofanya Ndugai ni kuiingiza nchi hii katika mgogoro mkubwa wa Kikatiba ambao haujawahi kutokea katika siku za nyuma.

Kwa maana hiyo watanzania wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa tunapaswa kumkemea kwa nguvu zetu zote huyu Spika Ndugai, kwamba anaipeleka nchi hii na kuitumbukiza shimoni
Hao ni wabunge wake na CCM yake
 
Ebu nikuulize kwanza, hivi Katibu Mkuu wa Chadema Bwana John Mnyika ameishamwandikia barua rasmi Spika wa Bunge kuhusu kuwafukuza uanachama akina Mdee?
 
Issue siyo Katibu Mkuu wa Chadema kuandika barua, suala ni yeye Spika wa Bunge kuonyesha dhahiri anawabeba hao wabunge waliofukuzwa na chama chao cha Chadema, kwa kusema hadharani kuwa hatambui maamuzi hayo yaliyofanywa na Chadema

Ina maana kuwa Katibu Mkuu wa Chadema aandike barua au asiandike, tayari Spika wa Bunge keshatoa msimamo wake kwa kuvunja Katiba ya nchi ambayo inaeleza wazi namna mbunge anavyoweza kupoteza nafasi yake ya ubunge
 
Issue siyo Katibu Mkuu wa Chadema kuandika barua, suala ni yeye Spika wa Bunge kuonyesha dhahiri anawabeba hao wabunge waliofukuzwa na chama chao cha Chadema, kwa kusema hadharani kuwa hatambui maamuzi hayo yaliyofanywa na Chadema
Dah!
 
Back
Top Bottom