Spika Ndugai haya uliyosema kuhusu Wabunge wa CHADEMA waliofukuzwa mbona mwaka 2017 hukuyasema wabunge wa CUF walipotimuliwa?

Spika Ndugai haya uliyosema kuhusu Wabunge wa CHADEMA waliofukuzwa mbona mwaka 2017 hukuyasema wabunge wa CUF walipotimuliwa?

Kama Nape Nnauye atakomaa nao lazima watatolewa nduki bungeni.

Nyuma ya Nape kuna nguvu kubwa isiyoonekana ambayo imeapa kuvisambaratisha vikaragosi vyote vya naniliu!
Mimi naamini Mama yuko nyuma ya Nape na watu wasidhani hawa jamaa walioamua kufunguka wanakurupuka, bali wajue wana support kubwa tu ya watu wazito katika chama na serikali.
 
Bila aibu wala kuona soni unadiriki kusema kuwa ili uamini kuwa hao akina Mdee na wenzake 18 lazima upewe muhtasari wa kikao kilichowafukuza? Mbaya zaidi unaongea bila aibu kuwa ili wewe upate uthibitisho kuwa hao akina Mdee walifukuzwa unataka uthibitisho kuwa natural justice ilizingatiwa. Hivi una mshipa wa aibu kweli?

Kama natural justice haukuzingatiwa mbona walikata rufaa? Kama kulikuwa hakuna kikao halali mbona walikata rufaa?

Mwaka 2017 mwezi julai ulipokea barua toka kwa Lipumba juu ya wabunge wa CuF waliofukuzwa. Na wewe bila mashariti yoyote unayotoa sasa hivi uliridhia kuwafukuza. Iweje kwa hawa akina mama 19 ndio uwe na masharti?

Tumia akili na utambue kuwa katiba ni sheria mama.
View attachment 1772141
Kuweni na huruma na wamama, wale ni mama zetu jamani!

Sasa mnataka warudi nyumbani wakaoshe vyombo na kupiga deki!
 
Kama Nape Nnauye atakomaa nao lazima watatolewa nduki bungeni.

Nyuma ya Nape kuna nguvu kubwa isiyoonekana ambayo imeapa kuvisambaratisha vikaragosi vyote vya naniliu!
Hiyo nguvu iliyopo nyuma ya Nape imeishia kwa Nape au imeenda mbali zaidi hadi kutoka nje ya bunge?
 
Mambo mengine ni aibu tupu, hivi unakuwaje mbunge usie na chama? Unafiki, usaliti na tamaa hii hakika haitakuja kuwa baraka kwao. Ndugai asipambane na Nape aeleze watanzania uhalali wa wabunge hao kuwepo bungeni, ajibu barua ya Chama na sio kuiita kipeperushi. You can full people but not all the time.
 
Kutokana na shinikizo la kutaka wabunge hawa waondolewe Bungeni, na pia ili kumpa Spika amani na zaidi ili kulinda hadhi ya Bunge isiendelee kuporomoka, wenye mamlaka watawataka wabunge hawa wajiuzu ila watahakikisha wanalindwa hata wakiwa nje ya Bunge.

CCM na Ndugai swala hili limewakalia vibaya na sioni uwezekano wao wao kuendelea kuwalinda hawa wabunge zaid ya kuwataka tu watangaze kujiuzulu ila watakubaliana wabunge hawa waseme nini kwa umma siku ya kutangsza kujiuzulu.

Hii aibu ni ngumu kuibeba tena huku nafasi inskusta hivyo ni swala la muda tu.

Baada ya Bunge hili kwisha,sitarajii kama watarudi katika mkutano ijayo wa Bunge

Tusubiri.
Una wazimu si bure
 
Mleta mada umesema sahihi, Ndugai akiachwa na Hawa Hawara zake aendelee kuvunja Katiba kuna siku atafanya kubwa zaidi na wote tutaathirika zaidi. Hapa naona sio suala la Vyama bali ni suala la kuilinda Katiba na Mpuuzi yoyote atayetetea hao wendawazimu wa Job nae atakua adui wa demokrasia yetu
 
Yeye anawaombea wenzake msamaha yeye hajiombei
Ila ashakubali kama alikosea. Atazingatia matakwa ya katiba hivi punde.
Nishampa maelekezo. Sawa jamani
 
Kutokana na shinikizo la kutaka wabunge hawa waondolewe Bungeni, na pia ili kumpa Spika amani na zaidi ili kulinda hadhi ya Bunge isiendelee kuporomoka, wenye mamlaka watawataka wabunge hawa wajiuzu ila watahakikisha wanalindwa hata wakiwa nje ya Bunge.

CCM na Ndugai swala hili limewakalia vibaya na sioni uwezekano wao wao kuendelea kuwalinda hawa wabunge zaid ya kuwataka tu watangaze kujiuzulu ila watakubaliana wabunge hawa waseme nini kwa umma siku ya kutangsza kujiuzulu.

Hii aibu ni ngumu kuibeba tena huku nafasi inskusta hivyo ni swala la muda tu.

Baada ya Bunge hili kwisha,sitarajii kama watarudi katika mkutano ijayo wa Bunge

Tusubiri.
Pale ni aiza afe beki ama afe kipa, ila mpira hauingii nyavuni.

Yaani waache 12plus warudi kijiweni maisha ya kuombaomba!
 
Back
Top Bottom