Tuendelee kuipigania Katiba Mpya ya Wananchi ili kuondokana na hii ya Katiba ya Ccm ya mwaka 1977! Simuungi mkono Spika Job Ndugai, lakini pia siungi mkono hicho kipengele cha kumuondolea Ubunge mtu aliyechaguliwa na wananchi mbalimbali kwa sababu ya kuvuliwa uanachama!
Ifikie wakati tuwe na Katiba ambayo haitamfunga Mbunge/Diwani, au Mgombea yoyote yule kuwa mtii kwa Chama na Mwenyekiti badala ya wale Wananchi waliomchagua.