Spika Ndugai: Huku Mtu akishakuwa Polisi anaona kuweka Watu ndani ni raha. Watu wanarundikwa tu mahabusu

Spika Ndugai: Huku Mtu akishakuwa Polisi anaona kuweka Watu ndani ni raha. Watu wanarundikwa tu mahabusu

Kwanini wasitunge sheria kuzuia hali hiyo, au mpaka Rais aseme.
Sheria zinatungwa na Bunge lakini matakwa ya sheria gani itungwe au ibadilishwe yanatoka Serikalini.

Bunge haliwezi kutunga sheria bila muswada wa sheria hiyo kuwasilishwa Bungeni na Serikali.
 
Kuna watu wanaamini kuwa ni rahisi kuwatenganisha CCM na UNAFIKI
 
Spika wa Bunge la Tanzania amesema Polisi wanakamata Watu hovyo wengine wenye heshima zao na wanajulikana wanakoishi lakini wanarundikwa tu Rumande bila ulazima wowote.

Ndugai amesema "inatakiwa tujifunze kwa Nchi za wengine ambapo Mtu huwa anaitwa kituoni na kufanyiwa mahojiano kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani kwasababu anafahamika na hawezi kukimbia. Huku ukishakuwa Askari tunaona kuweka Watu ndani ni raha".

Ameongeza "Hiki kitu binafsi kinaniuma sana. Mtu anawekwa ndani wiki nzima au mwezi halafu baadae anakuja anaachiwa wakati shughuli zake nyingi zimeshasimama. Sheria nazo hata ukitoka huwezi kudai chochote, Waafrika hatuthaminiani".

Halleluyaaah, usikute NTU kaingia na mafuta ya upakoo mjengoni, anyway wamisho atakuwa wa kwanza kama ilivyoandikwa.
 
Sawa spika kaongea point
Sasa wanaamuaje

Ova
 
Kwa nini hatungi sheria kurekebisha hilo??
 
Ndugai mwenyewe au umemlisha maneno?😂
Tuna viongozi wanaounda vidonge ganzi kama chanjo ya kuendana na awamu iliyoko ikulu. Usanii kweli kweli. Mtu anaongea leo utafikiri ubongo umebadilishwa?
 
Hata kupiga watu na fimbo hadi mgombea mwenzako anazimia nayo ni kosa. Ndugai mzandiki sana.
 
Back
Top Bottom