Spika Ndugai: Huku Mtu akishakuwa Polisi anaona kuweka Watu ndani ni raha. Watu wanarundikwa tu mahabusu

Spika Ndugai: Huku Mtu akishakuwa Polisi anaona kuweka Watu ndani ni raha. Watu wanarundikwa tu mahabusu

Hakuna kitu cha maana anachofanya huyu mwamba,,, amekuwa mropokaji tu..

Hili analosema limekuwa kama majungu tu,, ila na yeye ni wale wale
 
..kama yeye alivyokuwa anaona raha kudhalilisha na kuwaonea wabunge wa Chadema ktk bunge la 2015 -- 2020.
 
Tumchukie Ndugai kwa matendo na maneno yake lakini siyo kwa sababu tu ni Ndugai.

Kwa hili, nampongeza Ndugai. Asiishie tu kusema kuwa inamsikitisha bali aiamuru Wizara ya Sheria kuleta miswada itakayoondoa sheria zote za hovyo, zikiwemo zile alizozilazimisha marehemu Magufuli kwa lengo la kuwatesa na kuwakomoa Watanzania.

Ndugai anaweza asitoke hadharani na kukiri, lakini kwa kauli hizi anataka kusema kuwa aliyatenda na kuyasimamia yote mabaya wakati wa utawala wa Magufuli kwa sababu ya hofu ya maisha yake na na hofu ya kufungwa. Maana angepingana na Magufuli, lazima matumizi yake ya matibabu yangempeleka Segerea.
 
Wao wanatunga sheria za mitandao ya jamii na kuwaruhusu polisi kuchukua simu ya mtuhumiwa na kuipekua baadae wakaja na kipengele cha uhujumu uchumi hao hao bunge mwingine akaja na ishu ya kulike tuu ni kosa leo hii wanakana walichokua wanatunga na kuwalaumu polisi utadhani polisi wanasimamia Sheria ambazo hazijatungwa na wao huyo Ndugai asituone sisi makolo sana...
 
Spika wa Bunge la Tanzania amesema Polisi wanakamata Watu hovyo wengine wenye heshima zao na wanajulikana wanakoishi lakini wanarundikwa tu Rumande bila ulazima wowote.

Ndugai amesema "inatakiwa tujifunze kwa Nchi za wengine ambapo Mtu huwa anaitwa kituoni na kufanyiwa mahojiano kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani kwasababu anafahamika na hawezi kukimbia. Huku ukishakuwa Askari tunaona kuweka Watu ndani ni raha".

Ameongeza "Hiki kitu binafsi kinaniuma sana. Mtu anawekwa ndani wiki nzima au mwezi halafu baadae anakuja anaachiwa wakati shughuli zake nyingi zimeshasimama. Sheria nazo hata ukitoka huwezi kudai chochote, Waafrika hatuthaminiani".

Huyu kashakuwa Zumbukuku
 
Kuna kitu anaogopa huyu. Au kuna genge lake analilinda. Aliagiza akina Lema na akina Halima walikuwa wanakamatwa wakiwa Bungeni huku akijua sheria za bunge zinawapa kinga
 
Huyo zwazwa kuna kitu anataka kujitetea au analinda magenge yake.
 
Practise ni zero ikiwa maagizo ni kutoka juu. Huko juu ndio kunatakiwa kudhibitiwa.
Hii huweza kuwa ni sababu moja

Lakini sababu nyingn ni polisi wengi hawazijui sheria vizur japo kuwa wanafundishwa
So elimu kwa hao polisi inabidi iongezwe pia kwasababu sio kila wanapo kamata watu maagizo yanatoka juu
 
Walikua wanapongezana wewe wafukuze huko Bungeni wakiwa nje huku hawana kinga mimi ntawashughulikia leo hii anayakana matendo yake ....
 
Chuki imezidi kwa Job ,punguzeni jamani!
Nyinyi mko perfect?
Acheni hizo, be reasonable, acheni unazi.
Mnakera, yeye si angel, kuna wakati anafanya yasiyopendeza na pia kuna wakati anafanya yanayopendeza. Tuvumiliane!
 
Wao wanatunga sheria police wao wanasimamia hizo sheria zifuatwe*to enforce laws) kwani shida iko wap watu wanazuiliwa kutokana na nature ya makosa yao na kwa sababu za kiupelelezi kuna waheshiwa ukiwaita kwa simu au barua wanajidai kuzuga wapo bize mpaka uwafate so tuache vyombo vya dola vifanye kazi zao sababu vimewekwa kisheria.
 
Mnamnanga tu mzee wa watu kiuhalisia tatizo lipo magerezani na polisi na yeye ameonyeshwa kukerwa ni heri ameliongelea pengine asingetokea mtu wa kulipigania hilo.siku ukiingia mikononi mwa hao wapumbavu wa magereza na polisi ndio utatambua ndugai aliongea kitu cha maana
 
Spika wa Bunge la Tanzania amesema Polisi wanakamata Watu hovyo wengine wenye heshima zao na wanajulikana wanakoishi lakini wanarundikwa tu Rumande bila ulazima wowote.

Ndugai amesema "inatakiwa tujifunze kwa Nchi za wengine ambapo Mtu huwa anaitwa kituoni na kufanyiwa mahojiano kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani kwasababu anafahamika na hawezi kukimbia. Huku ukishakuwa Askari tunaona kuweka Watu ndani ni raha".

Ameongeza "Hiki kitu binafsi kinaniuma sana. Mtu anawekwa ndani wiki nzima au mwezi halafu baadae anakuja anaachiwa wakati shughuli zake nyingi zimeshasimama. Sheria nazo hata ukitoka huwezi kudai chochote, Waafrika hatuthaminiani".

Bunge ndilo linalotunga sheria na kuzipitisha na bunge ndilo pia linaloridhia mabadiliko ya sheria na kuyapitisha. One way of solving a problem is to name it.
 
Back
Top Bottom