Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unasemea huku sio kawaida ku resign shida ni kuwa huku kwetu ni njaa Sana.SPIKA NDUGAI AJIUZULU USPIKA
Mjukuu wa Mwalimu
Kujiuzulu uspika wa Bunge ndiyo ushauri wa haraka ambao ningeweza kumshauri Job Ndugai, kama ningekuwa mshauri wake wa masuala ya kisiasa.
Kwanini?
1. Spika kwenye Bunge la Tanzania anatokana na chama cha siasa. Vyama huchuja na kupitisha mtu mmoja ili akagombee uspika kisha hupigiwa kura na wabunge. Mwenyekiti wa chama chako akitamka hadharani kauli zinazoonesha wewe hutoshi au hufai kukalia kiti cha uspika, busara ni kuachia ngazi.
2. Spika ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, chombo chenye nguvu zaidi ya kufanya maamuzi ya mara kwa mara, kwa kukasimiwa madaraka na vyombo vingine vya chama. Huko katika vikao vya Kamati Kuu, Rais Samia ndiye mwenyekiti wa vikao na tayari ameonesha kuwa mjumbe mmojawapo (Spika) hana nia njema na serikali pamoja na utekelezaji wa ilani ya chama. Hivyo anayetuhumiwa busara ni kukaa pambeni.
3. Spika amesemwa hadharani na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama chake pia kuwa mawazo yake yapo kwenye jinsi atakavyonufaika na uchaguzi mkuu wa 2025. Lolote atakalofanya bungeni la kuibana serikali itaonekana ni harakati zake za uchaguzi wa 2025 na akiisifia au kuiunga mkono serikali itaonekana anafanya UNAFIKI TU. Hivyo, hakuna atakalofanya lisilete maneno. Busara ni kujiuzulu.
4. Kwa utamaduni wa CCM, NI LAZIMA Rais aliyeongoza muhula mmoja AACHIWE kugombea tena muhula wa pili. 2021 - 2025 ya Rais Samia inahesabika muhula wa kwanza. Mtu kama Spika anayetokana na CCM kutangazwa hadharani kuwa ana HOMA YA 2025, na pengine ana JAMBO LAKE tofauti na utamaduni na utaratibu wa chama, busara ni KUPISHA. Iwe ni kweli au lah busara ni kujiuzulu tu.
Utamaduni wa kujiuzulu haujazoeleka sana Afrika na Tanzania. Kwa wenzetu, watu hujiuzulu si kwasababu tu wamekosea bali hata kama mawazo yako yametofautiana sana na wenzako walio wengi au mkuu wako.
KWETU TANZANIA licha ya Spika kuwa mkuu wa muhimili wa Bunge kama alivyo Rais ambaye ni mkuu wa muhimili wa Serikali lakini kama Spika na Rais wanatoka chama kimoja hasa CCM, basi Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama tawala ndiye bosi wa Spika. Kutoa kauli zinazotafsiriwa kama ni za kumpinga au kumzodoa Rais na mwenyekiti wa chama chako hasa kama mawazo yako hujayatolea ndani ya vikao halali vya kikatiba na kisheria ni DOSARI KUBWA.
#BUNGEHURU
View attachment 2068729
Apishe kiti, anakidharirisha kiti