Spika Ndugai: Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) ipo ICU, imeshashindwa

Ipo wana eneo juzi kati nilisikia, hapo Mvomero mpaka Kilosa, wananuia kupangisha vitalu vya ufugaji, serikali, ikusanye mapato. Shida inakuja ndani humo huko kuna wakulima waliouziwa maeneo na watendaji sijui wenyeviti.

Vurugu tupu. Kweli serikali haiwezi kuchunga ng'ombe. Ilaaa mmmh

Everyday is Saturday............................... 😎
 
I
Ukweli ni upi? kwamba CCM inajipinga yenyewe wakati wana msemo wao wa MITANO TENA?

Ndugai yupo SUKUMA GANG na hata siku moja hayupo na mama , inajulikana, ni suala la muda atatoka tu kwa kiti kile, wala haisubiriwi 2025.
Inshallllah
 
Spika wa Bunge la Tanzania amesema Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) ipo 'ICU' na kwa miaka mingi wadau wamekuwa wakinyamaza, lakini imefika mahali lazima ukweli usemwe.

Amesema "NARCO hawezi kufufuka, ile sio Ranchi. Mkitaka tuibadilishe iwe Hifadhi ya Wanyamapori. Hata Serikali iende inunue na kujaza ng'ombe hamtafanikiwa".

Ameongea hayo Bungeni wakati wa Majadiliano ya Bajeti ya Wizara ya Migugo na Uvuvi ambapo amesisitiza, "Sio kazi ya Serikali kuchunga ng'ombe. Achieni wenye kazi yao".
Wameuza Ranchi za taifa Hawa ccm hasa kipindi Cha Kikwete, moja Ranchi ya Kongwa nayo ilikua mbioni kuuzwa ,kupitia mgongo wa kubinafsiwa ,lazima lanchi kurudi Sasa na mkiuza ya Kongwa mtapata majibu kila mmoja KWA nafasi yake ,tz viongozi wengi ni majizi sana
 
Spika wa Bunge la Tanzania amesema Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) ipo 'ICU' na kwa miaka mingi wadau wamekuwa wakinyamaza, lakini imefika mahali lazima ukweli usemwe.

Amesema "NARCO hawezi kufufuka, ile sio Ranchi. Mkitaka tuibadilishe iwe Hifadhi ya Wanyamapori. Hata Serikali iende inunue na kujaza ng'ombe hamtafanikiwa".

Ameongea hayo Bungeni wakati wa Majadiliano ya Bajeti ya Wizara ya Migugo na Uvuvi ambapo amesisitiza, "Sio kazi ya Serikali kuchunga ng'ombe. Achieni wenye kazi yao".
IMG-20210527-WA0140.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa sijui ndugai ana mawazo ya hovyo namna hii, yaani anadiriki kukashfu miradi ya serikali kwa maslahi yake binafsi. Kwa hiyo maeneo ya serikali yagawiwe tu kwa maneno ya rejareja ya ndugai ambaye wadau hapo juu wanasema anamiliki maelfu ya ng'ombe na ameshamegewa eneo la ranch, na kwenye kutoa hizo kejeli hakuweza ku-declare mgongano wa kimaslahi. Basi tuseme serikali imeshindwa kazi apewe ndugai aendeshe serikali...
 
Hatari Cha ajabu utakuta bado ina mkurugenzi,ana V8,linawekwa mafuta,na anaenda ofisini kusoma magazeti

Mwenyekiti wa bodi wa ranchi za Taifa ni Mzee Paul Kimiti!!!! Lowassa alipokuwa waziri wa mifugo alijichukulia yake mapema!!!

Ndugai ni Mbunge anaeiwakilisha constituency ya Kongwa ambako kulikuwa na ranch kubwa sana ya serikali; sasa kama hizi ranch zimekufa ikiwemo na hii ya Kongwa ,na yeye muda wote huu akiwa mbunge alikuwa wapi kushtukia ufisadi uliosababisha hizi ranch kufa na leo kuja na hoja eti zibinafsishwe? Huyu mgogo achunguzwe lazima amehusika kuhujumu ranch ili ajikatie na yeye!!
 
Ipo wana eneo juzi kati nilisikia, hapo Mvomero mpaka Kilosa, wananuia kupangisha vitalu vya ufugaji, serikali, ikusanye mapato. Shida inakuja ndani humo huko kuna wakulima waliouziwa maeneo na watendaji sijui wenyeviti.

Vurugu tupu. Kweli serikali haiwezi kuchunga ng'ombe. Ilaaa mmmh

Everyday is Saturday............................... 😎
Shirika lilikuwa na uwezo wa kufuga ng'ombe Ila Ni wizi wa viongozi unasababisha Ranchi haziendelei.
Watu wanaiba ng'ombe, wanaiba ndama, hata vifaa. Mtanzania kuiendeleza Mali ya imma Ni mtihani.
 
Huyu spika kwani hana namna nyingine ya kuwasilisha maoni yake au mapendekezo yake?
Haya mambo ya kukaa kwenye kiti cha spika na kuanza kupingana na serikali ile ile bila data kwa kile anacho kiita maoni hayana afya kwenye nchi hii.
 
Spika wa Bunge la Tanzania amesema Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) ipo 'ICU' na kwa miaka mingi wadau wamekuwa wakinyamaza, lakini imefika mahali lazima ukweli usemwe.

Amesema "NARCO hawezi kufufuka, ile sio Ranchi. Mkitaka tuibadilishe iwe Hifadhi ya Wanyamapori. Hata Serikali iende inunue na kujaza ng'ombe hamtafanikiwa".

Ameongea hayo Bungeni wakati wa Majadiliano ya Bajeti ya Wizara ya Migugo na Uvuvi ambapo amesisitiza, "Sio kazi ya Serikali kuchunga ng'ombe. Achieni wenye kazi yao".
Mbona kama anaitaka yeye anapigia chapuo ibinafsishwe aichukue?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Huyu spika kwani hana namna nyingine ya kuwasilisha maoni yake au mapendekezo yake?
Haya mambo ya kukaa kwenye kiti cha spika na kuanza kupingana na serikali ile ile bila data kwa kile anacho kiita maoni hayana afya kwenye nchi hii.
Wabunge wenu hao kina babu tale na Musukuma wanalala bungeni ndiyo maana spika anawasemea.
 
Back
Top Bottom