Spika Ndugai: Kwa sasa mitandao ya kijamii ina nguvu sana

Kwa mara ya kwanza kauli ya kiongozi mkuu wa Serikali kukili nguvu ya mitandao ya kijamii imetolewa na Spika Ndugai ambaye ni mkuu wa Mhimili wa Bunge Tanzania.

Mitandao siku hizi ina nguvu, inaweza ikatengeneza ajenda, ikapeleka ajenda ambako wala haikuwa, na mjadala ukawa ni wa moto sana." - Spika Job Ndugai.

My take:
Kwa kauli ile ni wazi Viongozi wameanza kuhofia mitandao ya kijamii.
Na bado !
 
Kama unafikiri ni kweli Ndugai alikua hajui mitandao inanguvu kiasigani basi wewe utakua unashida ya kufikiria sawasawa. Ki msingi alikua anatafuta namna ya yeye kuonekana ameomba radhi( amejishusha) kwakua mhimili ( Serikali) ni mkubwa Sana kikatiba na ki Chama na unaweza kumshughulikia yoyote imtakae kwa wakati unao ona inafaa.
 
ndugai wala hajaomba msamaha, kacheza bonge la mind game ili waendelee na mipango yao.
 
Kwa mara ya kwanza kauli ya kiongozi mkuu wa Serikali kukili nguvu ya mitandao ya kijamii imetolewa na Spika Ndugai ambaye ni mkuu wa Mhimili wa Bunge Tanzania.

Mitandao siku hizi ina nguvu, inaweza ikatengeneza ajenda, ikapeleka ajenda ambako wala haikuwa, na mjadala ukawa ni wa moto sana." - Spika Job Ndugai.

My take:
Kwa kauli ile ni wazi Viongozi wameanza kuhofia mitandao ya kijamii.
Hawa siyo viongozi ni majangili tupu
 
Kabisa, kazi iliyopaswa kufanywa na bunge, sasa inafanywa na mitandao. Huku mitandaoni ndio kuna mijadala halisi, kwenye media rasmi na bungeni kumebaki sehemu kusifia na kuabudu kila kitu cha serikali
Huku watu wapo huru hawahofii vyeo
 
Wamechelewa mno kujua nguvu ya social media, sema sisi ni bado bado kujua silaha tulio beba au itakayo tubeba.
 
na ina nguvu kweli, mitandao ndio muhimili wa nne wa serikali hasa pale Bunge linapoonekana ni dhaifu
 
Simshangai Mh Ndugai bali nitamshangaa aliyeombwa huu msamaha kama ataamini huo msamaha na kilichosemwa kuwa kinatoka katika dhati ya moyo ya muomba msamaha na msifia mkopo. Gavana wa BOT aliye tolea ufafanuzi kuhusu nchi kupigwa mnada alisikiliza clip iliyo katwa ikaleta maana tofauti? Only in Tanzania.

Nafikiri wako wanasiasa wanawaona Watanzania ni matahira.
Hili ndio jibu ila amini usiamini tayari watu milioni 35 ama zaidi sasa hivi wameshaelekea upande wa upepo huu wa leo,
 
Kwa mara ya kwanza kauli ya kiongozi mkuu wa Serikali kukili nguvu ya mitandao ya kijamii imetolewa na Spika Ndugai ambaye ni mkuu wa Mhimili wa Bunge Tanzania.

Mitandao siku hizi ina nguvu, inaweza ikatengeneza ajenda, ikapeleka ajenda ambako wala haikuwa, na mjadala ukawa ni wa moto sana." - Spika Job Ndugai.

My take:
Kwa kauli ile ni wazi Viongozi wameanza kuhofia mitandao ya kijamii.
Kwa hiyo ndio amegundua leo
 
Wasingelikuwa wanajua nguvu yake wasingelitunga na kupitisha sheria za matumizi ya mitandao...

Hapo anajikosha tu, mkubwa kaamua kuchutama...
Na hasa mijadala ikiwa na watu wasio na critical thinking...Tuwekeze kwenye elimu, maisha ya mbele hayana mjomba wala shangazi dunia itakuwa wazi na wenye akili, hekima na busara tu ndiyo watakao survive...Maana uovu umetamalaki mno mno na walioanzisha mitandao hiyo wao wana agenda yao permanent, sisi ma limbukeni ndiyo wenye shida kubwa
 
Kwa mara ya kwanza kauli ya kiongozi mkuu wa Serikali kukili nguvu ya mitandao ya kijamii imetolewa na Spika Ndugai ambaye ni mkuu wa Mhimili wa Bunge Tanzania.

Mitandao siku hizi ina nguvu, inaweza ikatengeneza ajenda, ikapeleka ajenda ambako wala haikuwa, na mjadala ukawa ni wa moto sana." - Spika Job Ndugai.

My take:
Kwa kauli ile ni wazi Viongozi wameanza kuhofia mitandao ya kijamii.
Huyu anataka mitandao ifungwe, anachuki binafsi kwa mitandao.
 
Muswaada wa kuifungia sii uliletwa mezani kwake...
 
Hii ndio kauli ya mwisho ya aliyekuwa Spika wa bunge la JMT mh Job Ndugai, " Mitandao ya Kijamii ina nguvu sana "

Mungu wa mbinguni awabariki nyote!
 
Back
Top Bottom