Spika Ndugai: Mbowe alikuwa Ulaya sasa katumwa na watu wake anapotosha kuhusu ripoti ya CAG

Spika Ndugai: Mbowe alikuwa Ulaya sasa katumwa na watu wake anapotosha kuhusu ripoti ya CAG

Audit (au evaluation yoyote for that matter) inapofanyika, uongozi husika hupewa nafasi ya kujibu those key findings na majibu yao huwa ni sehemu ya final report.

Unachokisoma kwenye report ya CAG kimeinclude explanations kutoka kwenye institutions husika. Kwa lugha rahisi ambayo hata layman ataelewa - hiyo ni final report. Rais huwa hawepi half-baked report yenye opinions eti ije kujibiwa baadae.
Hujui nini maana ya audit queries.
 
Spika hujatuhumiwa na CAG, waliotuhumiwa wapo na wanatakaiwa kujitetea wao sio wewe! wewe bila shaka unatakiwa kufanya kazi ya kuisimamia serikali kupitia kamati zako ulizotaja sio kujibebesha jukumu la kuelimisha wananchi
 
Kwanini wasisubiri hizo final conclussios ili wailete hiyo ripoti? Sasa huyo manager wa TTB kusimamishwa kazi kwanini wakati ni querries tu?
Queries zinatoa majibu ya kweli amesimamishawa ili kupisha uchunguzi. Utaratibu wa audit upo hivyo lazima mkaguzi auibue hoja kisha majibu.
 
Spika wa Bunge Job Ndugai, amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya CAG na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne, kwa kuwa inapotoshwa huku akimtaja Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuwa mmoja wapo

Spika wa Bunge Job Ndugai amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya Mdhibiti na Mkuguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne badala ya mkutano wa tano, kwa kuwa inapotoshwa.

Akizungumza leo Jumatatu Aprili 12 2021, Ndugai huku akimtaja Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amedai kuwepo upotoshaji wa ripoti hiyo.

Kauli ya Spika imekuja siku moja baada ya Mbowe kuhutubia kupitia mitandao ya jamii, ambapo pamoja na mambo mengine alilituhumu Bunge kwa vitendo vya rushwa.

“Watu wanabeba tu mabilioni yameibiwa sasa huyo rafiki yangu Freeman Mbowe alikuwa Ulaya huko sasa katumwa na watu wake huko anapotosha mambo,” amesema.

Amesema sio watu wengi wenye uelewa wa kuchambua taarifa za kihasibu na hivyo kunaweza kukawa na ujenzi wa kituo cha afya wa Sh 500milioni lakini Sh 499milioni zimetumika vizuri kabisa.

Hata hivyo, amesema lakini kati ya fedha hizo Sh1milioni ikikosa kiambatanisho fulani ni kawaida wakaguzi wanahoji fungu zima la Sh 500milioni.

Amesema kwa hiyo unaposoma mtaani unaona sh 500 zimeibwa lakini kumbe pale ni Sh milioni moja ndio hazina risiti.

Amesema kamati hizo zitaanza mapema kuchambua ripoti hizo ili waangalie ratiba yao na kuwaelimisha watu kuhusiana na ripoti ya CAG ambayo ni taarifa nzuri lakini baadhi ya watu wanabeba na kupotosha tu.

Mwananchi
acquired stupidity
 
Hivi katiba haisemi chochote kuhusu bunge kutokuwa na imani na Spika[emoji23][emoji23][emoji23]
 
job na mwiglu ni wanasiasa wa hovyo kabisa kuwahi tokea. hivyo wanahalalisha kila milioni moja kuibiwa kwenye ratio ya mradi au source ya m500? ni sawa na msemo wa dharau sana kwa hao wanaowaita wanyonge wao.
#kahela kenyewe kaliwa kahela kamboga tu.. #mama tibaijuka
 
Back
Top Bottom