Hata kupimwa hakusaidii. Tena kunaleta confidence mbaya na ya hatari ambayo inaweza kusababisha maambukizi zaidi. Imagine mtu akipima leo akikutwa hana kumbe wale virus aliambukizwa siku moja au mbili zilizopita? Nikupe mfano mmoja. Ndege ya mwisho ya Kenya Airways kutoka USA kabla hawajasitisha safari za USA ilirushwa na rubani mmoja anaitwa Daudi Kibati. Ilipofika Nairobi siku ya safari ya mwisho, ilibidi akae karantini kwa sababu alikuwa ametoak USA iliyokuwa na maambukizi mengi. Baada ya siku tatu wakam-test virus akawa hana lakini ikabidi akae karantini mpaka siku 14 ziishe. Siku ya tano wakam-test ikawa negative tena. Kufika siku ya tisa akaanza kuumwa na alipofanyiwa test ikawa positive na kufariki siku tatu baadae. Njia nzuri ya Bunge kufanya ni kukatiza vikao mara moja mpaka hali itakapokuwa nzuri.