Spika Ndugai: Nimechaguliwa na watu 400,000 kuwa mbunge kwa miaka 25, mara mbili nimepita bila kupingwa, unaniita ZUZU?

Spika Ndugai: Nimechaguliwa na watu 400,000 kuwa mbunge kwa miaka 25, mara mbili nimepita bila kupingwa, unaniita ZUZU?

Sindhani ata hao laki 4 wanafika.

Uchagizi wa siku hizi ni wizi wa wazi wazi.Inawezekana ni kura feki.
 
Screenshot_20211024-075919~2.png
 
Sindhani ata hao laki 4 wanafika.

Uchagizi wa siku hizi ni wizi wa wazi wazi.Inawezekana ni kura feki.
Umenifungua macho, sensa ya mwaka 2012 inaonesha wilaya ya Kongwa ilikuwa na jumla ya watu 309,973. Nafikiria si rahisi kupata kura hizo laki 4 kwa Kongwa hata kama watu wameongezeka.
 
Mwingine alivyoona zuzu linapingwa na spika akajiita BWEGE
 
Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema anakerwa na tabia ya baadhi ya watu kuwaita wabunge mazuzu na kuwataka wajenge utamaduni wa kuheshimiana.

Akifungua wiki ya Azaki jijini Dodoma leo Jumamosi Oktoba 23, Ndugai amesema, “Sio unaitwa Azaki basi unawasema wenzako maneno unayotaka ya hovyo. Tumewahi kugombana na baadhi ya wazee, mzee unatuita jina sisi hatulipendi…Hivi tumekosea wapi kama unamuita mtu jina la Juma anasema mimi jina hilo silitaki.

“Tatizo lako nini? Unang’anga’ania kuita hilo jina, we ni nani? Haiwezekani kama mwanadamu akikwambia hiki sina raha nacho kiache na wewe hukiachi, kama kweli wewe ni muungwana mtu wa Mungu utakiacha.”

Amesema matokeo ya kutoheshimiana ni wazee (ambao hakuwataja) wanawasema wabunge ni mazuzu wakati wana akili.

Amesema wao hawana muda wa kubishana bishana na watu wana namna hiyo.

Amesema yeye amechaguliwa na watu 400,000 kuwa mbunge kwa miaka 25 katika chaguzi mbalimbali na tena mara mbili amepita bila kupingwa.

“Hata kesho nikienda kusimama (kugombea) tafuta wa kusimama na mimi hutampata. Akisimama ni mpambe wa kusindikiza. Halafu wewe unaniita zuzu yaani wale watu una maanisha ni mazuzu wamechagua zuzu mwenzao?”amehoji.

Ndugai alipongeza Azaki kwa kazi nzuri wanazofanya lakini akasema wachache wao wamekuwa wakitumika na wana ajenda zisizokuwa za kwao na kwamba Azaki chache zimekuwa na ajenda za kupata fedha kutoka mahali fulani (hakukutaja).

“Sasa kama we njaa yako ni hela ndio maana lazima zitungwe sheria sasa zinazokufuata kwenye hela. Eeeeh utatuambia nani amekupa, kiasi gani, ziko wapi, utazitumiaje na utaleta taarifa kwa kila shilingi zamani haikuwa hivyo tuliaminiana lakini baada ya kuona mwenendo usio ridhisha ndio tukatunga sheria,”amesema.

Ndugai amesema kama wasipoweka sera ya kuambiana na kurekebishana (wao kwa wao mashirika) basi hata sheria zitakazotungwa siku za usoni zitakuwa kali zaidi.
Hata pale alipompiga na rungu mgombea mwenzake aliyekuwa anaongoza kwenye hatua ya kura za maoni bado anadai alishinda kihalali ?, ndugai na zuzu na waliomchagua (ambao ni wachache sana) nao ni mazuzu pia.
 
Umenifungua macho, sensa ya mwaka 2012 inaonesha wilaya ya Kongwa ilikuwa na jumla ya watu 309,973. Nafikiria si rahisi kupata kura hizo laki 4 kwa Kongwa hata kama watu wameongezeka.
Mkuu asante, unajua mafisiem huwa yanaamini watanzania wote mabozongo,
 
Kama wanapi5isha Sheria za ajabu ,ambao baadaye wanazinduka kuwa hii Sheria ,tuliipitashaje😂😂
Sio ndio uzuzu wenyewe au !
 
Alipita bila kupingwa,wanakongwa wanakutaka wewe au hukusikia siku mwendazake aliposimama kuwasalimia walipomwambia hawakutaki!
 
Azalaki Seyawaaa..,,,Seyawaaa!!!
Nabali mboni nangee,,,😂😂😂
 
Umeitwa kwenye ufunguzi wa Azaki badala ya kuzungumzia mambo yanayohusiana na hilo wewe unaleta hayo si ndiyo uzuzu huo sasa anauthibitisha
Yaan katika wabunge 359+ hakuna mtu anaezungumza lugha ya wananchi ila wanazungumza lugha yao ambayo wananchi wanna[emoji15][emoji15] jarb kujiuliza hakuna mtu anaongelea Leo namn ambavyo wamachinga wanapata wanakuwa wakimbizi kwenye nchi yao,

Viongoz woooteee wamepigwa ganzi, hakuna ambae hata kusema tu hkuna, halafu watu waache kuwaita majina yanayowafaa[emoji15][emoji15][emoji125][emoji125][emoji125]??

Na signout[emoji56][emoji56]
 
Amesema matokeo ya kutoheshimiana ni wazee (ambao hakuwataja) wanawasema wabunge ni mazuzu wakati wana akili.
Wao wanajiona wana akili lakini uhalisia ndiyo unao define kuwa ni mazuzu
 
Angekuwepo zuzu mkuu yule mzee angekuwa ameshaokotwa mahali fulani asingevumilia kabisa kusikia mazuzu wakisakamwa.
 
Back
Top Bottom