Spika Ndugai: Vyuo vikuu vianze kufundisha Ujasiriamali kama vile vya Kenya vijana wasisubiri ajira ambazo hazipo!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Spika Ndugai amesema ni wakati sasa vijana wetu wakaachana na mawazo ya kuajiriwa na badala yake wajikite kwenye shughuli za ujasiamali na kilimo.

Ndugai amesema vijana waliomaliza darasa la saba ni mfano mzuri wa kuigwa kwa sababu wao hawachagui kazi tofauti na wale wanaojiita wasomi ambao wanazeeka wakiwa bado wanatafuta ajira ambazo hazipo.

Amevitaka vyuo vikuu viwaige wenzao wa Kenya.

Source TBC 2

Maendeleo hayana vyama!
 
Naunga mkono hoja kwa 100% mbali na ajira baadhi ya maofisi kuna mizigo sana! Yaani mtu anaajiriwa hawezi kujishughulisha kabisa,kuandika hawezi! Kupanga file taabu yaani ni kulalama tuu na kupiga story + kunyoosha miguu...

Na baadhi ninahisi unakuta ni wale watoto wa mama from primary up to university hawajui hata kuku wanakunywa vipi maji.
 
Mbona ujasiriamali unafundishwa sana vyuoni, labda Mh. Spika hana taarifa sahihi na alipaswa kuuliza kwa wakuu wa vyuo kabla ya kutoa tamko hili.

"Entrepreneurial Spirit" nayo ni kipaji kama soccer. Sio kila mtu anaweza kuwa mfanyabiashara.

Ndio maana kuna wafanyabiashara wazuri ukiwapeleka katika soccer nao wanashindwa.

Tatizo mtaani hakuna pesa, hata ukilima mauzo yatakuwa ni madogo sana.
 
Somo la ujasiriamali mbona lipo, lakini mbona yeye alikuwa ana Force ubunge Hadi alitaka kumuua mwenzake na rungu kichwani. Yeye ka mfano ajiuzulu ubunge na u speaker aanze ujasiriamali Ili kufundisha vijana kwa mfano
 
Dear, mtu akiwa na uhakika wa kula na kulala kamwe hawezi kumkumbuka mwenye njaa na kama wapo wanaokumbuka wenye njaa basi ni wachache sana.

Kosa sio la Ndugai bali hiyo ni nature ya binadamu wote wakiwa wameshiba pesa.
 
Hii ngoma ni nzito mkuu na ni global issue..sio Tanzania pekee
Ukitaka kuamini nenda
Haiti
Algeria
Senegal
Burkina Faso
Syria
Albania bila kusahau
Afghanistan
Kila mahali tabu tupu! tusione kwamba hii ngoma ni kwa bongo pekee!
Upo sahihi sana tu mkuu. It is a global issue
 
Spika Ndugai amesema ni wakati sasa vijana wetu wakaachana na mawazo ya kuajiriwa na badala yake wajikite kwenye shughuli za ujasiamali na kilimo.

Ndugai amesema vijana waliomaliza darasa la saba ni mfano mzuri wa kuigwa kwa sababu wao hawachagui kazi tofauti na wale wanaojiita wasomi ambao wanazeeka wakiwa bado wanatafuta ajira ambazo hazipo.

Amevitaka vyuo vikuu viwaige wenzao wa Kenya.
Umesahau signature yako bwashee..
"Maendeleo hayana vyama"!!
 
Ndugai amesema vijana waliomaliza darasa la saba ni mfano mzuri wa kuigwa kwa sababu wao hawachagui kazi tofauti na wale wanaojiita wasomi ambao wanazeeka wakiwa bado wanatafuta ajira ambazo hazipo.
Kama mtu anaweza akaishia darasa la saba kisha akafanya kazi na kuingiza vipato, kwanini bado wanajenga shule za secondary?
 
Dear, mtu akiwa na uhakika wa kula na kulala kamwe hawezi kumkumbuka mwenye njaa na kama wapo wanaokumbuka wenye njaa basi ni wachache sana.

Kosa sio la Ndugai bali hiyo ni nature ya binadamu wote wakiwa wameshiba pesa.
Duh hawa viongozi wetu wamezidi ubinafsi mbona kwa wenzetu wamejitahidi kuweka mazingira yanayoweza kumsaidia mtu wa chini kabisa, sasa huyo ndugai ukute watoto wake wamemaliza nje vile ni speaker kaandika kimemo wamepata kazi then ana joke watu wanaojishughulisha kitaa wasio na connection
 
Spika Ndugai amesema ni wakati sasa vijana wetu wakaachana na mawazo ya kuajiriwa na badala yake wajikite kwenye shughuli za ujasiamali na kilimo.

Ndugai amesema vijana waliomaliza darasa la saba ni mfano mzuri wa kuigwa kwa sababu wao hawachagui kazi tofauti na wale wanaojiita wasomi ambao wanazeeka wakiwa bado wanatafuta ajira ambazo hazipo.

Amevitaka vyuo vikuu viwaige wenzao wa Kenya.
Watoto wake wanasoma china.
 
Naunga mkono hoja kwa 100% mbali na ajira baadhi ya maofisi kuna mizigo sana! Yaani mtu anaajiriwa hawezi kujishughulisha kabisa,kuandika hawezi! Kupanga file taabu yaani ni kulalama tuu na kupiga story + kunyoosha miguu...

Na baadhi ninahisi unakuta ni wale watoto wa mama from primary up to university hawajui hata kuku wanakunywa vipi maji.
Wavivu nao pia ni janga la taifa
 
Duh hawa viongozi wetu wamezidi ubinafsi mbona kwa wenzetu wamejitahidi kuweka mazingira yanayoweza kumsaidia mtu wa chini kabisa, sasa huyo ndugai ukute watoto wake wamemaliza nje vile ni speaker kaandika kimemo wamepata kazi then ana joke watu wanaojishughulisha kitaa wasio na connection
Mh. Spika alipaswa kufanya utafiti kidogo kabla ya kutoa kauli kama hii.
 
Back
Top Bottom