Spika Ndugai amesema ni wakati sasa vijana wetu wakaachana na mawazo ya kuajiriwa na badala yake wajikite kwenye shughuli za ujasiamali na kilimo.
Ndugai amesema vijana waliomaliza darasa la saba ni mfano mzuri wa kuigwa kwa sababu wao hawachagui kazi tofauti na wale wanaojiita wasomi ambao wanazeeka wakiwa bado wanatafuta ajira ambazo hazipo.
Amevitaka vyuo vikuu viwaige wenzao wa Kenya.
Source TBC 2
Maendeleo hayana vyama!
TBC1 iko wapi hapa? Unge upload video au audio na kuitupia pamoja na maelezo yako. Sasa wewe unatuambia source ni TBC1 wakati wengine huo kwetu ni msamiati tusiotaka kujua hata maana yake...
Huyu hapa Spika Ndugai. Lakini kwa upande mwingine hawa viongozi wetu ni wabinafsi sana. Na tunaweza kusema ni maboya sana na pengine hawaelewi dhamana waliyo nayo kwa wananchi na nchi hii nzuri ya Tanzania...
Sasa Spika Ndugai anapolamika wakati yeye ndiye kiongozi wa chombo cha wananchi chenye mamlaka kuu ktk nchi hii kinachoweza kuielekeza serikali nini cha kufanya kutatua jambo fulani, anakuwa haeleweki kidogo...
Tatizo hili ni kubwa mno na hii ni ishara moja tu ndogo ya kushindwa kwa SERA na MIPANGO ya chama kilichotawala nchi tangu Uhuru mwaka 1961...
Bahati mbaya zaidi ni kuwa awamu hii ya tano imepata viongozi ambao mtu anaweza kusema ni AFADHALI YA JANA....
Hawana kitu vichwani mwao kuanzia kwa Farao hadi kwa Vifarao vya chini huku. Na kama wana chochote kwenye vichwa vyao, basi ni kwa kiwango kidogo sana...
Wanatumia nguvu nyingi zaidi kuongoza kuliko BUSARA, HEKIMA, MAARIFA na UFAHAMU....
Busara (WISDOM), maarifa (KNOWLEDGE) na ufahamu/uelewa (UNDERSTANDING) ndivyo ambavyo Mfalme Sulemani aliomba kwa Mungu alipotawazwa kuwa Mfalme wa Israel enzi hizo...
Nini kilitokea baada ya kuomba hayo na kupewa na Mungu, Bwana?
Mengine yote yalifuata; ustawi Wa jamii yake yote, Amani na utulivu, Uchumi imara, upendo na furaha ya maisha katika taifa lote alilokuwa analiongoza...
Viongozi/wafalme wa mataifa ya leo, wametanguliza kujipenda wenyewe (ubinafsi), kupenda kukwezwa na kunyenyekewa, kupenda pesa na ufahari kwa kuwanyonya wananchi wanaowaongoza na wakijua kabisa kuwa wanaogolea kwenye taabu na umasikini wa kutupwa na hawana mipango ya kuwatoa huko...
OLE WAO HAWA KINA NDUGAI NA WENZAKE...