Spika Tulia Ackson ashauri itafutwe njia ya kuzuia mauaji yatokanayo na wivu wa mapenzi

Spika Tulia Ackson ashauri itafutwe njia ya kuzuia mauaji yatokanayo na wivu wa mapenzi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mh Tulia Ackson ametoa ushauri huo ndani ya bunge analoliongoza , kwa hoja kwamba Taarifa za vifo zinazotangazwa kila kukicha na Jeshi la Polisi hazisaidii kupunguza mauaji , na badala yake zinasababisha mauaji kuongezeka zaidi.

Bado haijafahamika hasa lengo la hoja yake hiyo.

Bali ikumbukwe kwamba wakati wa awamu ya 5 ambako vifo na maiti nyingi ziliripotiwa huko baharini na kwenye viroba , Dr Tulia alikuwa Naibu Spika na hakuwahi kushauri taarifa zile zifichwe.

========

Spika Tulia Ackson amesema kuwa ongezeko la mauaji huenda linatokana na kuripotiwa sana kwa taarifa za mauaji kutoka kwa polisi kwenda kwa vyombo vya habari hivyo taarifa hizo kuwa kama ni nzito na watu kuona huenda ni jambo la kawaida na kwa kuwa limetokea kuko na kule nao kuona hata wao wanaweza kufanya yaani ni kitu chepesi tu kujitoa uhai.

Ameshauri Wizara ya mambo ya Ndani watafute njia za kukabiliana na tatizo la mauaji yatokanayo na wivu wa mapenzi hasa kwa kuanza kushirikisha watu wa chini kabisa wawaulize kwa nini wivu wa mapenzi huenda wakapata njia za kumaliza tatizo hilo.

 
Anatafuta namna ya kutetea kiti chake, kumbuka JN aliambiwa awafurushe ili waje huku wamaliziwe, na yeye bila hiyana akawa anafanya kweli. Subiri tutasikia mengi, labda tuwe viziwi.
 
Sheria zipo Mahakama zipo anataka njia gani zitafutwe?
 
Mh Tulia Ackson ametoa ushauri huo ndani ya bunge analoliongoza , kwa hoja kwamba Taarifa za vifo zinazotangazwa kila kukicha na Jeshi la Polisi hazisaidii kupunguza mauaji , na badala yake zinasababisha mauaji kuongezeka zaidi...
Mlificha ukweli kuhusu Covid19 sote tunajua Nini kilitokea baada ya kujitoa ufahamu kuhusu Covid19..
 
Mh Tulia Ackson ametoa ushauri huo ndani ya bunge analoliongoza , kwa hoja kwamba Taarifa za vifo zinazotangazwa kila kukicha na Jeshi la Polisi hazisaidii kupunguza mauaji , na badala yake zinasababisha mauaji kuongezeka zaidi...
Njia mojawapo ni kuhamasisha afya ya akili, hapo ndio mzizi wa tatizo. Watekelezaji wengi wa mauaji hayo wanaonekana wazima ila uchunguzi ukifanyika kiundani kutakua na asilimia kubwa watakutwa na matatizo ya akili
 
Lengo kuu la kuoana ni watoto+ company. Tatizo watu wanaoana kwa lengo la kupata mbusy.. Tukiwa na falsafa ya maisha ya ndoa hakuta kuwa na mauaji yanayotokana na wivu wa mapenzi
 
Je yuko tayari KUTOA huduma Kwa wahitaji hao!

Manake kikubwa hapo ni walengwa wananyimana au kukosa Kupeana haki zao. Sasa hiyo Sheria itamhukumu yupo?

Badala ya kuzungumzia Tozo ambazo zinaumiza, vikiba navyo chanzo kikubwa wakina mama! Siku ikiingia mkononi hakukaliki Kwa nyumba
 
Ww jamaa hata ikija topic ya upungufu wa mvua mchango wako ni katiba mpya ije hahaha hivi hii katiba mpya yako unaona inaweza kuleta mpaka ela nyumbani kwako au
Kwani wewe katiba mpya ikija inakuuma nini?.maana naona unachukia kitu kizuri kwa manufaa na maslahi makubwa ya nchi.ni watu wabinafsi peke yake ndio ambao hawajui manufaa ya katiba bora.
 
Back
Top Bottom