Kwani wewe katiba mpya ikija inakuuma nini?.maana naona unachukia kitu kizuri kwa manufaa na maslahi makubwa ya nchi.ni watu wabinafsi peke yake ndio ambao hawajui manufaa ya katiba bora.
Kuoa zaidi ya Mke mmoja ndio dawa peke yake.Mh Tulia Ackson ametoa ushauri huo ndani ya bunge analoliongoza , kwa hoja kwamba Taarifa za vifo zinazotangazwa kila kukicha na Jeshi la Polisi hazisaidii kupunguza mauaji , na badala yake zinasababisha mauaji kuongezeka zaidi.
Bado haijafahamika hasa lengo la hoja yake hiyo.
Bali ikumbukwe kwamba wakati wa awamu ya 5 ambako vifo na maiti nyingi ziliripotiwa huko baharini na kwenye viroba , Dr Tulia alikuwa Naibu Spika na hakuwahi kushauri taarifa zile zifichwe.
========
Spika Tulia Ackson amesema kuwa ongezeko la mauaji huenda linatokana na kuripotiwa sana kwa taarifa za mauaji kutoka kwa polisi kwenda kwa vyombo vya habari hivyo taarifa hizo kuwa kama ni nzito na watu kuona huenda ni jambo la kawaida na kwa kuwa limetokea kuko na kule nao kuona hata wao wanaweza kufanya yaani ni kitu chepesi tu kujitoa uhai.
Ameshauri Wizara ya mambo ya Ndani watafute njia za kukabiliana na tatizo la mauaji yatokanayo na wivu wa mapenzi hasa kwa kuanza kushirikisha watu wa chini kabisa wawaulize kwa nini wivu wa mapenzi huenda wakapata njia za kumaliza tatizo hilo.
Hii ni layman solution.ukiweka mambo/mapungufu mengine pembeni utaona kuwa hili ni wazo zuri,,
Yaani hii itazuia watu wengine wasichukulie poa suala la kujiua.
Hata mimi kabla yake nilikuwa nishatoa maoni kama hayo ndani ya jukwaa hili!
Siyo maadili pekee bali Sheria za ndoa na mapenzi zibadilishwe haswa swala talaka, kupimana ugonjwa wa akili na Sheria za kazi zibadilishwe ziendane na teknolojia ya Sasa yaani kazi zifanyike masaa 24 na elimu ya vijana wakubwa iwe masaa 24 hata kilimo kiwe usiku na mchana iwe nikupumzika masaa machache tu kwaajili ya shift Ili kujenga jamii ya kuwajibika na inayowaza kujenga nchi na uchumi na siyo jamii ya kizembe na inayowaza mapenzi muda wote, hata tunaweza kuanza na bunge kama mfano, imagine siku hizi hata za ulinzi zinafanyika mchana kuliko usiku, kazi za hospital zinanyika mchana na usiku huduma hakuna Sasa kama siyo kujenga jamii ya kizembe na inayowaza usiku familia zote za ndoa zilale kwaajili ya mapenzi tu kama wanyama mpaka akili zinageuka za kinyama.Bila kusitiza maadili nadhani mengine ni makelele tu