Spika Tulia ameshindwa kujibu maswali badala yake kaongea vitu ambavyo hajaulizwa kwa kupanic na mhemko

Spika Tulia ameshindwa kujibu maswali badala yake kaongea vitu ambavyo hajaulizwa kwa kupanic na mhemko

Ukisikiliza vizuri anasema ameshajibu hilo swali mara nyingi hapo awali tena alikwenda Urusi baada ya Raisi zelensky na speaker wake kusema hawatakuwepo ukraine wanaenda kuhudhuria mkutano Ulaya au marekani na mialiko yake huko ukraine ipo ofisini kwake wakachukue
CHADEMA na hasira zao za kijinga. Media za kimataifa zinampongeza Spika Tulia lakini nchini kwake wapo vijana wanadai hakujibu vizuri maswali, hawa ni wa kuachana nao tu.
 
Angeishia apo tu ingetosha sio kujizalilisha vile halafu wanawake wanapenda kujitilisha huruma kanakwamba wanaonewa vile
Sio kweli, hujaelewa maana zinazojificha kwenye baadhi ya maswali haswa wanapomuona kiongozi ni wa jinsia ya kike.

Ilibidi awaeleze kwa kirefu kwani inaonekana kwa muda wa mwaka mmoja aliodumu kwenye cheo hicho zimekuwepo jitihada za kutaka kumchukulia kama vile haielewi kazi yake.
 
Tulia hajazuiwa kwenda urusi alipaswa ajibu swali na sio kupanic na kuaza kupayuka kama vile sio msomi bhn
Nafikiri hamjamsikiliza vizuri. Watanzania kama kawaida mmekimbilia kumhukumu kuwa amejibu kwa kupanic. Kuna maneno haya ameyasema ingawa sitanukuu kama yalivyo lakini maana ni ileile, " I have responded to these questions several time". Unapata maana gani? Hivi kama watu walewale wanauliza swali lilelile kila muda unafikiri alikosea kuongea kwa namna ile aliyoongea? Unafikiri hakuna vikao vya ndani vya committee vilivyomuuliza swali hilohilo moja na wakaamua kuliuliza tena kwenye mkutano unaorushwa live?

Agenda ya watu wa magharibi inaeleweka ndio maana aliamua kujibu kwa njia ile. Hawapendi kuongozwa na mtu mweusi, hawapendi mtu mweusi ajue udhaifu kupitia viti vya uongozi walivyovitengeneza wenyewe. Watahakikisha hapewi muhula mwingine wa kiti hicho kama ilivyo kwa mhindi mweusi wa Uingereza.

Tulia anajua anapambana na watu wa aina gani. Majibu ya aina hiyo kuna wakati hujibiwa na viongozi wengi duniani baada ya kuchoshwa na mashambulizi onevu yanayoelekezwa kwao.
 
Yaani rais Tulia Ackson lugha yake ya mwili hata kabla ya kufikia muda wa kuulizwa maswali live alikuwa amesha changanyika, ingawa maswali hayo siyo ya papo kwa hapo, tayari walishawasilisha kama kanuni za mabunge zinavyoelekeza. Hii ilimpa muda wa kutosha kujitayarisha, lakini pamoja na hisani hiyo ya kiutaratibu wa kibunge aka - panick.

Labda kuna kitu anakijua kama impeachment n.k kinakuja na hii rasharasha ya maswali ni mwanzo wa wabunge kusuka jambo kubwa juu ya uwezo wake ..
Mfululizo wa maswali yanayoelekea kufanana kwa kutoka kwa wabunge inaonekana kuna kitu hakiko sawa ambacho wabunge wanakijua.
 
Kinafiki tu kama kawaida yetu wabongo. Huyu dada wanamsifia hata hao wazungu kwa kuweza kusimama dhidi ya ubaguzi wa mawaziri wa Ulaya.

Tanzania nchi aliyotoka kuna wajuaji kuliko hao mawaziri, kuliko hao watu wa media za kimataifa.

Siasa mbovu za CCM na CHADEMA zinatengeneza kundi kubwa la wajinga.
Mojawapo ni wewe mkuu
 
Mbona dada yetu amejibu vizuri tu!!Tena kwamamlaka,Japo Ka Uccm nimekaona.😂
 
Angekuwa ni debe tupu asingekuwa Rais wa bunge la CPU, kuonana ana kwa ana na Putin au kiongozi wa ngazi hiyo sio mchezo.

Wabongo katika ubora wetu wa dharau za vijiweni. Kila kitu kukichukulia kwa uzito mwepesi tu. Sio mada za Simba na Yanga kupewa nafasi ya kuongoza bunge la kidunia.
Uongozi wanapewa kwa kupokezana sio kwa sababu nyingine yoyote ile mkuu. Uliwahi kugundua hilo au ymegundua leo?
 
Ukiacha ushabiki na mihemko ya uchawa ukweli ni kuwa spika ameshindwa kujibu moja kwa moja maswali aliyoulizwa badala yake aka[anoc na kuhemka na kuanza kunibu maswali kwa maswali badala ya majibu.

Hakukuwa na haja ya kuunda dhana zisizo kuwepo kwamba wanaomuuliza kwamba labda wanamdharau au kunafikra za kikoloni au wanadhani kwakuwa anatoka nchi ya chini kabisa hivuo hawezi kuongoza nk.

Spika kajibu na kuongea vitu vingi visivyokuwa na maana kuonesha kuwa anauwezo na kwamba waulizaji wanamdharau.

Yeye alitakiwa kutoa ufafanuzi wa moja kwa moja kukingana na swali na siyo kuanza kulalama na kufoka. Kwa sisi linguists na sychologists tathmini yetu ni kuwa spika alikasirika bila kukasirishwa akidhani wanamdharau.

Spika tayari alikuwa na inferiority complex akataka kuwaonesha kuwa yeye ni strong wakati waulizaji hawakutaka na hawakuwa na mawazo havyo. Spika ajitahidi kuwa mtulivu na kuto kujibu kwa makelele kulalamika na kufoka lile siyo bunge la CCM kama alivyozoea kuwafurusha akina Mpina.

Wengi wanaomsifia ni kuwa hawana uelewa wao ni kama mashabiki wa Simba na Yangu they are not analytical.

Pia soma
- Tulia Ackson awataka viongozi wa magharibi kumheshimu. Ni baada ya kushambuliwa kuhusu kukutana na Vladmir Putin
Acheni wivu, madam kaongea point... Kama umekatwa... Tuambie we ungeongeaje?
 
Uongozi wanapewa kwa kupokezana sio kwa sababu nyingine yoyote ile mkuu. Uliwahi kugundua hilo au ymegundua leo?
Hata kupewa uongozi katika taasisi hiyo sio jambo dogo, humo ukumbini kuna wasomi wangapi wanazeeka na kustaafu bila ya kupewa hiyo nafasi ya urais?. Siku zote kwepa akili za kibongo za kudharau kila kitu.
 
Ukiitwa mtanzania mnyonge kataa kwa nguvu zote mkuu hao ndio mtaji wa ccm.. na wanapowaita wanyonge wanamanisha a (wajinga, hawana ellimu, exposure, poor reasoning arguementation)
Haswaa....sijawahi kukubali hilo jina
 
Wana JF wengi wenu hasa wanaume suruali mna wivu na chuki kali sana, hua najiuliza ni maisha yamewapiga sana huko kitaa au ni tatizo la afya ya akili? mnajitia wajuaji kwenye kila kitu watu wenyewe exposure hamna hamjawahi hata kuizunguka nchi yenu mmebaki na mawazo mgando basi kichefu chefu tu,
Acheni wivu kwa watu waliowazidi akili, maarifa na mali mnazidi kujikosesha baraka na kuzidisha umaskini kwenye familia zenu.
 
si kweli gentleman,
unapotosha. Kajibu maswali ya wabunge wenye mihemko sana kwa ufasaha mno na ameongea kimamlaka na kuwaambia ukweli wabunge kwamba wasifikiri alikotoka bado wako chini ya wakoloni na hahitaji ruhusa kutembelea Ukraine wala Russian kwa mapenzi bali ni utaratibu na wajibu wa bunge hilo kufanya hivyo kote ulimwenguni 🐒

..masuala ya ukoloni yanahusiana nini na maswali aliyoulizwa?

..hoja ya ukoloni ni kichaka cha kukimbia maswali, sawa na ilivyo hoja ya jinsia.
 
si kweli gentleman,
unapotosha. Kajibu maswali ya wabunge wenye mihemko sana kwa ufasaha mno na ameongea kimamlaka na kuwaambia ukweli wabunge kwamba wasifikiri alikotoka bado wako chini ya wakoloni na hahitaji ruhusa kutembelea Ukraine wala Russian kwa mapenzi bali ni utaratibu na wajibu wa bunge hilo kufanya hivyo kote ulimwenguni 🐒
Kulikuwa na haja gani ya kuwaambia, 'wamheshimu, au natoka nchi ndogo au wasiwe na fikra za kikoloni',

Haya yote kiuongozi ni kuonyesha hali ya kutojiamini inferiority complex, kwanza hakuulizwa haya pili kwani wao (wazungu) hawajui kuwa anatoka kwenye nchi ndogo.
 
..masuala ya ukoloni yanahusiana nini na maswali aliyoulizwa?

..hoja ya ukoloni ni kichaka cha kukimbia maswali, sawa na ilivyo hoja ya jinsia.
Kweli mkuu, yeye kwenda kwa Putin kunahusiana vipi na ukoloni au yeye kutoka kwenye nchi ndogo.
 
Back
Top Bottom