Spika Tulia: Barabara ya Dodoma - Iringa inajengwa upya lakini haina umri wa kujengwa upya

Spika Tulia: Barabara ya Dodoma - Iringa inajengwa upya lakini haina umri wa kujengwa upya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Akson ameisisitiza Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) kuhakikisha miradi yote ya barabara inayokamilia inapimwa ubora kwa kutumia vifaa maalum kabla ya Makandarasi kuikabidhi kwa Serikali akitoa mfano Barabara ya Dodoma – Iringa ambayo imekuwa na mashimo mengi licha ya kuwa haina muda mrefu tangu ilipojengwa.

Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wamenunua Laser Crack Measurement System (Mtambo maalumu wa kupima ubora wa barabara) ambao umeanza kufanya kazi. Sasa barabara kabla ya kukabidhiwa Serikali, itakuwa inapimwa ubora kwa kutumia Mtambo huo

Dkt Tulia amesema hayo tarehe 27 Mei 2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akifungua Maonesho ya siku mbili ya sekta ya Ujenzi ambapo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya kwenye uwekezaji wa eneo la miundombinu ya Barabara.

Aprili 19, 2024, Mdau wa JamiiForums.com alisema Barabara hiyo ni hatari kwa usalama wa Watu na vyombo vinavyopita kutokana na kuwa na mashimo mengi, akadai TANROADS Dodoma wamekuwa wakijaza udogo kwenye mashimo hayo jambo ambalo hakisaidii

Pia soma
 
Back
Top Bottom