PreGE2025 Spika Tulia: Mshahara wa Mbunge hauna tofauti kubwa na wa mtumishi wa Umma

PreGE2025 Spika Tulia: Mshahara wa Mbunge hauna tofauti kubwa na wa mtumishi wa Umma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ntarudi ukiona mtu ana shepu na urefu kama wa shetani huyo sio wa kawaida
 
Hii dhana ya Mishahara ni Siri ya Mtu wakati Walipwaji wanalipwa kwa Kodi zetu?
Mbona tunatangaziwa Kiasi cha Kodi kilichokuwa Collected?

Usiri wa mishahara ubaki kwenye Sekta Binafsi ila Huko Government tunatakiwa sisi wananchi ambao ndio maboss za Hao watumishi na wawakilishi wa Umma Tujue Wafanyakazi wetu wanalipwa kiasi gani.
 
Spika Tulia amesema mshaara wa mbunge hauna utofauti na mishaara na watu anaolingana nao katika kada ya utumishi wa umma, pengine watu awafahamu kwamba mbunge ni sehemu ya mtumishi wa umma.

Sielewagi hata uwe msomi wa level ya juu kbs duniani but ukishaingia ndan ya CCM kwishaa habari yako, ni unapuyanga tu!!
 
Kashiba kande huyu na kuona watanzania wengine ni manguruwe! Tabia za kuvimbiwa kawaida zipo namna hii...
 
Hapo angesema mshahara wa Mbunge unalingana na wa mtumishi wa Umma wa ngazi ya juu kidogo ingekuwa afadhali.
 
Tumeanza kutukanwa walimu sasa.
Walimu lazima mulaumiwe kama kazi yenu ni kufundisha hawa vilawa wanaotaka kuuaminisha uma kwamba mapato ya mbunge ni sawa na ya DC? angetutajia, ni DC gani huyo ambaye huwa anapewa kiinua mgongo cha milion 240 baada ya kustafu ndani ya miaka 5?
 
Huyu sijui alipataje uspika aisee. Halafu ana dharau na kejeli balaa.
 
Aisee, hatari sana hizi ni dharau za moja kwa moja kwa za kwa walipa kodi.
 
Back
Top Bottom