Spika Tulia: Tusiweke mazingira ya kuonesha kuwa kila anayepotea amechukuliwa na Vyombo vya Dola. Tusitumie mihemko

Hawa ndiyo wasomi bobevu kiwango wa PhD ( think tank) wanayojivunia wanachama wa chama dola kongwe CCM
 
Kikao cha Bunge la chama kimoja Dodoma 2024

BUNGE LA KUMI NA MBILI MKUTANO WA 16 KIKAO CHA 3 TAREHE 29 AGOSTI, 2024 ASUBUHI, DODOMA

 
Atuelezee kwanini wanapelekwa karakana ya osterbay? Hao watekaji access ya kuhifadhi mateka wamepewa na nani?
 
Nani anawajibika kulinda usalama wa raia katika Nchi?
 
Cjawah kuw ccm au chadema wala chama chochote lakn ukwel n kwamba cna iman na polis wet, matukio ya utekaji kwa kipindi hik menge ynausishwa na jeshi letu au wat wnaotmia gar zenye usajil wa STL asa najiulza huyu spika hawaz hata kdg kwann wat wna ihusisha selikal yetu, inaumiza sana ila ipo cku t mana kila jambo lna mwanz na mwsho.
 
Upotoshaji huu uliasisiwa na serikali awamu ha sita ikiongozwa na Dkt Samia pale aliposhadadia kusema serikali ya awamu ya 5 ilihusika na viroba. Nadhani ni muhimu kuweka rekodi sawa, Dkt Samia ajitokeze tena akemee matukio ya watu kupotea afanye reference mpaka awamu ya 5, lasivyo jamii ni ngumu sana kuamini kuwa serikali haihusiki.
 
Mh Spika kakosea sana kujaribu kupoozesha hoja ya mbunge namsikitia kwa kuwa bado haijatokea kwake au jamaa yake wa karibu.

Mantiki ni hii hapa, vyombo vya dola ndio vinavyojaribu kutengeneza mazingira ya kwamba wanaopotea huenda wanauwawa na waganga wa kienyeji lakini cha ajabu kati ya wale wote wanaotajwa na kulalamikiwa hakuna hata mmoja aliyepatikana ameuwawa na mganga wa kienyeji!!!!

Pili, kuna watu wanaona watu wanaotekwa na watu wanaojitambulisha wanatoka vyombo vya dola.

Kati ya wale wote waliobainika na kupatikana kwa waganga wa kienyeji hakuna hata mmoja aliyetajwa kwamba alitekwa na kwamba alikuwa mwanasiasa!!!

Mamlaka za nchi ziache utani kwa malalamiko halisia
 
Uzuri huna mtoto, ungekuwa naye afu apotee ili uonje uchungu wa uzazi.
 
Natamani sana siku moja hawa watu wafikishwe kwenye mikono ya haki wawaelezee waTanzania maana ya fikra zao hizi.
Hawa wakitoka madarakani halafu waachwe tu na kuendelea na maisha yao kana kwamba hawakusababisha usumbufu wowote kwa wananchi itakuwa siyo sawa hata kidogo.
 
Ni kweli
Maana tuna shuhudia wengine wanagundulika wameuwawa na wapenzi wao wakati awali watu wakijua wametekwa na vyombo vya usalama
Wakati wa JPM alisingiziwa sana kuhusu utekaji na uuaji. Hamna mbunge aliyenyanyua mdomo kutetea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…