mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Spika amepotoka CAG anakagua fedha za umma.
Bunge ni kikao cha wananchi na wananchi ndio waajiri wakuu wa watendaji wa Serikali.
Hivyo wanayo haki za msingi kupatiwa majibu ya tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.
Hakuna Sheria iliyo juu ya haki hii ya msingi ya wananchi kufahamishwa kuhusiana na utendaji wa Serikali.
Kwamba ile mijizi inayotafuna kodi zetu na iendelee kuiba tu wala hakuna ajabu! Nchi ina ufala mwingi sana hii!!Nafikiri sijaelewa chochote.... Naomba kueleweshwa hili... Mimi Kama mwananchi wa kawaida.
SPIKA wa Bunge Dk. Tulia Ackson amesema serikali haitalazimika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakati wa Mkutano wa Bajeti unaoendelea na kwamba Bunge halitachukua hoja zitakazochangiwa na Mbunge kuhusu ripoti ya CAG kwa sababu Mkutano wa sasa wa Bunge ni wa Bajeti na si kujadili ripoti hiyo.
Mbona ndio taratibu. Hata hawa wanaoshutumiwa wengine wanaweza kukutwa hawana makosa. Baada ya kuhojiwa unaweza kukuta wagaguzi zipo taarifa au nyaraka hawakuweza kuziona au kuzipata kwa wakati wa ukaguzi. Sema kuna wizi au ubadhilifu mkubwa na ushahidi uko wazi hatua zinabidi kuchikuliwa hata kabla ya taratibu za kibunge kukamilika.
Ndiyo 'udikteta' huo.SPIKA wa Bunge Dk. Tulia Ackson amesema serikali haitalazimika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakati wa Mkutano wa Bajeti unaoendelea na kwamba Bunge halitachukua hoja zitakazochangiwa na Mbunge kuhusu ripoti ya CAG kwa sababu Mkutano wa sasa wa Bunge ni wa Bajeti na si kujadili ripoti hiyo.
Bi mkubwa alisha foka "STUPID", hiyo ni adhabu tosha kwa hao wote waliohusika!Spika amepotoka CAG anakagua fedha za umma.
Bunge ni kikao cha wananchi na wananchi ndio waajiri wakuu wa watendaji wa Serikali.
Hivyo wanayo haki za msingi kupatiwa majibu ya tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.
Hakuna Sheria iliyo juu ya haki hii ya msingi ya wananchi kufahamishwa kuhusiana na utendaji wa Serikali.
Ni kweli Chama ni watu.Bi mkubwa alisha foka "STUPID", hiyo ni adhabu tosha kwa hao wote waliohusika!
Kuna jibu umepewa hapo juu na mwanaCCM mwenzako 'Bishwaro'. Inaelekea baadhi yenu ndani ya chama chenu hamuelewi haya yanayofanyika yanamhusu nani.
Hivi hadi uambiwe ni kwa faida ya chama chenu ndipo utambue?
Dah!Ni kweli Chama ni watu.
Ila hakuna mahali kwenye ripoti ya CAG imetajwa CCM kuhusika.
Yametajwa maeneo yanayosimamiwa na watu.
Hivyo hayo ni matendo binafsi ya watu na sio kikundi cha watu wenye kuamini falsafa moja.
Hapa wanawajibishwa watu kwa matendo binafsi.
serikali haitalazimika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)