Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amesema serikali haitalazimika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amesema serikali haitalazimika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Hoja ya Spika ni dhaifu sana!! Ila hana jinsi!! Yaani fisadi kupewa muda wa kusafisha nyumba aliyoichafua hadi mwezi wa tisa!! Baada ya hapo utetezi utatokea na wabunge watasema sawaaaaa!!!
 
Spika amepotoka CAG anakagua fedha za umma.

Bunge ni kikao cha wananchi na wananchi ndio waajiri wakuu wa watendaji wa Serikali.

Hivyo wanayo haki za msingi kupatiwa majibu ya tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.

Hakuna Sheria iliyo juu ya haki hii ya msingi ya wananchi kufahamishwa kuhusiana na utendaji wa Serikali.

Kwani hilo bunge limechaguliwa na wananchi ama serekali ya Magufuli? Ingekuwa wamechaguliwa na wananchi wangekuwa na ulazima wa kujadili ripoti ya CAG, kwa sasa wanafanya kinachotakiwa na serikali na sio wananchi.
 
Huyu naye anakuwa hajielewi, kama hadi Kuna kuwaga na Baraza la Madiwani Maalumu kwenye Local Government kujadili Hoja za CAG kwanini Bunge lishindwe kujadili.

Kweli Kikulacho Kinguoni Mwako, Madam President should watch it out
 
Nafikiri sijaelewa chochote.... Naomba kueleweshwa hili... Mimi Kama mwananchi wa kawaida.
Kwamba ile mijizi inayotafuna kodi zetu na iendelee kuiba tu wala hakuna ajabu! Nchi ina ufala mwingi sana hii!!
 
Kama spika amesema hivyo hajatumia busara, yanayoweza kupata majibu, yajibiwe kwa faida ya uma, yasiyo na majibu yasubiri wakati wake.
Spika kuonesha upande kwenye mjadala bungeni hakusaidii serikali bali kuongeza mzigo baadaye, pia kuongeza shaka zaidi kwa uma kuhusu umakini wa serikali.
 
SPIKA wa Bunge Dk. Tulia Ackson amesema serikali haitalazimika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakati wa Mkutano wa Bajeti unaoendelea na kwamba Bunge halitachukua hoja zitakazochangiwa na Mbunge kuhusu ripoti ya CAG kwa sababu Mkutano wa sasa wa Bunge ni wa Bajeti na si kujadili ripoti hiyo.
Mbona ndio taratibu. Hata hawa wanaoshutumiwa wengine wanaweza kukutwa hawana makosa. Baada ya kuhojiwa unaweza kukuta wagaguzi zipo taarifa au nyaraka hawakuweza kuziona au kuzipata kwa wakati wa ukaguzi. Sema kuna wizi au ubadhilifu mkubwa na ushahidi uko wazi hatua zinabidi kuchikuliwa hata kabla ya taratibu za kibunge kukamilika.
 
SPIKA wa Bunge Dk. Tulia Ackson amesema serikali haitalazimika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakati wa Mkutano wa Bajeti unaoendelea na kwamba Bunge halitachukua hoja zitakazochangiwa na Mbunge kuhusu ripoti ya CAG kwa sababu Mkutano wa sasa wa Bunge ni wa Bajeti na si kujadili ripoti hiyo.

Ndiyo 'udikteta' huo.

Huyu sasa anajiona Bunge ni mali yake, anayo hiari ya kuamru tu anachotaka yeye!

Au kisha pewa amri toka kwenye mhimiri mwingine, asithubutu kuruhusu jambo hilo lijadiliwe.
Huu ndio utaratibu wa nchi yetu ulivyo mbovu.
 
Spika amepotoka CAG anakagua fedha za umma.

Bunge ni kikao cha wananchi na wananchi ndio waajiri wakuu wa watendaji wa Serikali.

Hivyo wanayo haki za msingi kupatiwa majibu ya tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.

Hakuna Sheria iliyo juu ya haki hii ya msingi ya wananchi kufahamishwa kuhusiana na utendaji wa Serikali.
Bi mkubwa alisha foka "STUPID", hiyo ni adhabu tosha kwa hao wote waliohusika!

Kuna jibu umepewa hapo juu na mwanaCCM mwenzako 'Bishwaro'. Inaelekea baadhi yenu ndani ya chama chenu hamuelewi haya yanayofanyika yanamhusu nani.
Hivi hadi uambiwe ni kwa faida ya chama chenu ndipo utambue?
 
Ni kweli Chama ni watu.

Ila hakuna mahali kwenye ripoti ya CAG imetajwa CCM kuhusika.

Yametajwa maeneo yanayosimamiwa na watu.

Hivyo hayo ni matendo binafsi ya watu na sio kikundi cha watu wenye kuamini falsafa moja.

Hapa wanawajibishwa watu kwa matendo binafsi.
 
Dah!

Naamini kwa maksudi tu hutaki kuelewa.

Hao watu wapo hapo kwa hisani ya CCM na wanafanya kazi kwa maelekezo ya CCM.
Viongozi ndani ya CCM wameamua njia nzuri ya kupata pesa ya kukipigania chama ni hii ya kukwapua mali za wananchi.
Ndiyo maana huoni jitihada za kuwajibisha wahusika toka kwenye mamlaka, na sasa akina Tulia wanatengeneza njia za kuondoa joto kwa maksudi kabisa.
Hao watu binafsi unaowasema ni vifaa tu vinavyotumiwa na chama.
 
serikali haitalazimika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Basi bunge letu huru la wananchi litaendelea kuichambua ripoti ya CAG kwa niaba ya wananchi

Pia mikutano ya hadhara ya kisiasa itaendelea kuelimisha na kuwachambulia ripoti ya CAG wananchi kote nchini, kwani bunge la Dodoma la chama kimoja cha CCM limeshindwa kujadili ripoti ya CAG
 
Back
Top Bottom