butron
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,640
- 7,943
Hiyo tisa,kumi kuzuia Bunge kujadili ripoti ya CAG iliyojaa ubadhirifu wa kutisha.Sasa ana rekodi gani ya Bunge lake kuheshimu Utawala bora mpaka achuguliwe kuwa Spika wa Bunge la Dunia!SPIKA Tulia Ackson anajipigia debe kuchaguliwa kuwa Rais wa Bunge la Dunia huku akiwa na Kashfa kubwa ya Bunge la Tanzania kuridihia Mkataba wa kuuza bandari zote za Tanzania kwa Mwarabu.
Bila aibu anagombea nafasi hiyo ili akauze mali zote za dunia nzima kwa waarabu?
Tulia ameshindwa kuendesha Bunge la Tanzania ataweza kuongoza dunia? tuache unafiki jamani tunaompigia debe tulia.
Tumesahau Bunge lake hivi majuzi limetunga sheria ya kuruhusu kununua ndege chakavu, meli chakavu, mabehewa chakavu, vichwa vya treni chakavu leo anapata wapi sifa za kuwa spika wa dunia?
Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app