Spika wa Bunge la Tanzania Tulia Akson Mwansasu bado haamini kama Polisi Tanzania wanahusika na utekaji na mauaji ya Wanachi

Spika wa Bunge la Tanzania Tulia Akson Mwansasu bado haamini kama Polisi Tanzania wanahusika na utekaji na mauaji ya Wanachi

Boi Manda

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2023
Posts
388
Reaction score
506
Akiongea na na Watangazaji wa kipindi cha asubuhi Good Morning cha Wasafi radio Septemba 27, 2024 Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Akson Mwansasu ameshangaa Jeshi la Polisi kuhusishwa na utekaji na mauaji ya raia wema

Hivi karibuni vijana watatu wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) walitekwa na watu wanaodaiwa wasiojulikana na mpaka sasa hawajapatikana

Pia mzee Kibao alishushwa na watu wenye siraha kali za kivita na pingu kwenye basi la Tashirif pale Tegeta Jijini Dairisalama na baadaye kukutwa eneo la Ununio akiwa marehemu huku amajehiwa vibaya

Pamoja na matukio hayo bado spika wa wa Bunge ambao ndio muhimili wa uwakilishi wa wanachi anaona Polisi na Serikali wanasingiziwa hawahusiki kwenye masakata hayo

Kwa maoni yangu Bunge ndio chombo kinachoisimamia Serikali nilitegemea wawe mbogo juu ya uharifu huu wa wanachi dhidi ya muhimili wa Serikali lakini kwa bahati mbaya au nzuri wamekuwa watetezi wa Serikali baadala ya kuwa watetezi wa wanachi ambao Wabunge wao ndio wanaowawakilusha Bunge

Nchi hii inahitaji mabadiko makubwa ya katiba ili mihilimi hii mitatu Serikali, Bunge na Mahakama ijitegemee kila mmoja uwe huru hapo ndio haki zitatendekq na nchi itapiga hatua za maendeleo

Serikali iliyopo madaraka inatakiwa kukubali kukosolewa na kujirekebisha makisa yake ili nchi isonge mbele

Mchezo wa drafti una tabia moja nzuri ambayo naipenda waangalizi wa nje ambao sio wachezaji wanaona makosa na fursa za ushindi kuliko wachezaji lakini huyo huyo akifanikiwa kuwa mcheji hawezi fursa alizokuwa akiziona alipokuwa nje ya mchezo

Nchi za Magaharibi zinepata maendeleo makubwa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa kutokana na strong opposition party natamani nchi yangu Tanzania tuwe na strong opposition party ili tosonge mbele

Soma Pia: Kuelekea 2025 - Spika Dkt. Tulia na Wabunge wa CCM wagomea hoja ya watu kutekwa na kuuawa kujadiliwa. Wananchi Tuwaambie "YOU ARE FIRED"


Kwenye nchi za wenzetu huko duniania mihili inajitegemea na haiingilia kwa mujibu wa katiba zao

Lakini huku kwetu dunia ya tatu rais anakuambia muhimili wa Serikali ndio baba lao mizizi yake imejichimbia chini na kwamba wao ndio wenye hazina ya oesa na wanatoa fedha kwenye mihimili mingi ili ijiendeshe


Comasa
 
Back
Top Bottom