Akiongea na Wasafi FM leo Spika wa bunge Mh. Tulia Ackson amesema anashangaa kwanini hadi leo hii polisi bado inamshikilia Kombo Mbwana kada wa CHADEMA.
Mbwana alipotea tangu June 15 baada ya kutekwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana huko Tanga, awali polisi ilikana kuwa naye baadae ikakiri kumshikilia.
Tulia amesema "siyo sahihi kwa polisi kumshikilia mtu bila kutoa taarifa kwa jamii kwa sababu inaweza kuzua taharuki".
Alikuwa akijibu swali aliloulizwa na Waandishi wa habari kina Kitenge, 'ni kwa nini Polisi inakamata watu na kuwaficha bila kutoa taarifa hii inapelekea jamii kuhisi kuwa polisi inahusika na utekaji'.
Tulia aliongeza kusema, hili ni changamoto na linahitaji marekebisho ya sheria.