Spika wetu anapotamka 'Sank You' badala ya 'Thank You'

Spika wetu anapotamka 'Sank You' badala ya 'Thank You'

Kwa hali hii bora aongee uswaa tu, ngeli ngumu jamani asikudanganye mtu! Wengine kabla ya kuongea lazima tutafsiri toka kisubi au kisukuma ndo twende kwenye uswaa badae Ngeli sasa mkuu unategemea nini kama si ze yu ze mi. Mwingine atakwambie DONT PULL THE CIGAR. Kwa kiswahili jibu unalo!

Duh mkuu, niko alone harafu nacheka ka sina akili nzuri hapo kwenye blue kha!
 
Mi naona sawa tu, speaking english is not an issue! What we want from her is a significant balance during the debate hours in the Bunge and eventually be the reasonable bridge towards getting back our deprived opportunities to developing our country. It is too earlier to judge her.
 
Semeni yote mimi sielewi kama wabunge naspika wanajua ngel au swa ninacho hitaji
Mabadiliko yakatiba ya nchi
Tume huru ya uchaguzi
TAKUKURU ivunjwe
UWT uvunjwe

Hakika tuta onana wa baya, kama mnakumbu story ya mlenga shabaha basi wabunge wajiaandae
 
Wewe unashangaa ya spika tu! Heee! Wagombea je?

Kilichonisikitisha ni uwezo mdogo kabisa kabisa wa wanasiasa hawa kujieleza kwa lugha hiyo maana naamini walijiandaa.

Kumbe tatizo siyo hesabu tu, Nadhani tukiendelea kuwachunguza huenda hakuna kinachoeleweka bungeni.

Sasa naona chanzo cha wakenya kutuburuza huko East Africa Community. Kujieleza ni hivyo, je, ukizuka ubishi itakuwaje?


Hapo kwenye BOLD.... I took my masters......
 
kwa kweli Lugha nimeona ni Utata mkubwa kwa wabunge wetu...ila Mwanasheria Lissu yupo Sawasawa ...Yaani wakenya wapo juu kweli ..wabunge wabongo hata kuuliza maswali walikuw wanaogopa
 
Senki yu mama. ngelesa yako inapwaya sana. Sasa veve ikipata jazba itawesa kweli ngeresa!!
 
matamshi mengine yana sababishwa na lafudhi ya sehemu mto anapotoka, ukiwa wa kasikazini unaweza kuwa na rara nyingi tu ukiwa wa nyanda za juu kusini L L nyingi tu, matokeo yake unapata zambi zako mwenyewe. oh ups sank you.
 
Mheshimiwa spika tatizo lake sio hii lugha ya kikoloni pekee hata anavyotamka baadhi ya Majina ni utata mtupu hii ni mifano michache: Badala ya kutamka Tundu Lissu yeye alitamka Lindu Lissu na hii imetokea zaidi ya mara moja. Badala ya kutamka Mizengo Pinda yeye anatamka Mizengwe Pinda sasa ije chiingereza msameheni tu jamani kwa maana lafudhi tamu ya kibena haijamtoka.
Napendekeza wenye CV yake watuletee ili tujue alibobea kwenye fani gani isiyo na uhusiano na lugha ya kikoloni.
 
Infwakiti, kuongea kiingereza vizuri sio kigezo cha kuipeleka Tanzania yetu kwenye maendeleo ya kweli. Sidhani kama vichaa wa London au New York, kwa kuwa wanaongea vizuri zaidi kiingereza basi waje watuongozee nchi. Tunachotaka sisi ni mabadiliko ya kweli, hatujali yanakuja kwa lugha gani. Go parent and bring your home because you are drinking ze cigar in ze school
 
Sasa mbona sheria nyingi wanazotunga zipo kwa kimonbo?
 
Jamani hamuwezi kutuwekea ka video tuone mambo yalivyokuwa?
 
Is this 'no school' or?

Lakini sioni ajabu manake hata mkuu wa nchi lugha inampa shida pia, akiwa anatoa speech za kiswahili mbwembwe nyingiii! aki swap kuongea ki MISSION kigugumizi kinaanza, manake hiyo THE itarudiwa rudiwa mara kibao, du! sasa kama hali ndio hii lakini kwanini wasibadilishe mfumo wa elimu nchini?
 
Kwa hali hii bora aongee uswaa tu, ngeli ngumu jamani asikudanganye mtu! Wengine kabla ya kuongea lazima tutafsiri toka kisubi au kisukuma ndo twende kwenye uswaa badae Ngeli sasa mkuu unategemea nini kama si ze yu ze mi. Mwingine atakwambie DONT PULL THE CIGAR. Kwa kiswahili jibu unalo!

mkuu, hiyo ya "dont pull..." ni kali sana! imenivunja mbavu
 
Au labda mother tongue??? Msimlaumu sana maana ungumbaru haujui kama we Speaker bana
 
mi sioni kama kimombo ni ishu. hata mimi nina degree kibao lakini sijui vizuri kimombo, sembuse huyo mwenye advanced diploma moja? kimombo ni ligha tu wakuu, tuangalie masuala mengine. mnajua watu wa afrika magharibi wanavyoongea kiingereza au wakenya wanavyozungumza kiswahili? sasa tunaweza kujinasibu kuwa tunawazidi nini wote hao?
 
Nilicho-note leo kwake ni kwamba kila kwenye "H" anaiondoa yaani kwa sisi wataalamu wa kiswahili tunasema UDONDOSHAJI na pasipo stahili "H" yeye anaipachika kwa mf; tusishangae kesho atakaposema mheshimiwa "RAHISI" hawa akina KAMWENE wanamatatizo ya lugha kidogo! ale yuve
 
Back
Top Bottom