Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Katika hili sakata,
1. Inashangaza kwamba spika ndio umekuwa wa kwanza badala ya Waziri Bashe au upande wa serikali kumtaka Mpina alete uthibitisho au maelezo kwamba Waziri Bashe amelidanganya bunge katika suala la upungufu wa sukari na mchakato mzima uliofutia wa manunuzi ya sukari ya ziada nje ya nchi.
2. Inashangaza kwamba unasema Mpina amekiuka taratibu za bunge kwa kuwasilisha taarifa yake mbele ya umma wakati kanuni za bunge zinakataza kuwasilishwa kwa umma taarifa mahususi ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuwasilishwa bungeni. Taarifa ya Mpina ni mahususi? Mbunge akisema bungeni Tanzania ina raia milioni 70 halafu mbunge mwingine akabisha kwa kuonyesha ripoti ya sensa inayoonyesha Watanzania wako milioni 60 hiyo taarifa ya sensa inakuwa taarifa mahususi?
Kuna umahususi gani kwenye kusema fulani amedanganya na kutumia taarifa au nyaraka public kuonyesha uongo wake?! Hata hivyo taarifa ya Mpina bado sio mahususi kuwasilishwa bungeni kwa sababu spika au kamati yake wanaweza wasiiwasilishe bungeni, hio sio taarifa kama taarifa rasmi za kamati za bunge, hotuba za bajeti au kamati teule kama ile ya Mwakyembe sakata la Richmond ambazo hakuna namna spika anaweza kuzuia kuwasilishwa bungeni.
3. Jambo la kushangaza zaidi spika anaisifia serikali kwa utulivu! Kwa kukaa kimya na kutojibu hoja za Mpina!. Hapa mimi ndio nimechoka zaidi.