Mkuu Sumu si kila nukuu inafaa kila sehemu na kila wakati!
Hii nukuu ukimpelekea mtoto anaye soma secondary school ata kushangaa!
Hii nukuu ukiwapelekea watu ambao wako universities hapa Tanzania watakushangaa na kukulaumu!
Hii nukuu kama Kanumba angekuwa hai lazima Ray ange kosolewa maana kwa jinsi kanumba alivyo kuwa anawaza kimataifa lazima wote mgemshangaa Ray!
Ray target yake ni local market na hafikirii kuja kufanya film na wanaigeria au watu wa mataifa .....
Hii nukuu akiiona mtu anayewaza kufanya biashara kimataifa kila Leo mfano Ay Lazima akushangae!
Hii nukuu akiiona mchina atafurahi maana yeye uchumi wake una mruhusu kuto kuwa na ulazima wa kukijua na anaweza kuweka mtafsiri!
Hata wachina nao hulazimika kujifunza kiswahili ili wawasiliane nasi na tusiwatapeli!
Mahitaji yanawafanya watu kujifunza lugha fulani na bila shaka hata we we ukienda china kukaa miezi sita lazima utataka kujua maneno Fulani ya kichina ili uwasiliane!
Huo mfano wa mesi hebu kuutafakari anawasiliana vipi? Hapo jibu lazima liwe kuwa ana mtafsiri maana anayo pesa ya kuajiri mtafsiri!
Leo hii watanzania mnasema kingereza ni ulimbukeni lakini mmesahau Mh Mlugo alisakamwa kwa kushindwa kuongea kingereza ..... ...
Watanzania hatujafikia hatua ya kukikataa kingereza maana uchumi wetu bado unatulazimisha kukijua!Hivi unge sema nini kama Diamond ange kwenda kwenye tunzo akashindwa kuwasiliana na wenzie kisa hajui kingereza? Hapa swala ni kuwasiliana si kukitumia kuimba!
Safi sana mkuu upo sahihi kabisa
Last edited by a moderator: