Yanga wanaondolewa mashindanoni kwa penalti.
Leopards wanapata penalti 4, Yanga wanapata penalti 2
Muda wa kupigiana penalti.
Dakika 93: Mwamuzi anakamilisha kipindi cha pili, sasa ni hatua ya penalti.
Dakika ya 93: Mwamuzi anamuonya kipa wa Leopards kwa kuchelewesha muda.
Dakika ya 92: Yanga wanapata kona, anapiga Juma Abdul inaokolewa.
Dakika ya 91: Kipa wa Leopards anapata mpira anauchezea, anaonekana anapoteza muda.
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 88: Kipa wa Yanga, Dida anafanya kazi nzuri ya kuokoa hatari, ilikuwa nafasi ya wazi kwa Leopards.
Dakika ya 85: Kasi ya Yanga imepungua na mchezo umekuwa mgumu kwao.
Dakika ya 80: Yanga wanafanya mabadiliko mengine, anaingia Said Juma Ally, anatoka Maka.
Dakika ya 72: Mchezo umeongezeka kasi, Leopards wapo makini hasa kipa wao, Otieno.
Dakika ya 68: Yanga wanafanya mabadiliko mengine, anatoka beki Pato Ngonyani, anaingia Babu Ally.
Dakika ya 60: Yanga wanafanya shambulizi kali mara mbili mfululizo lakini wanakosa mmaliziaji wa mwisho.
Dakika ya 51: Mabadiliko mengine kwa Yanga, anaingia Said bakari anatoka Emanuel Martin.
Dakika ya 50: Yanga wanafanya mabadiliko, Yusuph Muhlu anatoka nafasi yake inachukuliwa na Saimon kutoka kikosi cha vijana.
Dakika ya 48: Yanga wanakuwa na kasi kubwa ya kutafuta bao.
Kipindi cha pili kimeanza.
MAPUMZIKO
Dakika ya 45: Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza, matokeo bado ni 0-0.
Dakika ya 42: Yakub Ramadhani wa Leopards anacheza vizuri na Kateregga, wanajipanga vizuri katikati ya uwanja.
Dakika ya 39: Kateregga wa Leopards anafanya shambulizi lakini lakini kipa wa Yanga, Dida anauwahi mpira na kuudaka.
Dakika ya 32: Mashabiki wa Yanga wanashangilia timu yao kuongeza hamasa ya ushindi.
Dakika ya 30: Juma Mahadhi wa Yanga anatanguliziwa mpira lakini anashindwa kuuwahi.
Dakika ya 25: Mchezo unaedelea na timu zote zinamiliki mpira kwa zamu.
Dakika ya 20: Leopards wanajipanga vizuri na kujibu mapigo ya kushambuliwa.
Dakika ya 16: Yanga wanafika langoni mwa Leopards lakini kipa anauwahi mpira na kuudaka.
Dakika ya 15: Juma Abdul anachezewa faulo na Yakub Ramadhani, mwamuzi anamuonya mchezji huyo wa Leopards na kuwa faulo.
Dakika ya 10: Juma Abdul anashirikiana na Emanuel Martine kutenenezea mashambulizi kwa Yanga lakini bado mambo ni magumu.
Dakika ya 8: Yanga wanaonekana kucheza kwa kuchangamka, wanatumia zaidi winga wao kutengeneza mashambulizi.
Dakika ya 3: Mchezo umeanza kwa kasi na timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Mchezo umeanza..
Huu ni mchezo wa Nusu Fainali wa SportPesa Super Cup unaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.