SPORTPESA SUPER CUP SPECIAL THREAD: Taarifa za Mechi zote na matokeo yote mpaka Ubingwa

SPORTPESA SUPER CUP SPECIAL THREAD: Taarifa za Mechi zote na matokeo yote mpaka Ubingwa

Kaacha mill 60 anamkimbiza Simba huu ni utani wa jadi wa damu
 
Yanga kujeni hapa mjibu mashambuliz aya. Sikufarahia timu zetu zitolewe zote lakni afadhal huku mtaani tunaheshimiana sasa
 
Sijui niseme nini. Ila iko namna hii. Kwanini mmeshindwa kuyapa heshima mashindano ya SportPesa super cup?

Mmeona wenzenu walivyokuwa wanajua kutumia fursa? Au ndio tuseme kuwa mil 60 kwenu nyinyi ni ndogo sana...?

Ngoja nianze na "Dar es salaam Young Africans SC''. Hivi nyinyi, tena hasa nyinyi ndio mmetia fora sana kwenye hii michuano.

Kwanini hamkuipa uzito sana hii michuano? Msinipe sababu kuwa wachezaji 8 ambao ni First Choice wote hawapo!

1. Tambwe
2. Hajji
3. Bossou
4. Kamusoko
5. Niyonzima
6. Msuva
7. Kessy
8. Beno

Mkinipa hiyo sababu, nitawauliza kwanini mmewapa mapumziko wachezaji hawa ambao kwa namna moja au nyingine wangeweza kushindana (ambao wengi wao ni Second Choice (SC)).

1. Mwashiuya (Rested)
2. Yondani (Rested)
3. Barthez (Rested)
4. Busungu (Rested)
5. Osca Joshua (Rested)
6. Zullu (Rested)
7. Matheo Anthony (Rested)

8. Ngoma (Huyu tunajua ni Majeruhi)

Hivi nini lengo lenu la kutumia wachezaji wengi wa Under 20? Kwani mmeambiwa kuwa hii ni michuano ya pre season? Acheni dharau. Mwambusi alipoulizwa kwanini wanatumia kikosi hiki ambacho ni dhaifu kwenye michuano hii, alijibu kuwa Anatafuta wachezaji wa kuwapandisha 11 eleven ya Kikosi kikuu pamoja na kuwafanyia majaribio wachezaji 2 waliosajiliwa

Kikosi cha Dar Young Africans SC kwenye michuano ya SportPesa Super Cup.

FC - First Choice Player
SC - Second Choice Player
NP - New Player
U20 - Under 20 Player

1. Munishi (FC)
2. Abdul (SC)
3. M Ally (U20)
4. Nadir (SC)
5. Andrew (SC)
6. Pato (SC)
7. Mhilu (U20)
8. Makka (U20)
9. Obrey (FC)
10. Martin (SC)
11.Mahadhi (SC)
12. Samwel Greyson (U20)
13. Babu Seif (NP)
14. Mbaraka Jumanne (U20)
15. Bakari Othman (U20)
16. Said Mussa (U20)
17. Ema Kichiba (NP)



Siku nyingine kama mnadhani hii michuano ni ya majaribio ni kheri mkaomba nafasi yenu ichukuliwe na wengine wenye nia ya kushindana.

USHAURI; kwa waandaaji wa michuano ya SportPesa Super Cup. waandaaji wanapaswa kuangalia hili suala la kuandaa michuano kipindi ambacho kila klabu inawacgezaji wake muhimu ili kuondoa visingizio vya wachezaji muhimu kukosekana.


yanga.jpg
 
Mkuu nimekuelewa sana aisee

Nyinyi yanga mnadharau sana! Kwanini (Licha ya kuwa na kikosi ambacho kingeweza kutumika) mmeamua kutumia Vijana wa Under 20?

Acheni dharau, Mil 60 sio ndogo....ukizingatia mishahara iligonga mwamba mwezi jana...
 
Kaugonjwa ka. Muro bado kanawatesa,maneno meeengi pumba tupu.Haya sasa leteni story.
 
Nyinyi yanga mnadharau sana! Kwanini (Licha ya kuwa na kikosi ambacho kingeweza kutumika) mmeamua kutumia Vijana wa Under 20?

Acheni dharau, Mil 60 sio ndogo....ukizingatia mishahara iligonga mwamba mwezi jana...
Mipango ya benchi la ufundi hiyo mkuu
 
yanga mafundi wew..ach kutuweka level moja na simba.wakenya daraja la pili tu nyie simba mmewashndwa,sijui huko uarabuni shirkisho mkienda kushrik mtafanya nin?
 
Back
Top Bottom