SPORTPESA SUPER CUP SPECIAL THREAD: Taarifa za Mechi zote na matokeo yote mpaka Ubingwa

Turudi kwenye usajili sasa japo jirani najua mpunga umekata hali ni tete majembe yanakuja yanachungulia magorofa then yanaxepaaaa
 
Hakika wahenga walisema ukiona mwezio ananyolewa nawe weka Maji.Timu ya AFC Leopard ya Kenya imeibamiza Yanga ya Tanzania bao 4-3 Na kuikosesha sh.Milioni 60 ambazo zingetumika kusajili.Yanga ilijigamba kuwa Simba umeikimbia baada ya kufungwa Na Nakuru ya Kenya.Je kama Simba iliikimbia Yanga Je Yanga kamkimbia nani?
 
Yanaga bana kama waimba taarab, maneno mengi hawaja kamilisha ukio, wangelipata kombe wangesema wanalitoa zawadi kwa simba, acha walikose warudi kuchangisha hela za usajili.
 
Kamkimbia Everton..si kwa mishuti ya Lukaku
 
Hah hah mkuu haya mambo ya kutegemea baadhi ya wachezaji yanatugharimu sana hapa bongo! Ukiacha timu ngeni katika mashindano haya Singida United, mathalani Simba na Yanga zinatuaibisha sana..kuondoka kwa wachezaji baadhi waliokwenda kuzitumikia timu zao za Taifa imekuwa ni janga kubwa sana..waliopo wameshindwa kufunga hata goli moja ndani ya muda wa dakika 90 kweli hii ni aibu! Bado tuna safari ndefu kama Taifa kisoka na itatuchukua muda mrefu sana kufika pale tunapopataka!
 
Kuna mtangazaji wa kituo cha Magic fm anaitwa Kilumanga ni shabiki wa Yanga kindakindaki basi akitangaza habari za michezo anaiponda Simba vibaya ila yanga anaisemea vizuri hatakama jambo analolizungumzia halijaikakia hiyo Yanga vizuri.
Kama leo asubuhi ameipamba kweli Yanga nikamuombea tu kwa Mungu atimize haja ya moyo wangu na namshukuru Mungu kwa kunisikiliza.
 
Hapo yanga amemfuata simba. akufaaye kwa dhiki, ndio rafiki [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] yanga na simba wana mapenzi ya dhati kweli kweli. Timu zetu za kibongo hizo, mwingine ana tamba kabla hajajua hatima yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…