Mimi siku zote huwa nasema na nitasema siku zote , sumu ya simba ni HAJI MANARA. Kwa mtu Mwenye akili timamu na anaejua Job Description ya Public Relation officer hawezi kumpa hiyo kazi Huyo Manara.
Kitengo cha habari cha team ni moja ya sehemu nyeti katika taasisi yoyote bora duniani. Ile ni taaluma. Watu wanapita vyuoni wanasomea hayo masomo.
Ndio maana huwezi kumsikia msemaji wa PSG ya ufaransa akisema wataifunga timu yoyote/kuidharau timu yoyote eti kwasababu wanafanya sajili zenye gharama kubwa duniani. Si tu PSG hata wasemaji wa timu zote kubwa duniani hali ni hivyo ( MANCHESTER UNITED, REAL MADRID, BAYERN, CHELSEA N.K)
Kama mashabiki wa timu ya simba wangekuwa wanajua kazi na majukumu ya PR na anachofanya Manara wangekuwa wameshaandamana kumzuia asiendelee kuonekana kwenye ofisi za simba.
Najua kuna changamoto za benchi la ufundi. Ila kuna mambo mengi hayapo sawa kwenye ofisi ya PR. Ambayo ni kikwazo kwa maendeleo ya timu.
Sent using
Jamii Forums mobile app