Springs city garage (wachina) ya Mwanza, huduma zao ni bora? Kunyoosha bodi ya gari

Garage kubwa zote ndo wanachofanya. Hata dealership.

Ndio maana bei zao zimeenda shule.

Rangi ya mjapan gari zinakaa hadi 5 years bado iko vizuri kimuonekano.

Hivi hizi rangi za kurudishia kwenye magereji huwa zinadumu kweli? ama zinapauka mapema?

Maana kuna jamaa yangu mmoja alirudia rangi gari zima kwenye hizi gereji za kiswahili. Baada ya miezi 7 hivi, pale juu ya boneti pakawa rangi inababuka na kuwa muonekano tofauti hivi.
 
Wapo vizuri sana, ilikuwa arusha niliminya mlango wa gari yangu kipindi naiingiza ndani, mlango ukaminya nguzo ya geti wakaninyioshea kwa 250k, wapo expensive lakin kazi ni nzuri nzuri sana
 
Kwa nini usipereke maraha auto gereji pale furahisha wapo vizuri halafu ni waswahili bei mnabageini

Gereji za waswahili wenzetu mapungufu ni mengi mno mkuu. Mfano: gereji unakuta haina booth ya kupakia rangi. Unakuta gari inapuliziwa rangi uwanjani nje kwenye upepo na vumbi letu hili la bongo.
 
Wapo vizuri sana, ilikuwa arusha niliminya mlango wa gari yangu kipindi naiingiza ndani, mlango ukaminya nguzo ya geti wakaninyioshea kwa 250k, wapo expensive lakin kazi ni nzuri nzuri sana

Walikuwa ni gereji ya wachina? Vipi hadi sasa muda gani umepita, rangi waliyopiga haijapauka?
 
Rangi ya mjapan gari zinakaa hadi 5 years bado iko vizuri kimuonekano.

Hivi hizi rangi za kurudishia kwenye magereji huwa zinadumu kweli? ama zinapauka mapema?

Maana kuna jamaa yangu mmoja alirudia rangi gari zima kwenye hizi gereji za kiswahili. Baada ya miezi 7 hivi, pale juu ya boneti pakawa rangi inababuka na kuwa muonekano tofauti hivi.
Sijawahi piga rangi gari yangu.

Kwahiyo sijui chochote kuhusu hilo.
 
Back
Top Bottom