Swala la pampu ishu sio hizo diameter. Unaweza ukanunua fittings ku adjust diameter. Kinachotakiwa kny pump ni kuangalia capacity yake, yaani discharge capacity kiasi gani (m3/h) na kitu kinaitwa Head (m), yaani uwezo wa kuinua maji. Nikupe mfano mdogo.
Let's say una pump maji kutoka kny kisima chenye kina cha 20m na sprinklers zako zina pressure ya 300kPa (=30m). Ina maana unahitaji pump yenye uwezo wa kupandisha maji kwa at least 50m, yaani 20 za kutoa kny kisima na 30 za kuumeet pressure ya sprinklers. To be safe ongezea kama 10m nyingine kwa ajili ya head loss kny pipes na fittings, au kama kutakua na mwinuko knye shamba pia unatakiwa uongeze. Hivyo utahitaji kuselect pump yenye Head ya 60m. Kila pump inakuaga na operationg curve, inayoonyesha Discharge capacity vs Head.
Sasa kama kwa mfano unahitaji kutumia sprinklers 2 kwa wakati mmoja, jumulisha discharge zake, kwa mfano kama kila moja ina 0.5m2/h, maana yake unahitaji pump itakayoweza ku deliver 1m3/h kwa pressure ya 60m.