St. Francis Mbeya kuna siri gani?

St. Francis Mbeya kuna siri gani?

Hivi pale St. Francis Girls Mbeya pana siri gani wazee? Mwaka huu licha ya kwamba imekuwa ya pili kitaifa lakini ufaulu wake ni wa ajabu na kuogofya sana.

Picha linaanza darasa lina watahiniwa 92 ambao wote wamepata div 1, hii si ajabu sana ajabu ni hili hapa kati ya hizo 1- 92, div 1.7 ambazo ndo ufaulu wa juu kabisa nchi hii kwa upande wa olevel zipo 79 yani 1.7 pale St Francis Girls zipo 79 kama utapata shida kuelewa na maanisha hivi wanafunzi waliopta A saba kwenye jumla la masomo yao wapo 79.

Mwanafunzi wa mwisho pale yani mwenye ufaulu dhaifu au unaweza kuuita goigoi ama kilaza, mmoja ana div 1.14 na mwingine ana div 1.13 na wapo wawili pekee.

Mabinti wamejua kukung'uta aisee div 1.10 ipo moja, 1.9 zipo 6 na 1.8 zipo 4

Kama unadhani maajabu yao mwaka huu ni hayo tu basi Pole mabinti hawa wameendeleza maajabu mpaka kwenye Wanafunzi bora ambapo kumi bora imepambwa na wao.Hatari sana hii mwanafunzi 1-5 kwenye kumi bora anatoka kwao afu wanajichomeka others kwenye 6,kisha namba 7 wanarudi wao afu 8,9 wanajikongoja fedha na ilboru kisha kumi kitabe kabisa wanamaliza wao. Kifupi 10 bora wanafunzi 7 wote wametoka St FRANCIS.

1. Consolata Prosper Luguva - St. Francis Mbeya🔴

2. Butoi Ernest Kangaza - St. Francis🔴

3. Wllhemia Steven - St. Francis 🔴

4. Cronel John - St Francis🔴

5. Merry George Ngoso - St Francis🔴

6. Holly Beda Lyimo - Bright Future
Girls🔴

7. Brandina - St. Francis🔴

8. Imamu Suleiman - Feza Boys

9. Mfalme Hamis Madili - Ilboru

10. Clara Straton - St. Francis🔴

Huu ufaulu si wa kitoto, sasa nauliza siri yao hasa ni ipi maana tangu miaka hiyo hawa mabinti wamekuwa moto ina maana shule zingine wameshindwa kabisa kujifunza?

View attachment 2082037

View attachment 2082038
Swali lako lina jibu lahisi. Hii shule uwa wanachukua "cream" ya wanaofaulu mitihani ya darasa la saba. Kwa kuwa ni kimbilio la kila mtu basi wale "vipanga" woote wanaoongoza darasa la saba kitaifa ndio wanaochukuliwa na kunolewa kidogo...hizi shule zilizobaki "zinaokoteleza zalokauka"
 
Jack of all trades ,master of none .

We unadhani hawajui hilo

Ila wameamua kukomaa na olevel and it pay them handsomely
Thank you...that is the power of concentration at work...most of the owners start well, the problem comes when things turn well, they forget all about consistency, they only think about money, they increase the number of students with no consideration in other factors, and eventually they end up being normal...
WE HAVE SO MUCH TO LEARN FROM ST FRANCIS GIRLS...
 
Shule za vipaji maalumu za serikali nazo zinachuja wanafunzi.
Siku hizi zinachuja nina binti yuko huko vipaji maalumu anasema ukifeli kwenye pepa za mwisho. Wa mwaka unarudishwa shule ya kata yako[emoji2]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] laFA sana ww
Multiple choice, ndio uzuri wa mitihani ya siku hizi. Hata ukisahau kidogo, ndani ya majibu ulio wekewa pale jibu sahihi lipo, unakumbuka. Maswali ya how, why, explain, find etc yaliondolewa kurahisisha usahihishaji

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Kama ulishawahi pata hata A Moja kwenye vyeti vyako nyosha mkono au jifanye kama unajikuna tuone[emoji1787][emoji3577]
 
Bahati mbaya sana, baadhi tumesoma ila siyo critical thinkers. Pata muda nenda st. Francis shuleni, ingia ndani ya darasa, angalia nidham ya wanafunzi, morali ya ufundishaji, mazingira ya kujifunzia, support ya wazaz/walezi, gharama ya mafunzo, uongozi wa shule na usimamizi, upatikanaji wa vifaa na nyenzo za kufundishia. Utakubali matokeo Yao ni halisi. Kama una wasiwasi omba vyombo vya serikali na Dola vifanye uchunguzi watoke hadharani kueleza wamegundua nini. Nimekaa mbeya naifaham shule, nawafahamu baadhi ya walimu wake. Tumalize kujenga madarasa, tukamilishe matundu ya vyoo, tupandishe madaraja, tuwe na vifaa vya kufundishia na Kujifunza, tutafanyia vizuri huko mbeleni. Kiwango Cha uwekezaji kitatoa matokeo halisi ya uwekezaji huo. Uwe na amani moyoni
 
Multiple choice, ndio uzuri wa mitihani ya siku hizi. Hata ukisahau kidogo, ndani ya majibu ulio wekewa pale jibu sahihi lipo, unakumbuka. Maswali ya how, why, explain, find etc yaliondolewa kurahisisha usahihishaji

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Tujifunze jamani...mambo sio marahisi kiasi hicho...e.g kwenye maths f4, kama mwanafunzi hajaandaliwa vizuri, ni ngumu kufaulu ule mtihani.
1. Hakuna kuchagua maswali,mtahiniwa anatakiwa afanye maswali yote 14.
2. Mgawanyo wa maswali umebadilika, miaka ya nyuma kuna baadhi ya maswali yalikuwa yanawasaidia watahiniwa wengi kufaulu kwa kupewa alama nyingi, e. g Accounts...swali hili lilikuwa na alama 10 na watoto wengi walikuwa wanalipenda na wengi walifaulu(necta analysis), sasa hivi liko section A, swali la 7 na lina alama zisizozidi 6
3. Mitihani ya sasa inapima ubobevu(competency), mtahiniwa asipoandaliwa vema, anaweza asielewe matakwa ya swali husika.
4. Maswali yamejitosheleza, lazima mtahiniwa awe na spidi nzuri, bila hivyo hamalizi mtihani.
Kwa ufupi, mambo sio marahisi kiasi hicho!
 
Walau kuna watu mnaukubali uhalisia.Hawa wanaobisha,si wapeleke kwanza watoto wao tuone kama hata watapata hiyo nafasi ya kuingia pale
Wanaokataa wana sababu zao ambazo siyo njema hata moja:

1: Wawekezaji wa shule nyingine: Wanatumia mbinu ya kuiponda na kuisema vibaya St. Francis ili ikose soko,

2: Kutokutimia ipasavyo malengo yao au ya watu waliokua wanawatumainia: Malengo yanaweza kuwa ya kitaalama au kiuchumi, hivyo wanamwonea kinyongo kila anayefanya vizuri au shule iliyofanya vizuri,

3: Kiburi cha pesa cha kusifiwa: Kwasababu mwenye pesa ni mtu wa kunyeyekewa, kutukuzwa na kusifiwa, anakua hayuko tayari kumsifia yeyote, anataka asifiwe yeye tu,

4: Umasikini: Sizitaki mbichi hizi,

5: Udini na udhehebu: Dini ni njia ya kukufanya uwe na moyo safi na ufurahie mafanikio ya wengine, sasa kwanini usifurahie mafanikio ya taasisi nyingine?,

6: Roho mbaya: Mtu mwenye roho mbaya hana sababu, anakichukia kitu bila sababu maalum,

7: Imani iliyongeka mtaani St. Francis wananunua mitihani: Maneno haya yalikuwepo tangu zamani.
 
Special schools
Gallery_1642316520858.jpg
Gallery_1642316493012.jpg
Gallery_1642316440803.jpg
Gallery_1642316408906.jpg
Gallery_1642316378697.jpg
Gallery_1642316345235.jpg
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]nimesoma hapo funny thing toka enzi zetu wa mwisho alikuwa na 2 ya mwanzo
Hatukuwahi kuletewa mtihani wala majibu
Ila niwashauri tu Kama mnataka shule nyingine ziperform kama hivyo nendeni mkae week moja tu mtajifunza kitu
Hakuna uchawi wowote ni kitabu na sala kwa sana
Nilikuwa nasali jamani nusu niwe sister na mimi [emoji2]
Pale mtakuwa mnapiga sana novena [emoji1787][emoji1787]
 
Thank you...that is the power of concentration at work...most of the owners start well, the problem comes when things turn well, they forget all about consistency, they only think about money, they increase the number of students with no consideration in other factors, and eventually they end up being normal...
WE HAVE SO MUCH TO LEARN FROM ST FRANCIS GIRLS...
Ukifocus na kitu kimoja ukaweka nguvu zako hapo. Roho yako hapo, furaha yako hapo hapo na machozi yako hapo happ possibility ya kuwa mtabe ile mbaya kwenye hicho kitu ni kubwa sana sana saa aisee
 
watoto wale wanaandaliwa vizuri,pia washajengewa spirit ya kufaulu.

walimu wao wako strictly ukizingua uko nje ya duara yaani hawacheki na kima.

#watoto wapewe sifa zao bhna, wanajua
 
St Marian imefia wapi ?Ilikuja moto sana.
Marian girls na mazinde wana mambo mengi sana mara huku o level mara kule a level hawana concentration ndio maana siku hizi wanakuja na kusepa na wanarudi tena na wanapigwa upaja tena.

Marian
Mazinde
Kifungilo

Wamebakia na majina tu ila wapo wapo

Siku hizo tabora gilrs ni wakali kuliko izo shule nenda kacheki matokeo ya miaka mitatu nyuma uone
 
Unakutana na mzazi St. Kayumba picha linaanza

mtoto hana viatu (stress number 1)

Mzazi hela ya Ada analalamika (stress number 2)

Shuleni Choo cha kulenga na hakuna maji (stress number 3)

Watoto hawali shuleni na wala mzazi hataki kusikia mtoto ana njaa au hana anachojua anatakiwa asome (stress number 4)

Ukirudi shule mzee kalewa [emoji23] unatakiwa ukamuogeshe na uhakishe mbuzi zimekula, kuku ziko bandani, vyombo umeosha, matusi kutoka kwa mdingi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] (stress number 5)

Mwalimu anatoka na demu wako [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] na kakuonya atakufelisha ukiendelea kudate naye [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] (stress number 6)

[emoji23][emoji23]

Mtaendelea kumalizia wengine

Kinachofelisha shule zetu za kata ni njaa [emoji23][emoji23][emoji23], ujinga na umasikini [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Elimu ya siku hizi imekuwa mdebwedo sana! Ukitaka kujua hili waulize walimu wa vyuo na waajiri. Binafsi sio Mara moja nimewafanyia interview vijana kwenye mambo ya kazi na naishia kusikitika jinsi uelewa wao ulivyo wa mashaka.
Kuna kitu huwa kinashangaza sana, watoto wanafaulu vizuri ila kiuhalisia hakuna kitu,
Tatizo ni kuifanya elimu kuwa biashara, shule itafanya lolote ili kufaulisha watoto,iweze kupata wanafunzi wangu,
Hivi hamjawahi kujiuliza ni kwa nini serikali huwa inawang'ang'ania wazee waliostaafu kurudi makazini?
 
Bahati mbaya sana, baadhi tumesoma ila siyo critical thinkers. Pata muda nenda st. Francis shuleni, ingia ndani ya darasa, angalia nidham ya wanafunzi, morali ya ufundishaji, mazingira ya kujifunzia, support ya wazaz/walezi, gharama ya mafunzo, uongozi wa shule na usimamizi, upatikanaji wa vifaa na nyenzo za kufundishia. Utakubali matokeo Yao ni halisi. Kama una wasiwasi omba vyombo vya serikali na Dola vifanye uchunguzi watoke hadharani kueleza wamegundua nini. Nimekaa mbeya naifaham shule, nawafahamu baadhi ya walimu wake. Tumalize kujenga madarasa, tukamilishe matundu ya vyoo, tupandishe madaraja, tuwe na vifaa vya kufundishia na Kujifunza, tutafanyia vizuri huko mbeleni. Kiwango Cha uwekezaji kitatoa matokeo halisi ya uwekezaji huo. Uwe na amani moyoni
Ongezea na mishahara na marupurupu ya walimu

Hata shule iwe na majengo mazuri ,mavitabu mengi kama mwalimu hana motisha hapewi motisha unampa vitisho daily badala ya motisha ni kazi bure tu

Ofisi za walimu zimekaa kama stoo wakati kuna shule ukienda walimu wa kila dept wana ofisi yao kuna viyoyozi ,samani za kisasa ,wanapewa motisha kama posho na wanafunzi lake wakipata A anahesabiwa pesa kwa kilaA kwa nini huyu Ticha asikomae kufundisha na kuipenda kazi yake
 
Unakutana na mzazi St. Kayumba picha linaanza

mtoto hana viatu (stress number 1)

Mzazi hela ya Ada analalamika (stress number 2)

Shuleni Choo cha kulenga na hakuna maji (stress number 3)

Watoto hawali shuleni na wala mzazi hataki kusikia mtoto ana njaa au hana anachojua anatakiwa asome (stress number 4)

Ukirudi shule mzee kalewa [emoji23] unatakiwa ukamuogeshe na uhakishe mbuzi zimekula, kuku ziko bandani, vyombo umeosha, matusi kutoka kwa mdingi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] (stress number 5)

Mwalimu anatoka na demu wako [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] na kakuonya atakufelisha ukiendelea kudate naye [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] (stress number 6)

[emoji23][emoji23]

Mtaendelea kumalizia wengine

Kinachofelisha shule zetu za kata ni njaa [emoji23][emoji23][emoji23], ujinga na umasikini [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hahahhh
 
Back
Top Bottom