St. Francis Mbeya kuna siri gani?

St. Francis Mbeya kuna siri gani?

Endelea kukataa ila ungewah kusoma private kwenye shule inayofanya vzr hata usingeshangaa

Mm nimesoma prvt inayofanya vzr na form four yetu tulikuwa wa 18 kitaifa huku tukiwa na division 2 moja pekee

But nikusaidie tu mchujo wa kuingia form one walikuja watoto zaid ya 3000 ila shule ikachagua 200 tu ambao walipitia mchujo mara tatu kisha wakawekwa darasan dec nzima then january walim waliokuwa wanawafundisha ile dec wakasort watoto 150 pekee wengine 50 wakasepa home

Hapo kidato cha pili na cha tatu mchujo ni mkubwa sana

Tulipokuwa tunaingia kidato cha tatu tukaambiwa kabisa form four haizid watu 40 na hapo tuko 90 ivyo kupambana kwako ndo kufaul kwako

Wastan wa kuingia kidato cha nne ilikuwq 65 ufaul wetu ukawa mkubwa wakapandisha mpk 78 ndo tukapita watu 40 pekee

Hapo usisahau tukiwa kidato cha tatu tulimaliza topic zote za kidato cha tatu na cha nne

So form four hatukusoma topic yoyote tulishacover huko nyuma

Kidato cha nne tulifanya mitohani kama huo wa taifa 16 kabla ya necta yenyewe(na haikuwa inatungwa wala kusahihishwa na walim wetu walikuwa wanaenda mikoa tofaut kukodi walim bora ndo wanafanya hilo)

Usisahau kuwa tangu tuneingia kidato cha nne kazi yetu ilikuwa kufanya marudio ya topic za nyuma zenye shida/kujisomea na kubwa kabisa kuna walim ambao mara nyingi wanachaguliwaga kwenda kusahihisha mitihan ya taifa(walikuwa wanakodiwa kuja kutufundisha mitihan ya taifa inasahihishwaje? Marking scheme zao zinakuwaje? Hii ilitujenga namna ya kujibu mitihan ya taifa tofaut na mitihan ya shule

Bro kubali shule bora zina vitu vingi zina offer kwa mwanafunzi bora(ukumbuke pale hawaendi vilaza)
Hivi hapa ulikua unamjibu nani aisee?!!
 
Haujui tu

Binti zangu wamesoma hapo, najuwa ninachokisema.

Wana nidhamu ya hali ya juu.

Hata kama una mtoto legelege, akifika pale utashangaa likizo ya kwanza akirudi kwako atakavyokuwa amebadilika.

Wanastahili
Mkali hii mbona kama kamba? We watoto wa kupita mchujo wa ST Francis umewatoa wapi😂😂😂😂😂😂
 
Mzumbe, Kibaha, Tabora, Pugu, Uru, Maua, ST. James, Minaki, Kilakala walau Ilboru imetoa kimasomaso. Hizi shule tuzipambanie zirudi kwenye nafasi yake, nakumbuka jamaa mmoja 1999 alipiga 1.8 akamaindi kinoma ila six akapiga 1.3. Vijana siku hizi imekuajee
Hahahah hizi Ilboru, Kibaha, Mzumbe, Tabora, Kilakala na shule zingine kongwe za serikali zinakuwaga na majitu yenye akili za kutisha. Imagine mwaka 2006 Tanzania one form six katoka Tosamaganga. Raha ni kwamba hawa majamaa hadi chuo yanakimbiza hatari kabisa.
 
Na mkae mkijua st Francis wanafunzi wana masomo ya upishi na ushonaji so wanatoka na kaujuzi pia
 
Mkali hii mbona kama kamba? We watoto wa kupita mchujo wa ST Francis umewatoa wapi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Siyo kamba mkuu

Ona hiyo
IMG_20220115_235303_843.jpg
 
Daah hongera sana mzee wangu mi wa kwangu sijui atapiga one au ndo vitakua vya kurithi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jitihada na nidhamu na utulivu wa kiroho.

Mungu amsaidie.
 
Mimi binafsi nakataaa hayo matokeo aisee, hata kama wana akili huo ufaulu wa kiasi hicho kuna kitu cha ziada... Hiyo shule ichunguzwe vzuri kuanzia miezi mitatu kabla ya kufanya mtihani na siku za mitihani
Mitihani ya NECTA hutungwa na walimu kutoka shule kama hizo...Ilboru, Mzumbe, St Francis, Kibaha etc.

Lazima wafaulu kwa sababu maswali mengi wanakuwa wameyafanya kupitia mazoezi kujiandaa na Final
 
Sikia nikwambie mkuu maisha ya shule Mimi nayajua Tena zaidi ya unavodhani ...

Shule kubwa kama hizo ,zinawalimu wakubwa Sana wenye uzoefu wa hali ya juu ,na wanakuwa na connection na walimu wengine zaidi ..

Wanaotunga mitihani ni walimu kutoka kanda mbalimbali ,na wabobevu ,hutoa maswali na mwisho wa siku mtihani kitungwa ...

Utake usitake ,upende usipende hizi shule zinamazingira Safi ,walimu Safi ,lakini wananunua mitihani week kadhaa kabla ya pepar ,.....

Fuatilia mitihani wanayofuanya week mbili kabla ya mtihan pre -necta ,ready for necta ,hio ndio mitihan inayotolewa imejaa maswali yanayotoka necta ...

Sio kwamba wanasoviwa siku ya mtihan hapana ,wanafanya maswali yatakayotoka necta week kabla na walimu wanasisitiza kuyakalili ,....

Kama Kuna swali gumu ambalo linasahaulika ,basi mwalimu ataliimba darasana kila siku na mwisho wa siku wanalikuta necta ....

A inaanzia 81-100 ,bro mtihan wa physics , mathematics , biology , chemistry kwa watoto wote 97 wapate A ,???????? Hawa wa kibongo kabisa ? Woteeeee ? ....

Aiseee ,Mimi nakataa hayo matokeo ...hao watoto uwezo wao wa kawaida tu ,sio wa kupata huo ufaulu wote ,kwa kusema sijui walimu Bora ,mazingira Bora ,...
Unazungumziaje ilboru yenye 1.7 39?
 
Mimi binafsi nakataaa hayo matokeo aisee, hata kama wana akili huo ufaulu wa kiasi hicho kuna kitu cha ziada... Hiyo shule ichunguzwe vzuri kuanzia miezi mitatu kabla ya kufanya mtihani na siku za mitihani
Mkuu amini maana wanasimamiwa na watu wa Baraza
 
Elimu ya siku hizi imekuwa mdebwedo sana! Ukitaka kujua hili waulize walimu wa vyuo na waajiri. Binafsi sio Mara moja nimewafanyia interview vijana kwenye mambo ya kazi na naishia kusikitika jinsi uelewa wao ulivyo wa mashaka.
Siyo vijana tu, hata viongozi...imagine Rais anahimiza kabisa mawaziri wale kwa urefu wa kamba zao (meaning waibe)🤔
 
Mkuu hao ni walimu wako kwenye mfumo mzima ....


Unajua mitihani ya necta form four inatugwa vip? Kama unajua mtihani unatugwa vip ndio utaweza kukubaliana na Mimi kuwa kuvujisha maswali yanayotoka kwenye mtihani wa necta ni simple Sana....


Kama mnadhani ni uongo ....

Naomba mkafuatilie pepar wanazofanya hawa watoto kabla ya necta ...hapa namaanisha "pre -necta examination na "ready for necta"....

Baada ya kupitia hizo Pepar njoo uangalie necta ,ndio utajua hujui ....

Kwenye physics ,biology na chemistry practical ndio usiseme [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]yaani hapa uanaambiwa live kabisa kuwa ,swali la volumetric analysisi volume of acid (Va=23.6 ) hakuna haja ya kuhangaika na pipete ,Wala measuring cylinder ...

Biology sample zote za viumbe wanaambiwa ,na ndio vinatoka ..

Physics kwenye equilibrium ,electric current ,sample zote wanaambiwa ...

Watoto wanatafuniwa kila kitu kuanzia ,bwenini kufanya usafi ,shule kufagia wanafanyiwa ,kutandika vitanda ,vyooni kudekiwa ,Hadi kufuliwa nguo ,walimu wanawatafunia material darasani ,Hadi mitihani ya necta wanatafuniwa .....hao watoto wanachojivunia ni uelewa wa mambo mbalimbali kutokana na tour ,na safari mbalimbali mbunga za wanyama n.k ....Ni mayai mayai tu

Lakin mtoto wa vidumu na maji ni more powerful and creative ,ni vile tu kiingereza ndio inakuwa tatizo ...


Msiwe wajinga Sana ,[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mimi sio mjinga wala hapo hakuna udanganyifu.
 
Kuna binamu yangu amepata division three, nawaza kwenda kuappeal. Binamu yangu ni kilaza alietukuka. Amefaulu vipi?
 
Hivi pale St. Francis Girls Mbeya pana siri gani wazee? Mwaka huu licha ya kwamba imekuwa ya pili kitaifa lakini ufaulu wake ni wa ajabu na kuogofya sana.

Picha linaanza darasa lina watahiniwa 92 ambao wote wamepata div 1, hii si ajabu sana ajabu ni hili hapa kati ya hizo 1- 92, div 1.7 ambazo ndo ufaulu wa juu kabisa nchi hii kwa upande wa olevel zipo 79 yani 1.7 pale St Francis Girls zipo 79 kama utapata shida kuelewa na maanisha hivi wanafunzi waliopta A saba kwenye jumla la masomo yao wapo 79.

Mwanafunzi wa mwisho pale yani mwenye ufaulu dhaifu au unaweza kuuita goigoi ama kilaza, mmoja ana div 1.14 na mwingine ana div 1.13 na wapo wawili pekee.

Mabinti wamejua kukung'uta aisee div 1.10 ipo moja, 1.9 zipo 6 na 1.8 zipo 4

Kama unadhani maajabu yao mwaka huu ni hayo tu basi Pole mabinti hawa wameendeleza maajabu mpaka kwenye Wanafunzi bora ambapo kumi bora imepambwa na wao.Hatari sana hii mwanafunzi 1-5 kwenye kumi bora anatoka kwao afu wanajichomeka others kwenye 6,kisha namba 7 wanarudi wao afu 8,9 wanajikongoja fedha na ilboru kisha kumi kitabe kabisa wanamaliza wao. Kifupi 10 bora wanafunzi 7 wote wametoka St FRANCIS.

1. Consolata Prosper Luguva - St. Francis Mbeya🔴

2. Butoi Ernest Kangaza - St. Francis🔴

3. Wllhemia Steven - St. Francis 🔴

4. Cronel John - St Francis🔴

5. Merry George Ngoso - St Francis🔴

6. Holly Beda Lyimo - Bright Future
Girls🔴

7. Brandina - St. Francis🔴

8. Imamu Suleiman - Feza Boys

9. Mfalme Hamis Madili - Ilboru

10. Clara Straton - St. Francis🔴

Huu ufaulu si wa kitoto, sasa nauliza siri yao hasa ni ipi maana tangu miaka hiyo hawa mabinti wamekuwa moto ina maana shule zingine wameshindwa kabisa kujifunza?

View attachment 2082037

View attachment 2082038
Mkuu ukitaka ujue vizuri kuna nini pale, mpeleke mwanao halafu utakuja kutuambia umeona nini 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom