Hivi pale St. Francis Girls Mbeya pana siri gani wazee? Mwaka huu licha ya kwamba imekuwa ya pili kitaifa lakini ufaulu wake ni wa ajabu na kuogofya sana.
Picha linaanza darasa lina watahiniwa 92 ambao wote wamepata div 1, hii si ajabu sana ajabu ni hili hapa kati ya hizo 1- 92, div 1.7 ambazo ndo ufaulu wa juu kabisa nchi hii kwa upande wa olevel zipo 79 yani 1.7 pale St Francis Girls zipo 79 kama utapata shida kuelewa na maanisha hivi wanafunzi waliopta A saba kwenye jumla la masomo yao wapo 79.
Mwanafunzi wa mwisho pale yani mwenye ufaulu dhaifu au unaweza kuuita goigoi ama kilaza, mmoja ana div 1.14 na mwingine ana div 1.13 na wapo wawili pekee.
Mabinti wamejua kukung'uta aisee div 1.10 ipo moja, 1.9 zipo 6 na 1.8 zipo 4
Kama unadhani maajabu yao mwaka huu ni hayo tu basi Pole mabinti hawa wameendeleza maajabu mpaka kwenye Wanafunzi bora ambapo kumi bora imepambwa na wao.Hatari sana hii mwanafunzi 1-5 kwenye kumi bora anatoka kwao afu wanajichomeka others kwenye 6,kisha namba 7 wanarudi wao afu 8,9 wanajikongoja fedha na ilboru kisha kumi kitabe kabisa wanamaliza wao. Kifupi 10 bora wanafunzi 7 wote wametoka St FRANCIS.
1. Consolata Prosper Luguva - St. Francis Mbeya🔴
2. Butoi Ernest Kangaza - St. Francis🔴
3. Wllhemia Steven - St. Francis 🔴
4. Cronel John - St Francis🔴
5. Merry George Ngoso - St Francis🔴
6. Holly Beda Lyimo - Bright Future
Girls🔴
7. Brandina - St. Francis🔴
8. Imamu Suleiman - Feza Boys
9. Mfalme Hamis Madili - Ilboru
10. Clara Straton - St. Francis🔴
Huu ufaulu si wa kitoto, sasa nauliza siri yao hasa ni ipi maana tangu miaka hiyo hawa mabinti wamekuwa moto ina maana shule zingine wameshindwa kabisa kujifunza?
View attachment 2082037
View attachment 2082038