Maswali mepesi lakini mbona wanafunzi wengine kule Kazulamimba wanafeli? Hawa watoe strategies tujue wengine waige vipi. Inaniuma kuona karne hii wanafunzi wanashindwa kufaulu hata kidato cha nne. Kuna jamaa yangu alifeli form 2 nilisoma name shule moja ya ajabu ajabu uko. Juzi akanambia eti daktari alivyompima akamwambia anaumwa ugonjwa unaitwa "INFECTIONS", nikamuuliza mara mbili na akasisitiza sana.
Sasa taifa linakuwa na watu wa hivi hata kutumia mbolea shambani hawataweza, lishe kwa watoto hawawezi, uzalishaji wao kitaifa ni duni. Shule walienda kuishi, kuvaa sweta na kunywa uji. Elimu ya bongo hasa uswahilini uko ni ile wazazi wanawaambia watoto wao wakiwa wamefunga eti "mmetuchosha hebu shule zifunguliwe wazazi tupumzike". Hapo usitegemee maajabu ya kufaulu. Sasa hawa waliofaulu wangetoa strategies imekuwaje ingesaidia wengine