St. Francis Mbeya kuna siri gani?

Hizi one zingekuwa zinaonekana kwenye mchango wa maendeleo ya taifa tungekuwa mbali.
 
Mtu mzima kuwa muongo kwa kiwango hiki ni aibu kubwa sana,itendee haki JF,usitake kutufanya sote hapa ni hamnazo.Sote tunajua mchujo mkali kuanzia kupata nafasi pale, Mkuu usiwe na hasira kama mtoto wako hakufaulu vizuri kiasi cha kutuletea blah blah hapa.
 
Kama mtuani wa tume ulifuja na kupelekea mpk sas hawajatangaza Ni hatar sna wa iliboru respect


Ingawa pia utungaji wa mitiani hz za daras la sba Ni za kuchagua zote unashindwaje kuotee maaswal ukienda secondaries hawakunyi maswali San Kam zamani zetu 2005
 
Pia aina ya watoto wanaokwenda pale ni top cream kuanzia walikotoka,halafu mtu anatuletea hapa hadithi za Shule kununua mitihani😂
 
Unalosema ni kweli, angalia A zao ni za yale masomo ambayo wakipiga past paper za kutosha lazima wapate A. Waangalie katika physics Wana C na B za kutosha. Mwanafunzi akifundishwa vizuri mitihani ya kidato cha 4 ni rahisi sana kwa masomo ya sanaa.
 
Mitihani ya siku hizi hamna kitu 1. Rais wa kwanza wa Tanzania ni nyerer......... 2. Binadamu ana macho mawi.......
Pole sana ndugu. Mitihani ya siku hizi ni Competence Based Curriculum (CBC). Ni mitihani migumu kuliko ya zamani sema watu wanaichukulia poa kwasababu ya maswali mengi kuwa ya multiple choice. Lakini ukitaka kujua mitihani ya multiple choice ni migumu waulize madaktari.
 
Kama hakuna Janja Janja Nadhani ni uwezekazaji mzuri katika Elimu
 
Mimi binafsi nakataaa hayo matokeo aisee ,hata kama Wana akili huo ufaulu wa kiasi hicho Kuna kitu cha ziada ...hio shule ichunguzwe vzuri kuanzia miezi mitatu kabla ya kufanya mtihani na siku za mitihani
Ni hivi; kwanza tuelewe, kabla ya kuwachuja wanafunzi wanaochukuliwa, tukumbuke hata walimu waliochukuliwa (wanaofundisha pale), nao wamechujwa. Sasa hebu pata picha hapo; mwalimu amechujwa na mwanafunzi amechujwa (nadhani jibu unalo).

Jambo la pili, hawataki kuharibu (kupoteza sifa yao), hivyo wana mikakati (strategies) maalumu ya ufundishaji. Mwalimu anamjua kila mwanafunzi, uwezo na udhaifu (strengths and weaknesses), hivyo, penye mapungufu mikakati maalumu hufanywa na hatimaye kuziba pengo hilo. Unaweza kukuta hata ile prep, mwalimu anaingia na kuziba magap yote mpaka ahakikishe amejiridhisha. Hivyo, hakuna mwanafunzi anayeachwa nyuma, wote wanaenda sambamba; na ndio ufaulu huu tunaouona. Labda huu ndio uchawi wanaofanya.
 
Kwa hiyo hii shule tangu miaka ya 1990 wananunua mitihani na bado necta hawajawastukia! Necta imekuwa na wafanyakazi tofauti tofauti tangu miaka hiyo, je wote wanaopelekwa hapo ni corrupt kiasi hicho?

Fanya homework yako vizuri na siyo kuwapaka matope!
 
Achana na mawazo hayo. Unataka kusema shule nyingine zote za Tanzania zimekosa hela ya kununua mitihani na kuiacha st. Francis iongoze miaka yooote hiyo??
 
Hapo chini umeongea vizuri. Siri ya mafanikio ni mazingira mazuri pamoja na walimu wazuri. Kamawangekua wanategemea kusoviwa maswali basi wasingekua wanazingatia sana ile interview wanazowafanyia watoto wanapojiunga kidato cha kwanza.
Zile interview zinawasaidia wao kuchagua watoto bright "ZAIDI" na kuanza nao safari ya Olevel
 
Acha kudanganya watu hadharani hivi nina uhakika hata ilipo shule hii hujui na pili hujui kitu chochote kuihusu shule hiyo ndugu yangu zaidi ya chuki na wivuu hebu badilika aiseee
 
Hivi unataka kutuaminisha mnunuzi wa paper ni St.Francis tu na ndiyo maana wanafaulu kwamba miaka yote wameingia ubia wa kuuziwa paper! Hapa ndiyo tunakwama kupata ukweli badala ya kujifunza kutoka kwao namna wanavyofanikiwa tunajipoza kwa wananunua paper ndiyo tumemaliza
 
Mkuu kwenye Aya ya mwisho nimependa maoni yako, mdogo wangu alikuwa bogus kabisa, tukamhamishia shule X ipo mkoa X, alivyofika pale wakatushauri aanze form one, kipindi hicho alikuwa form 2, akaanza form one, kwenye matokeo yake ya form four, alimaliza na Div 3. Wote tulipigwa na butwaa maana hatukugemea, Kama angejitahidi kiasi kile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…