St. Francis Mbeya kuna siri gani?

St. Francis Mbeya kuna siri gani?

Chura

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2009
Posts
1,385
Reaction score
2,402
Hivi pale St. Francis Girls Mbeya pana siri gani wazee? Mwaka huu licha ya kwamba imekuwa ya pili kitaifa lakini ufaulu wake ni wa ajabu na kuogofya sana.

Picha linaanza darasa lina watahiniwa 92 ambao wote wamepata div 1, hii si ajabu sana ajabu ni hili hapa kati ya hizo 1- 92, div 1.7 ambazo ndo ufaulu wa juu kabisa nchi hii kwa upande wa olevel zipo 79 yani 1.7 pale St Francis Girls zipo 79 kama utapata shida kuelewa na maanisha hivi wanafunzi waliopta A saba kwenye jumla la masomo yao wapo 79.

Mwanafunzi wa mwisho pale yani mwenye ufaulu dhaifu au unaweza kuuita goigoi ama kilaza, mmoja ana div 1.14 na mwingine ana div 1.13 na wapo wawili pekee.

Mabinti wamejua kukung'uta aisee div 1.10 ipo moja, 1.9 zipo 6 na 1.8 zipo 4

Kama unadhani maajabu yao mwaka huu ni hayo tu basi Pole mabinti hawa wameendeleza maajabu mpaka kwenye Wanafunzi bora ambapo kumi bora imepambwa na wao.Hatari sana hii mwanafunzi 1-5 kwenye kumi bora anatoka kwao afu wanajichomeka others kwenye 6,kisha namba 7 wanarudi wao afu 8,9 wanajikongoja fedha na ilboru kisha kumi kitabe kabisa wanamaliza wao. Kifupi 10 bora wanafunzi 7 wote wametoka St FRANCIS.

1. Consolata Prosper Luguva - St. Francis Mbeya🔴

2. Butoi Ernest Kangaza - St. Francis🔴

3. Wllhemia Steven - St. Francis 🔴

4. Cronel John - St Francis🔴

5. Merry George Ngoso - St Francis🔴

6. Holly Beda Lyimo - Bright Future
Girls🔴

7. Brandina - St. Francis🔴

8. Imamu Suleiman - Feza Boys

9. Mfalme Hamis Madili - Ilboru

10. Clara Straton - St. Francis🔴

Huu ufaulu si wa kitoto, sasa nauliza siri yao hasa ni ipi maana tangu miaka hiyo hawa mabinti wamekuwa moto ina maana shule zingine wameshindwa kabisa kujifunza?

Screenshot_20220115-104943_Samsung Internet.jpg


Screenshot_20220115-104948_Samsung Internet.jpg
 
Mimi binafsi nakataaa hayo matokeo aisee ,hata kama Wana akili huo ufaulu wa kiasi hicho Kuna kitu cha ziada ...hio shule ichunguzwe vzuri kuanzia miezi mitatu kabla ya kufanya mtihani na siku za mitihani
Inawezekana lakini binafsi nishawahi ona mtihani wao wa geography namna wanaandika essay aisee nikalinganaisha na mwanangu wa Kajamba nani nikaona kabisa kuna tofauti mkubwa mno. Wale mabinti wanaandika essay point to point afu kitu clear sio mtoto anaandika essay afu point inafichwa fichwa ndani kama gaidi🤣🤣.....hawa mabinti kwa essay ni moto wa kuotea taliban, wanakuandikia essay afu wanakupangia kwa paragraphs kwa tumikogo kiasi kama vile Furthermore sijui nevertheless mara to begin with yani lazima msahishaji ufurahi.
 
Hio shule inanunua mitihani na kufanya mwezi mmoja kabla ya mitihani ya taifa na huwa maswali yanarudiwa kwa msisitizo mkubwa Sana ......

Hao watoto wanaomaliza huko hawana uwezo kabisa wa kufaulu hivyo, never ever....

Hapa bongo ukishakuwa na pesa hakuna kinachoshindikana, paper za NECTA zinanunuliwa na watoto Wana solve mapema kabisa ...

Hio shule ada yake tu unaweza kula mwaka mzima ,kununua pepar wizaran kupitia kwa mamuruki ni kitu rahisi Sana .....mbaya zaidi wafanyakazi wengi wa serikali dawa yao ni pesa ,kwa million 20 anakuletea pepar la necta lotee mwezi mmoja kabla .....


Niamaini Mimi haya nayoyasema
 
Hio shule inanunua mitihani na kufanya mwezi mmoja kabla ya mitihani ya taifa ,na huwa maswali yanarudiwa kwa msisitizo mkubwa Sana ......

Hao watoto wanaomaliza huko hawana uwezo kabisa wa kufaulu hivo ,never ever ,....

Hapa bongo ukishakiwa na pesa hakuna kinachoshinfikana ,pepar za necta zinanunuliwa na watoto Wana solve mapema kabisa ...

Hio shule ada yake tu unaweza kula mwaka mzima ,kununua pepar wizaran kupitia kwa mamuruki ni kitu rahisi Sana .....mbaya zaidi wafanyakazi wengi wa serikali dawa yao ni pesa ,kwa million 20 anakuletea pepar la necta lotee mwezi mmoja kabla .....


Niamaini Mimi haya nayoyasema
We endelea kushabikia mpira una low IQ sijawahi kuona kwa haya uliyoandika nimeamini kuwa upo na akili ndogo sana
 
Sie Waswahili tumewekeza sana kweny ufaulu na si ueleawa

Hizi division one kalikali zinapoteleaga wapi hadi hazionekani tena?

Tanzania one wa form four walio graduate sambamba na Samia Suluhu miaka hiyo sijui sasa hivi yupo pori gani wakati mwenzie sasa ni Rais?
 
We endelea kushabikia mpira una low IQ sijawahi kuona kwa haya uliyoandika nimeamini kuwa upo na akili ndogo sana

Mimi nimesoma chuo na watoto wanaotoka hizo shule mkuu ...

Siku ya mtihani wanakutana na maswali waliyokuwa wanasolve mwezi mmoja kabla ya NECTA...

Sio kwamba siku ya mtihani wanasoviwa hapa, ila paper linasoviwa week kadhaa kabla ya NECTA na hayo maswali ndio yanatoka NECTA, mbaya zaidi walimu wanawasisitiza.

Usiwe mjinga kuelewa mambo yanayoendelea huko ...

Wananunua mtihani, pamoja na kuwa na mazingira mazuri ya kusomea, walimu wazuri, malazi na ufundishaji mzuri ....wananunua mtihani mkuu ....
 
Watanzania tuko kinyume sana na mafanikio ya wengine......mioyo yetu na akili zetu muda wote zinatarajia habari mbaya na maanguko ya watu baada ya mafanikio......

Taarifa za mafanikio ya mtu au kikundi cha watu tunazipokea kwa mshituko wa chuki na hasira ili kufurahisha mioyo yetu hasi tunatafuta namna ya kuyatia doa mafanikio hayo.......

Wengi wetu hatutambui na kuthamini juhudi za watu wengine juu ya mafanikio yao badala yake tunawapachika majina mabaya......

Ili uishi Tanzania unatakiwa kuwaelewa watanzania na hawa ndio waTanzania kwa wingi wao......

Hongereni ST FRANCIS MBEYA juhudi zenu zimeonekana na kuwaangaza kwa watu wanaoshangilia na kufurahia mafanikio ya watu.....
 
Back
Top Bottom