St.Kayumba wote tukutane hapa Wazee wa kidumu na Maji

Nakumbuka nko darasa la nne ,,,,mm mzee wangu alkua mkuu wa shule niliyokua nasom so tukawa tunaish nyumba ya shule ilkua karibu na shule,,sas cku moja asubuhi tuko mstarini kuna wanafunz waliochlewa walkua wanachapwa,, acha mdogo wangu mdogo alkua miaka km mitano ivi akaropoka "mama njoo uone wanafunzi wanachapwa kam mbwa" acha shule nzima igeuke kuangalia ni nan mwenye ujasir wa kusema hivo wakakuta ni mtoto wa mwalimu mkuu, ikabd tu kupotezea hamna hata aliyeleta mdomo kuongea ongea…!!!
 
Nilivokua darasa la saba kulikua na mitihani ya mashindano, mnafanya mtihani shule kama 5 hivi...sasa shule yetu isiposhika nafasi ya 1 walimu wanaandaa siku maalumu halafu wanaagiza fimbo kwa madarasa ya chini sisi bila kujua.....aiseeh!!! Hiyo siku ikifika utasikia tunaitwa darasa flani hivi lipo tupu halina madawati wala nini, utasikia mwalimu wa darasa anasema "shikeni masikio mali ya serikali juu(makalio)" hapo fimbo zitatembea hatari......tukirudi darasani kila mtu hawezi kukaa

Sent from my HUAWEI Y330-U01 using JamiiForums mobile app
 
Tukunti yuu?
 
Nilianza st kayumba... Ila darasa tulikua tunajazana ile mbaya hadi wengine wanakaa chini... Kuna la kwanza A-F... Tunapangwa kwa akili. Nilikua darasa E. Mzee akanichongea dawati langu... Yaani ata nichelewe wananiachia nafasi kwenye lile dawati.
Mama alikua hanipi hela ya kutumia (walikua hawatuzoeshi kushika pesa kabisa). Atanipikia vitu na kuniwekea kwenye lunch box na water bottle ya kamba.. Mda wa mapumziko nakaa chini ya mti na rafiki zangu tunakula.

Mzee alinihamisha nikiwa darasa la nne!
 
Mkuu hiyo Id yako,nilipojiunga Jf kwa mara ya kwanza nilikuwa naitumia -kwa mwaka 1 badaye nikabadili

miliitoa kwenye wimbo moja unaitwa chupa 1
 
Nakumbuka walimu walikuwa na tabia za kututumikisha kama punda, walikuwa wametugeuza vibarua....pesa wana kula WAo

Siku moja walichukua pesa toka kwa mwanakijiji inakadiliwa laki 3, mwaka 1994 nikiwa la 3, tukaambiwa tukalime palizi katk shamba lake la ekari 5....

Siku hiyo nakumbuka hatukuingia darasani, SAA 2 asbh kuhesabu namba na jembe lako mkononi(toka nyumbani) kisha tukanyooka kwa mguu kwenda shabani, tukiwa njiani kaka na Dada zetu wa drs la 7 walianza kutupiga mkwara na kutuhamasisha kuwa tukiwa tunapalilia tuhakikishe either tunakata mzizi mkuu wa mhindi au tunang'oa vichwa kisha tunavirudishia'

Tulifika shambani tukiwa na yoga tukaanza kuchapa kazi huku tukitekeleza agizo la wakuu, by SAA 6 ekari 5 zilikuwa tayari zimepaliliwa na kungo'olewa vitop, kwa kuwa ulikuwa bado jua sio Kali usingejua.....

Yule mzee alivyorudi kesho yake.. Alikuwa mahindi yote yamesinyaa vichwa... Aki cha gani kuwa, alifika shuleni akipiga mayowe.....walimu walimuitia walinzi akafukuzwa, na kengere iliitisha watu, walimu kwa mkwara wakaanza kutuuliza nani aliyeleta mgomo ule, tuko kimya

Tangu siku ile hatukutumikishwa tena
 
Hahahahahahaah unakuta hata kunawa ulinawa hivo hivo......unakuwa kama vile ulikuwa unatumia kigimbi kama unyayo
Hahahaah....[emoji122] [emoji122]
Ukinawa unanawa upande wa mbele tu wa miguu na mikono... kupaka mafuta ni hivyo hivyo unapaka mbele nyuma ya mikono na miguu kweupe kumepauka kama nini[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hahahahaa hapo unajiona mjanja sana, alafu hujulikani.
Those days..............
Hata ukiambiwa nenda kaoge unaenda kupiga passport ukitoka unakutana na mzee anakuuliza umeoga kweli wewe .. unajibu nimeoga ... anachekaa tu maana kama kichwa kilikuwa na vumbi bado kimejaa vumbi miguu kigimbi kimepauka cheupe na unaenda kujikandika mimafuta ya mgando unang'aa
 
Nakumbuka kujaladia kaptura kupunguza makali ya fimbo, walimu wakikustukia umekwisha.
 
Tunapasuaga ingawaje kwenye interview wale wa St Joseph na St Mary wanatushinda kwa Kiingilishi, jibu tunalijua lakini ile ze makanizim ni tatizo.
Sky si kweli, tunao ndugu zetu/ watoto wetu/wajukuu zetu hawajui. Walimu wao wana mashaka na training zao. Unamhoji mwanafunzi unaona kuwa amefundishwa /hajaielewa concept. Tuna mifano, niko uswahilini, unamuuliza mtoto say kuhusu Mole concept unaona kabisa kuwa mwalimu hajafanya kazi yake. Ukienda St Mary's kama ulivyoziita unaona the clear difference!
 
Hahahhaa.. Kitambo sana.. Sie enzi hizo tulianzisha chama cha kuleta vyakula.. Bas kwenye kikundi kila mmoja akawa na zam yake.. Hapo yule aliekua mambo saf kdg zam yake ndio ilikua inasubiriwa kwa hamu sana maana analeta bites kibao.. Wengne ikifika zamu yao ni balaa.. Mara mihogo mibichi, karanga mbichi, viazi vya kuchemsha, na mambo kibao.. Maisha yale yalikua matamu sana asee. Japo tulikuwa wamoja ila walikuwepo watoto manunda hatar, ye ni mbabe tu na anataka umletee had ela ya kutumia tena kwa lazma duuuh. Tuliishi kwa umoja sana hakukua na gape la mwenye nacho na maskin.. Mpeleke mwanao Int Sch sa hiv kama huna ela ya kutosha atateseka sana aseee labda awe mafia na yeye..
 
[QUOTE="Paprika
Mama alikua hanipi hela ya kutumia (walikua hawatuzoeshi kushika pesa kabisa). Atanipikia vitu na kuniwekea kwenye lunch box na water bottle ya kamba.[/QUOTE]
Mimi hela nilikuwa napewa, maana sikuwa napikiwa na kupewa chakula kwenda nacho shule. Hata hivyo, nilianza kupewa sh.20 ile ya duara ile inafanana na sh.10. Hapo ni darasa la kwanza, mpaka la tatu.
Hiyo Sh.20 nilinunua ice cleam moja, na muhogo/andazi/kitu
mbua,n.k.....

Kuanzia la darasa la nne mpaka darasa la sita hela ya matumizi ikapanda, ikawa sh.50(hapo napata ice cleam moja na maandaz mawili saa nne, na mapumziko ya mchana napata ice cleam moja na andazi moja)

Darasa la saba ndo salio likapanda, nikawa napewa sh 100. Hapo sasa ni mwendo wa ubwabwa wa sh.50, saa nne asubuh, na saa 6:30 mchana.

Kipindi hiko hatukuzoeshwa kupewa hela, na hata ukipewa unapewa kidogo, na sio mara zote. Lakini tulikuwa tunaridhika, na maisha yakaenda. Na tulikuwa tunapendana sana, nakumbuka kwa wale wasio nacho tulikuwa tunawapunguzia ice cleam, tunagawana maandazi, tunachoteana ubwabwa, n.k
Maisha yalikuwa mazur sana, na tuliishi kwa umoja sehemu kubwa.

Yote ya yote, kubwa kuliko ilikuwa ile siku ya kumaliza mtihani wa mwisho, wa kuhitimu elimu ya msingi, hususani kwenye suala la menu, hapa watu walibeba mapocho pocho ya maana, wali, pilau, ugali, kuku, ndondo, n.k na tulishirikiana kula pamoja...unakuta mtu kaja na pilipili mfuko mzima(ile ya kaki ile inayotokana na mifuko ya saruji ya enzi zile) hafu anaweka yte kwenye wali wake wa ndondo ulioungwa kwa nazi ili ale peke yake, lkn watu tuliunga tela na kula huku tukitokwa na machozi. Acha kabisa!!!Kitu cha wali ndondo kilihusudiwa kuliko wali nyama.

Acha tu, "kila ufalme na zama zake" yale maisha tuliyafurahia sana.... Ndo hivyo wakati ni moshi, ukishatoka haurudi! Ila yale yalikuwa maisha ya upendo sana
 
Nilikuwa natembelea ndala moja aaf njiani naokota nyingne chakavu ticha akiuliza vp namwambia moja hii hapa kwnye mfuko imekatika ananisamehe kumbe yapili sina either imepotea au imechakaa.

Dah mbl kinoma
 
Nakumbuka gwaride la saa nane mchana linapigwa..... Tunaimba mtukula pole wakati mtukuka yenyewe siijui na wala sijawahifika huko..hii ni wakati wa vita ya IDD Amin Dada..... Nduli.....
Hahahahaha, propaganda za Nyerere hizo ili kujenga uzalendo.
 
Hahahahaha, propaganda za Nyerere hizo ili kujenga uzalendo.
Aisee na alifanikiwa kwelkwel... Tulikuwa wazalendo hasaaa.... Tuliipenda nchi yetu na hata viongozi wetu pia walikuwa wazalendo. Tofauti na tulionao sasa ni wazalendo njaa.... Wanahubiri amani mkononi wameshika mapanga.... Wanahubiri uzalendo mkononi wameshika kalam za kifisadi na wizi mkubwa sana.....
 
Walioko juu hawana uzalendo kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…